Pendragon24
Member
- Aug 8, 2018
- 68
- 97
Kama taifa sasa tunashuhudia kumea kwa matabaka ya chuki kati ya jamii na watu wenye itikadi kali dhidi ya wengine ambao wanaonekana kuwa inferio ndani ya nchi yao.
Wananchi ambao wanaonekana kuwa inferio ndani ya jamii wengi wao wanasumbuliwa na tatizo la uelewa mdogo kuhusu maswala mtambuka yaliyopo nchini,hivyo watu wenye nguvu hutumia mwanya huo kupora haki na kudhulumu mali za wananchi ndani jamii na kuwatisha kutumia itikadi walizonazo.
Jamii imeanza kupandikizwa mbegu za chuki na matabaka kati ya dini na dini,dhehebu na dhehebu, siasa za chuki ndani ya chama na nje, kabila moja kuonekana ni bora,masikini kukosa haki zao dhidi ya watu wenye pesa,uonevu wa kimabavu wa polisi dhidi ya raia,siasa za uzanzibari na utanganyika na matabaka kati ya viongozi na raia.
Matendo hayo yanaendelea kuchipua kati ya jamii kwa kasi kubwa sana na watu hawaoni aibu wala ukakasi kusimama mbele za watu na kuzungumza maswala ya ukabila na udini mbaya zaidi mpaka viongozi wa kidini wameingiza rasmi siasa ndani ya nyumba za ibada.
Ukuaji wa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ndio vilitegemewa hasa kuwa darasa la kuhabarisha umma namna ya kuishi kwa umoja na kutumia itikadi zilizopo kama Strength ili kujiletea maendeleo lakini baadhi ya vyombo hivyo ndio vimekuwa mstari wa mbele kuchochea chuki kati ya watu.
Haya yote yanatokea kwa sababu kizazi hiki cha sasa hakijui madhara ya matendo hayo ya kuwagawa watu katika itikadi na hakijawahi ku experience moto waliowahi kukutana nao mataifa mengine ndio maana wanachukulia kawaida tu.
Tangu unyakuo wa baba wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere mwaka 1999 bado hapajatokea kiongozi mwingine wa kisiasa na kitaifa anayepiga marufuku na kukemea vitendo hivyo hadharani bila haya na woga kwa watu wanaomzunguka.
Viongozi wengi baada yake sio tu wameshindwa kukemea maisha ya itikadi kali ndani ya jamii bali wao wenyewe wamekuwa mstari wa mbele kuchochea chuki hizo za kiitikadi kwa kuwaweka kwenye nafasi na vyeo ndugu na marafiki zao katika kabila, dini au ukanda ingawa hawastahili.
Msanii wa mziki wa kizazi kipya wa hiphop kutoka Arusha MOTRA ZE FUTURE aliwahi kuimba akisema “Nafika kwa juhudi zangu wala sio kwa ubini,undugu, kabila moja usela wala udini”
Ukiangalia viongozi wengi serikalini niwachache sana walioingia kwa juhudi na uwezo wao wa kitaaluma wengi wameingia kwa ajili ya majina yao ya ukoo,udini,ukabila,uchama au ukanda.
Wananchi wengi sana wanateseka na kudhulumiwa haki zao na watu wenye nguvu kwa sababu hawana uelewa juu ya maswala ya kijamii kuhusu sera,sheria na mienendo ya nchi hivyo uwepo wa madarasa huru ya kijamii yataweka msingi katika yote.
Sasa katika kuelekea TANZANIA TUITAKAYO ni lazima kujenge tena msingi wa uelewa ambao utasaidia watu waovu kuto kutumia milango ya kiitikadi tuliyonayo kufanikisha agenda zao.
Madarasa huru ya kijamii yatasaidia kufundisha watu kwamba kitendo cha kuwa na itikadi tofauti katika jamii si dhambi ila ni kitendo cha asili hivyo sote tunapaswa kuishi kwa mshikamano ndani ya utofauti huo.
