SoC04 Uanzishwaji wa viwanda vya msingi kwa kila kaya kulingana na malighafi zinazopatikana katika kanda ili kujenga uchumi imara kwa kila Mwananchi

SoC04 Uanzishwaji wa viwanda vya msingi kwa kila kaya kulingana na malighafi zinazopatikana katika kanda ili kujenga uchumi imara kwa kila Mwananchi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Llny

New Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Viwanda vya Msingi ni viwanda vidogo vidogo vinavyofanya uchakataji wa malighafi mbalimbali ili kuleta bidhaa katika soko.

Mwananchi anapowezeshwa kumudu kuanzisha kiwanda kidogo nyumbani itapelekea kumudu gharama za maisha, kuikwamua familia na umasikini pia kurithisha familia ujuzi hivyo kupunguza umasikini katika familia.

Kutoa fursa za wananchi kuanzisha viwanda vidogo majumbani pia kutapunguza idadi ya Vijana kukimbilia mjini kutafuta ajira maana atakuwa ameshapata ujuzi wa kutosha na kupunguza muda wa kwenda kukaa kwenye magenge mbalimbali yatakayomchagiza kuwa na akili ya kuajiriwa.

Kuwepo na mpango wa kila Mkoa, Wilaya , Kata, kijiji na kaya ni mazao au malighafi gani zitakazochakatwa ili kuwepo na dira nzuri ya kwa kila mwananchi katika kujiandaa na Tanzania ya viwanda.

Kutolewa kwa elimu itakayowawezesha raia kuanzisha viwanda vidogo ili kuwa na zao moja wapo katika uzalishaji. Mfano viwanda vya kuchakata karanga kupata siagi mkoani Dodoma. Pia viwanda vidogo vya uchakataji wa zabibu kupata mvinyo. Hilo litapunguza uagizaji wa bidhaa hizo nje.

Kuandaa wataalam wa kutoa mafunzo juu ya uandaaji wa nishati mbadala mfano biogas ili iweze kupunguza gharama za uendeshaji wa viwanda hivi vidogo maana wataweza kuzalisha nishati ya gesi na nishati ya umeme.

Kuchukua takwimu sahihi za kila uzalishaji na kuwajengea uwezo katika suala la kuongeza thamani ya bidhaa kuanzia kwenye maandalizi ya bidhaa hadi kwenye hatua ya kufungasha.

Kuunganisha masoko mtandao kwa kila watengenezaji kwa kuzingatia aina za bidhaa ili kufanya usambazaji katika nchi nzima kwanza kwa kuzingatia utozaji mdogo wa kodi.

Kutoa nafasi ka wafanyabiashara wakubwa kuanzisha viwanda ili kununua malighafi kwa wajasiriamali kisha kuongeza thamani na kupeleka bidhaa nje ya nchi kwa kutoka kodi za kawaida ili kukuza pato la wanachi hadi pato la Taifa.

Kuweka utaratibu wa kutoka kodi kubwa kwa bidhaa zinazoingia nchini na hasa kama zinapatikana hapa nchini.
Serikali kuweka usimamizi wa karibu katika kuanzia kwenye sensa ya malighafi zinazotarajiwa kupatikana mfano mazao, madini na malighafi nyingine maana hapa ndipo mapato ya serikali yatakapoanzia.

Serikali kuandaa mpango kazi madhubuti ili kuhakikisha wananchi wanaweza ili kuiwezesha nchi katika tozo na kodi mbalimbali.

Serikali kuandaa wataalam wa kutosha ikiwemo kuandaa makundi mbalimbali yatakayoweza kuwezesha Jamii kwa njia ya semina na vipindi vya televisheni na redio ili elimu iwafikie wananchi kwa gharama ndogo na kwa wakati mmoja eneo kubwa mfano kuwepo na kipindi cha uchakataji wa mazao na malighafi mbalimbali ili kila mwananchi achague kile anachoona Ana uwezo wa kuanza nacho napiga namna ya kuongeza thamani katika bidhaa.

Serikali kuazisha maduka yake ya viongeza thamani vilivyothibitishwa kimataifa na kuwauzia wananchi kwa gharama Nafuu ili uzalishawaji uwe wenye kulinda afya ya walaji.

Serikali kuongeza nguvu katika taasisi za TBS na TFDA pia TMDA na nyingine zenye kuthibiti ubora ili wananchi wafanye kazi kwa uaminifu na uzalishaji wenye kuzingatia Sheria na kanuni za nchi na za kimataifa.

Serikali kuandaa timu ya wataalam wa afya kutoa elimu juu ya uandaaji bora wa bidhaa za vyakula ndio utaandaa Taifa lenye afya hivyo kulifikia lengo la Taifa linalotakiwa.

Serikali kuingia makubaliano na nchi za afrika zenye uhaba wa chakula na bidhaa zitakazozalishwa nchini kuuziwa bidhaa hizo na wafanyabiashara waliosajiliwa ili kudhibiti mapato ya nchi Maana sensa itakayofanyika itasaidia nchi kwa na takwimu ya mazao na bidhaa zote zinazozalishwa kwani serikali ndiye muuzaji wa viongeza ubora.

Kuanzishwa kwa maduka ya serikali ambayo yatakuwa yananunua malighafi zilizobaki na kuzitunza katika maghala kisha kuuza nje ya nchi.

Serikali kuanzisha viwanda vikubwa na kuwajengea vijana uwezo wa kuviendesha lakini pia kutumia nguvukazi ya wafungwa, wanafunzi wanaopita katika jeshi kwa mujibu wa Sheria.

Serikali kuanzisha miradi katika shule za msingi na sekondari ili kujenga kizazi kinachopenda kazi za mikono kama kilimo, ufugaji, na ufundi mbalimbali.

Kutunga sera zitakazowabana wabadhirifu wa Mali za umma na kutoa adhabu kali mara moja.

Unapoikomboa familia basi umeikomboa nchi elimu ya vitendo hudumu kuliko elimu ya nadharia maana hasa ya sentensi hii ni kwamba tuanzishe viwanda majumbani ili kila mtoto arithi ujuzi na hata mzazi akimuacha basi mtoto huyu ataweza kuendeleza maana alikua anashiriki vema na amejifunza kwa vitendo hapo tutakua tueliandaa taifa lenye nguvu na lisilo tetereka kiuchumi hata mzazi akiondoka. Naipenda Tanzania mpya na kwa kufanya haya basi tutakuwa kwenye Tanzania tunayoitaka Asante.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom