SoC04 Uanzishwaji Wa Vituo Vya Marekebisho (Rehabilitation Centre) Katika Majiji Tanzania: Soluhisho la Watoto wa Mitaani na Ongezeko la Wazalishaji Mali

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Dec 8, 2019
Posts
11
Reaction score
2
Utangulizi

Ili tuifikie Tanzania tuitakayo ni muhimu kushughurikia suala la Watoto wa mtaani. Watoto wa mtaani ni Kundi la watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani, mara nyingi bila usimamizi wa watu wazima, pia mitaa wameifanya ndio sehemu ya kujipatia mahitaji yao ya kila siku ikiwemo chakula na fedha.

UN linakadiria Watoto wa mitaani kuongezeka kufikia milioni 150 duniani. Utafiti uliofanyika kuhusu watoto wa mtaani (1) ulibaini kuwa majiji 6 yenye wimbi kubwa la tatizo hili ni Dar es salaam, arusha, Tanga, Mwanza, Morogoro na Mbeya. Watoto wa mtaani hukua hadi kufikia utu uzima wakijishughurisha na shughuli za uhalifu hivyo kuhatarisha usalama wa umma. Hatua zinazochukuliwa mara nyingi zimekuwa za kurekebisha (reactive) badala ya kuzuia (preventive) (2).

Kundi hili ni moja ya makundi ya Watoto ambapo jamii na serikali bado haijawekeza rasilimali kusaidia kizazi hiki, kundi hili linasaidiwa na NGO na serikali japo hakuna njia bunifu ya kuondoa changamoto ya Watoto wa mtaani.

Kundi hili ni moja ya kundi lilotengwa na jamii mwisho wa siku huishia kupata kesi za uhalifu/ukatili na kupata makazi magrerezani baada ya kukamatwa, hivyo jamii hutazama matokeo zaidi (uhalifu, ukatili, ugaidi, wizi) badala ya kuzuia.

Kulinyanyapaa kundi hili ndio matokeo ya PANYA ROAD, lakini ukweli ni kwamba baada ya miaka 5 hadi 10 ijayo mtoto huyu atakuwa amejifunza mambo ya uhalifu/ukatili, hivyo huishia kujihusisha na uhalifu.

Watoto hawa hufanyiwa vitendo vya ukatili (Ubakaji, ulawiti, kunyanyaswa, kuumizwa), kwa sababu hakuna mtu wa kuwasemea wanaishia kubaki na matatizo yao, pia serikali haiwezi kubaini kirahisi matendo ya ukatili wanayofanyiwa.

Kundi hili kukoswa mtetezi hivyo huishia kuingizwa kwenye wimbi la utumiaji wa madawa ya kulevya, kukosa haki ya elimu, matibabu, chakula, kupigwa na kutengwa. Hatima ya kundi hili kwa Taifa huishia kuwa na vijana wategemezi na wenye kuhitaji kuhudumiwa na serikali kwa sababu ya kufungwa magerezani, kulelewa katika vituo malumu vya watumia madawa ya kulevya kwa gharama kubwa.

Sababu za Watoto kuishi mtaani

Kwa mjibu wa UNICEF limebainisha vyanzo kadhaa Pamoja na; ongezeko la ukuaji miji, umaskini uliokisiri katika familia, kuaji wa viwanda, ongezeko la watu, ongezeko la ugonjwa wa VVU/UKIMWI ambapo inapelekea vifo kwa wazazi na kuwaacha Watoto na Kutengana kwa familia.