Uanzishwaji wa madarasa huru ya kijamii yatasaidia kutoa elimu mbadala nje kabisa na elimu ya darasani, itasaidia wananchi kuelewa mabadiliko ya kiitikadi ndani ya taifa na mataifa yanayotuzunguka ili yasiweze kuleta madhara nchini.
Madarasa huru ya jamii yatawaabarisha wananchi kuwa nguvu na mamalaka yote ya serikali zinatoka kwa wananchi na hivyo wananchi wanapaswa kupewa muda wa kutosha wa kutoa maoni yao na kusikilizwa katika mijadala hii itasaidia mipango ya taifa kuto kupangwa na viongozi pekee.
Madarasa huru ya jamii yatawajengea uwezo wananchi kuto kushirikisha kabisa siasa za udini ndani ya nchi na kuwapuuza kabisa viongozi wa dini wanao hamasisha siasa za udini.
Madarasa huru ya kijamii yatasaidia kujenga upya uelewa wa wananchi juu ya haki na uhuru wa kuabudu uliopo kwa kila raia na umuhimu wa kuvumiliana kiimani, hii itasaidia watu wenye nia ovu kuto kutumia mlango huu wa dini ili kupenyeza chuki kati ya jamii.
Madarasa huru ya kijamii yatasaidia kupunguza chuki za ukabila zilizoanza kumea ndani ya watu na jamii ya kabila fulani kujiona wao ndio wanastahili kuwa ndani ya ofisi za serikali kwa kuwa wamesoma zaidi na jamii za makabila nyingine hawastahili.
Madarasa huru ya kijamii yatasaidi kuondoa ujinga wa raia wengi wanaodhani ili kufanikiwa ndani ya nchi hii ni lazima uwe na kadi ya chama fulani na ukiwa tofati basi ni muasi, watu wanapaswa kuelewa kuwa nchi hii ni yetu sote na hakuna chama au kikundi ambacho kina hati miliki ya taifa hili.
Madarasa huru ya jamii yatasaidia kuwajengea uwezo wananchi watambue kwamba rasilimali zilizopo nchini ni kwa maslai ya watu wote na wote tuna haki sawa dhidi ya rasilimali hizo na hakuna mtu mwenye haki zaidi kuliko mwingine.
Madarasa huru ya jamii yatasaidia kuwajengea uwezo raia kuhusu haki zao ili wajua mipaka ya jeshi la wananchi,jeshi la polisi na vikundi vya ulinzi shirikishi sio hali iliyopo sasa vyombo hivi vinatumia mamlaka yao nje ya sheria kuwajeruhi na kuwaumiza wananchi.
Madarasa huru ya jamii yatasaidia kutoa elimu kuhusu haki ya wananchi kukataa,kugoma na kuandamana pale wanapoona uonevu uliokisiri katika jamii dhidi ya viongozi kushindwa kutatua kero zao.
Madarasa huru ya kijamii yatasaidia wananchi kujua umuhimu wa kujiandikisha na kupiga kura ili kuchagua viongozi sahihi watakao waongoza na kwamba kitendo cha kuacha kwenda kupiga kura ni kuzidi kuwapa nafasi wanyonyaji kuharibu taifa.
Madarasa huru ya jamii yatasaidia wananchi kujua sheria za ardhi na mabadiliko yake ili kusaidia wanachi kuto kuitwa wavamizi katika maeneo yao yaliyoingiliwa na watu wa hifadhi,wawekezaji na miradi ya kiserikali.
Madarasa huru ya jamii yataongeza uelewa juu ya uamiaji na wawekezaji na vigezo vinavyotumika kumfanya mtu kuwa mwekezaji hii itasaidia kupunguza wimbi kubwa la wachina,wahindi na waarabu wanaokuja nchini na kufanya biashara za reja reja na kuajiriwa huku wazawa wakikosa nafasi.
Mwisho, wananchi hasa wanaoishi vijijini wanao toa fedha ili kuwekewa whatsapp, kutolewa pesa na wakala na wote wasio na uwezo wa matumizi ya mifumo ya kidigitali watapata kuelewesha namna sahihi ya matumizi ya mifumo hiyo kupitia madarasa huru ya jamii.

Upvote
1