Ubabe vyuo vikuu

Ubabe vyuo vikuu

Soccrates

New Member
Joined
Aug 6, 2012
Posts
4
Reaction score
0
Hivi kwanini kila serikali za wanavyuo zinapochaguliwa na wanachuo wenyewe kwa nini utawala hupenda kuingilia kati maamuzi ya wanachuo kuleta uvunjifu wa amani vyuoni..Mfano UDSM, LUKO, TEKU...Kulikoni?
 
Hii inasababishwa na serikali isiyojiamini. Kwa Tanzania serikali iko kuwanyonya wananchi badala ya kuwatumikia. Tuliosoma kwa mfano UDSM tunalijua sana hili hasa wakati wa chama kimoja na baada ya kuja marais vilaza. Hii inasababisha na kuvunja mioyo ya wanafunzi. Kwa tuliosoma pale na baadaye nje ya nchi tunaona tofauti kati ya utawala wa vyuo vyetu. Bado baadhi ya maprofesa wana hang overs za ukoloni wakipenda kufelisha hata kuwatoa rushwa hasa ya ngono wanafunzi. Dunia imebadilika sharti tubadilike.
 
Sasa huu ni ubabe! Au ujinga na ufinyu wa utawala wenye akili mgando! For udom mlacha ni panya kama walivyo panya wengine! Ndo mana wakati wetu tulimtia vdole huyo mzee!
 
hivi bado kuna serikali za wanavyuo? au zimefufuliwa lini?
 
Hivi kwanini kila serikali za wanavyuo zinapochaguliwa na wanachuo wenyewe kwa nini utawala hupenda kuingilia kati maamuzi ya wanachuo kuleta uvunjifu wa amani vyuoni..Mfano UDSM, LUKO, TEKU...Kulikoni?

mtoa mada umesahau kutaja UDOM chuo ambacho kinaongozwa na vilaza, akina mlacha, makangara ambao wamefanya chuo kama chakifamilia, wamefukuza wanafunzi ambao walikuwa wanadai haki yao ya kupata mafunzo kwa vitendo toka july mwaka jana mpaka sasa wapo kitaa. inasikitisaha sana
 
Sasa huu ni ubabe! Au ujinga na ufinyu wa utawala wenye akili mgando! For udom mlacha ni panya kama walivyo panya wengine! Ndo mana wakati wetu tulimtia vdole huyo mzee!
unamaanisha nini hapo kwenye red???
 
mtoa mada umesahau kutaja UDOM chuo ambacho kinaongozwa na vilaza, akina mlacha, makangara ambao wamefanya chuo kama chakifamilia, wamefukuza wanafunzi ambao walikuwa wanadai haki yao ya kupata mafunzo kwa vitendo toka july mwaka jana mpaka sasa wapo kitaa. inasikitisaha sana

Tatizo kubwa ninaloliona itikadi za vyama vimeathiri serikali halali za vyuo, wanatakiwa waelewe, serilkali hizi ni kama micro training ambazo husaidia watu kama akina Obama kujitokeza na kuleta mageuzi..lets unite and fight for our own rights..maisha mema kwa wale wote waliofukuzwa kwa ajili ya wengine, big up sana!
 
Back
Top Bottom