Changamoto Kwa Watoto wa Mtaani

Watoto
hawa hupata viwango vya juu vya unyanyapaaji pia hushuku kuhesabiwa, wakiogopa kukutwa na mabaya kutokana na kuhesabiwa, hivyo hupelekea kutokuwa na idadi halisi ya Watoto wa mtaani licha ya makadirio yanayofanywa na serikali. Changamoto ni pamoja na:

  • Wana asilimia kubwa ya kuambukizwa VVU/UKIMWI ambapo ni 12.2% kuliko Watoto wengine wanaoishi kwa wazazi au walezi 4.7% (1), hii ni kwa mjibu wa utafiti uliofanyika kuhusu watoto wa mtaani.
  • Kuingia katika biashara ya ngono zembe
  • Utumiaji wa madawa ya kulevya
  • Kufanyiwa vitendo vya ukatili
  • kujihusisha katika vitendo vya uhalifu huwapelekea kuishia kuuawa na kufungwa gerezani.
  • Kupata magonjwa ya akili kwani hupata msongo wa Mawazo,
  • Kwa ujumla Watoto hawa hukoswa haki ya kupata elimu, mahitaji ya kijamii, na ueleweshwaji juu ya programu mbalimbali.
Uanzishwaji wa Vituo vya marekebisho (Rehabilitation Centre)

Ili tuweze kutatua tatizo hili linahitaji kujidhatiti kwa serikali, NGO, na wadau kwa kushirikiana kuanzisha vituo vya marekebisho katika majiji. Vituo hivi vijengwe na kuwachukua Watoto waliomtaani ili waishi hapo baada ya taratibu zote za kiserikali kufanyika na kubaini kuwa mtoto atafaa kubaki kituoni ili asaidiwe.
A1A1.jpg

Picha 1. Kituo cha Marekebisho kwa Watoto wa mtaani (Chanzo- google search)

Vituo visiwaruhusu Watoto kutoka nje ya kituo hadi pale watakapokuwa wamekidhi sifa za kuondolewa. Vituo vitoe huduma hizi:

  • Elimu ya ujuzi na ufundi: Elimu itolewe pasipo kufuata udahili maalumu wa vyuo vya ufundi, hii itasaidia kuwapa uwezo wa kuzalisha katika jamii.
  • Elimu ya afya: Vituo vitoe program mbalimbali za elimu ya afya ikiwemo elimu ya uzazi, madhara ya madawa ya kulevya usafi n.k
  • Elimu ya saikolojia: Kupitia elimu hii itawasaidia Watoto kupunguza magonjwa ya akili lakini pia kuweza kuhimili matatizo mbalimbali.
  • Elimu ya Maadili: Itasaidia kuwapa uwezo wa kuishi kama Watoto wengine waishio kwa wazazi na kuondoa kujihusisha na vitendo vya uhalifu na ukatili.
  • Elimu ya kujitegemea: Itawasaidia hata baada ya kutoka kwenye kituo na kuingia kwenye jamii watakuwa wameweza kujisimamaia na si kujingiza kuomba omba mtaani.
  • Elimu ya ujasiliamali: wafundishwe waweze kuwa wazoefu wa biashara na usimamizi wa fedha.
  • Kutoa mtaji kwa wahitimu: Mtoto atakapohitimu katika vituo, apewe mtaji kulingana na fani yake ili akajitegemee mtaani akiwa ni kijana mzalishaji.
  • Masomo ya darasani: Watoto wengi ni wenye umri wa miaka 8 na kuendelea, wapo ambao wameacha masomo yao, wawapo kituoni wapewe elimu ile ile ya darasani ili wapate haki yao.
  • Kupewa huduma ya afya bure: Kwa sababu kitakuwa ni kituo kinacholea Watoto wa mtaani, hivyo ni muhimu serikali au NGO kugharamia matibabu yao wakati wanapokuwa wameumwa.
  • Utoaji wa huduma za jamii: Watoto wahudumiwe huduma zote za kijamii.
  • A2A2.jpg

  • Picha 2: Watoto wakiwa wanakula Pamoja katika Kituo cha marekebisho cha Watoto wa mtaani (chanzo- google search)
  • Kupitia vituo hivi vitasaidia kuondoa Watoto kuwa mtaani na kulelewa sehemu moja. Ni muhimu mtoto awapo kituoni zifanyike jitihada za kuwapata wazazi au walezi, huku tukibaini zilizowapelekea kuwa mtaani. Njia hii ya vituo ni husaidia kuzuia Watoto wa mtaani na siyo kuwanyanyapaa au kuwasulubu wafanyapo maovu. Jamii isiwe mbele kushughurika na maovu yao isipokuwa kuwakinga.

Ongezeko la wazalishaji mali na kupunguza Wategemezi na magonjwa ya maambukizi Kupitia uanzishwaji wa vituo vya marekebisho

Kuifikia Tanzania Tuitakayo, Kupitia vituo hivi vitaenda kuongeza wazalishaji mali, maana kumtengeneza vizuri mtoto ndio chanzo cha kijana mwajibikaji. Vituo vitasaidia kupunguza ongezeko la magonjwa ya kuambukizwa maana watapata elimu bora na hawatahusishwa na biashara za ngono Pamoja na kupunguza uhalifu na ukatili.
Kuna haja ya kuwepo jukwaa la kusikiliza ili kujumuisha maoni ya Watoto wa mtaani, wazazi na wadau katika mikakti ya uanzishwaji wa vituo vya marekebisho pia kuanzishwa mfumo wa ushirikiano kwa kuwaleta wadau katika bodi katika uanzishwaji wa vituo ili kuongeza ufanisi endelevu wa sera ya umma na Utawala

Rejelea

1. Nyumayo S, Konje E, Kidenya B, Kapesa A, Hingi M, Wango N, Ngimbwa J, Alphonce V, Basinda N. Prevalence of HIV and associated risk factors among street-connected children in Mwanza city. PLoS One. 2022 Nov 8;17(11):e0271042.

2. Lusire L. The Effectiveness of Rehabilitation Interventions on Street Children’s Social Development in Kakamega Central Sub-County, Kenya.
 
Upvote 7
Dawa ni moja tu

Familia
Familia
Familia

Bila familia bora hao wataendelea kuwepo
 
Utangulizi

Ili tuifikie Tanzania tuitakayo ni muhimu kushughurikia suala la Watoto wa mtaani. Watoto wa mtaani ni Kundi la watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani, mara nyingi bila usimamizi wa watu wazima, pia mitaa wameifanya ndio sehemu ya kujipatia mahitaji yao ya kila siku ikiwemo chakula na fedha...
Hakika hili wazo nimelipenda sana,

Ni wazo linalopaswa kutekelezwa hakika na jamii pampja na Serikali.
.
Maua yako Mr. Paul
 
Utangulizi

Ili tuifikie Tanzania tuitakayo ni muhimu kushughurikia suala la Watoto wa mtaani. Watoto wa mtaani ni Kundi la watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani, mara nyingi bila usimamizi wa watu wazima, pia mitaa wameifanya ndio sehemu ya kujipatia mahitaji yao ya kila siku ikiwemo chakula na fedha.

UN linakadiria Watoto wa mitaani kuongezeka kufikia milioni 150 duniani. Utafiti uliofanyika kuhusu watoto wa mtaani (1) ulibaini kuwa majiji 6 yenye wimbi kubwa la tatizo hili ni Dar es salaam, arusha, Tanga, Mwanza, Morogoro na Mbeya. Watoto wa mtaani hukua hadi kufikia utu uzima wakijishughurisha na shughuli za uhalifu hivyo kuhatarisha usalama wa umma. Hatua zinazochukuliwa mara nyingi zimekuwa za kurekebisha (reactive) badala ya kuzuia (preventive) (2).

Kundi hili ni moja ya makundi ya Watoto ambapo jamii na serikali bado haijawekeza rasilimali kusaidia kizazi hiki, kundi hili linasaidiwa na NGO na serikali japo hakuna njia bunifu ya kuondoa changamoto ya Watoto wa mtaani.

Kundi hili ni moja ya kundi lilotengwa na jamii mwisho wa siku huishia kupata kesi za uhalifu/ukatili na kupata makazi magrerezani baada ya kukamatwa, hivyo jamii hutazama matokeo zaidi (uhalifu, ukatili, ugaidi, wizi) badala ya kuzuia.

Kulinyanyapaa kundi hili ndio matokeo ya PANYA ROAD, lakini ukweli ni kwamba baada ya miaka 5 hadi 10 ijayo mtoto huyu atakuwa amejifunza mambo ya uhalifu/ukatili, hivyo huishia kujihusisha na uhalifu.

Watoto hawa hufanyiwa vitendo vya ukatili (Ubakaji, ulawiti, kunyanyaswa, kuumizwa), kwa sababu hakuna mtu wa kuwasemea wanaishia kubaki na matatizo yao, pia serikali haiwezi kubaini kirahisi matendo ya ukatili wanayofanyiwa.

Kundi hili kukoswa mtetezi hivyo huishia kuingizwa kwenye wimbi la utumiaji wa madawa ya kulevya, kukosa haki ya elimu, matibabu, chakula, kupigwa na kutengwa. Hatima ya kundi hili kwa Taifa huishia kuwa na vijana wategemezi na wenye kuhitaji kuhudumiwa na serikali kwa sababu ya kufungwa magerezani, kulelewa katika vituo malumu vya watumia madawa ya kulevya kwa gharama kubwa.

Sababu za Watoto kuishi mtaani

Kwa mjibu wa UNICEF limebainisha vyanzo kadhaa Pamoja na; ongezeko la ukuaji miji, umaskini uliokisiri katika familia, kuaji wa viwanda, ongezeko la watu, ongezeko la ugonjwa wa VVU/UKIMWI ambapo inapelekea vifo kwa wazazi na kuwaacha Watoto na Kutengana kwa familia.

Changamoto Kwa Watoto wa Mtaani

Watoto
hawa hupata viwango vya juu vya unyanyapaaji pia hushuku kuhesabiwa, wakiogopa kukutwa na mabaya kutokana na kuhesabiwa, hivyo hupelekea kutokuwa na idadi halisi ya Watoto wa mtaani licha ya makadirio yanayofanywa na serikali. Changamoto ni pamoja na:

  • Wana asilimia kubwa ya kuambukizwa VVU/UKIMWI ambapo ni 12.2% kuliko Watoto wengine wanaoishi kwa wazazi au walezi 4.7% (1), hii ni kwa mjibu wa utafiti uliofanyika kuhusu watoto wa mtaani.
  • Kuingia katika biashara ya ngono zembe
  • Utumiaji wa madawa ya kulevya
  • Kufanyiwa vitendo vya ukatili
  • kujihusisha katika vitendo vya uhalifu huwapelekea kuishia kuuawa na kufungwa gerezani.
  • Kupata magonjwa ya akili kwani hupata msongo wa Mawazo,
  • Kwa ujumla Watoto hawa hukoswa haki ya kupata elimu, mahitaji ya kijamii, na ueleweshwaji juu ya programu mbalimbali.
Uanzishwaji wa Vituo vya marekebisho (Rehabilitation Centre)

Ili tuweze kutatua tatizo hili linahitaji kujidhatiti kwa serikali, NGO, na wadau kwa kushirikiana kuanzisha vituo vya marekebisho katika majiji. Vituo hivi vijengwe na kuwachukua Watoto waliomtaani ili waishi hapo baada ya taratibu zote za kiserikali kufanyika na kubaini kuwa mtoto atafaa kubaki kituoni ili asaidiwe.
View attachment 3030184
Picha 1. Kituo cha Marekebisho kwa Watoto wa mtaani (Chanzo- google search)

Vituo visiwaruhusu Watoto kutoka nje ya kituo hadi pale watakapokuwa wamekidhi sifa za kuondolewa. Vituo vitoe huduma hizi:

  • Elimu ya ujuzi na ufundi: Elimu itolewe pasipo kufuata udahili maalumu wa vyuo vya ufundi, hii itasaidia kuwapa uwezo wa kuzalisha katika jamii.
  • Elimu ya afya: Vituo vitoe program mbalimbali za elimu ya afya ikiwemo elimu ya uzazi, madhara ya madawa ya kulevya usafi n.k
  • Elimu ya saikolojia: Kupitia elimu hii itawasaidia Watoto kupunguza magonjwa ya akili lakini pia kuweza kuhimili matatizo mbalimbali.
  • Elimu ya Maadili: Itasaidia kuwapa uwezo wa kuishi kama Watoto wengine waishio kwa wazazi na kuondoa kujihusisha na vitendo vya uhalifu na ukatili.
  • Elimu ya kujitegemea: Itawasaidia hata baada ya kutoka kwenye kituo na kuingia kwenye jamii watakuwa wameweza kujisimamaia na si kujingiza kuomba omba mtaani.
  • Elimu ya ujasiliamali: wafundishwe waweze kuwa wazoefu wa biashara na usimamizi wa fedha.
  • Kutoa mtaji kwa wahitimu: Mtoto atakapohitimu katika vituo, apewe mtaji kulingana na fani yake ili akajitegemee mtaani akiwa ni kijana mzalishaji.
  • Masomo ya darasani: Watoto wengi ni wenye umri wa miaka 8 na kuendelea, wapo ambao wameacha masomo yao, wawapo kituoni wapewe elimu ile ile ya darasani ili wapate haki yao.
  • Kupewa huduma ya afya bure: Kwa sababu kitakuwa ni kituo kinacholea Watoto wa mtaani, hivyo ni muhimu serikali au NGO kugharamia matibabu yao wakati wanapokuwa wameumwa.
  • Utoaji wa huduma za jamii: Watoto wahudumiwe huduma zote za kijamii.
  • View attachment 3030182
  • Picha 2: Watoto wakiwa wanakula Pamoja katika Kituo cha marekebisho cha Watoto wa mtaani (chanzo- google search)
  • Kupitia vituo hivi vitasaidia kuondoa Watoto kuwa mtaani na kulelewa sehemu moja. Ni muhimu mtoto awapo kituoni zifanyike jitihada za kuwapata wazazi au walezi, huku tukibaini zilizowapelekea kuwa mtaani. Njia hii ya vituo ni husaidia kuzuia Watoto wa mtaani na siyo kuwanyanyapaa au kuwasulubu wafanyapo maovu. Jamii isiwe mbele kushughurika na maovu yao isipokuwa kuwakinga.

Ongezeko la wazalishaji mali na kupunguza Wategemezi na magonjwa ya maambukizi Kupitia uanzishwaji wa vituo vya marekebisho

Kuifikia Tanzania Tuitakayo, Kupitia vituo hivi vitaenda kuongeza wazalishaji mali, maana kumtengeneza vizuri mtoto ndio chanzo cha kijana mwajibikaji. Vituo vitasaidia kupunguza ongezeko la magonjwa ya kuambukizwa maana watapata elimu bora na hawatahusishwa na biashara za ngono Pamoja na kupunguza uhalifu na ukatili.
Kuna haja ya kuwepo jukwaa la kusikiliza ili kujumuisha maoni ya Watoto wa mtaani, wazazi na wadau katika mikakti ya uanzishwaji wa vituo vya marekebisho pia kuanzishwa mfumo wa ushirikiano kwa kuwaleta wadau katika bodi katika uanzishwaji wa vituo ili kuongeza ufanisi endelevu wa sera ya umma na Utawala

Rejelea

1. Nyumayo S, Konje E, Kidenya B, Kapesa A, Hingi M, Wango N, Ngimbwa J, Alphonce V, Basinda N. Prevalence of HIV and associated risk factors among street-connected children in Mwanza city. PLoS One. 2022 Nov 8;17(11):e0271042.

2. Lusire L. The Effectiveness of Rehabilitation Interventions on Street Children’s Social Development in Kakamega Central Sub-County, Kenya
imekaa sawa
 
Bandiko zuri.
 
Back
Top Bottom