Ubabe wa TRA, ugumu wa biashara na utitiri wa kodi; nini kifanyike?

Mnyororo wa rushwa ni mrefu sana.. Senior officers/Managers wa leo walikuwa juniors miaka 10 iliopita..vivo hivyo Commisdioners na deputies..

Chukua chako mapema.. Mfumo wa kulindana mwanzo mwisho..

Mabadiriko yanawezekana..Hakuna lisilowezekana
Kama wananchi hawajui haki zao dawa yao ni kuwabambika kodi zaidi
 
Tulilaumu bunge kwa kutunga sheria za kipumbavu. Wabunge ambao hawajasoma tuwapige chini kwasababu wanachangia bunge kuwa kama rubber stamp tu.
 
TRA waongeze kiwango cha kodi mpk tupate akili
Duh

Wenye ufahamu ni wakati wa kufanya maamuzi ya kuingia kwenye Ulingo wa kuijenga nchi kupitia vyombo vya maamuzi..

Lakini Kwa uzalendo mkubwa tusisite kukosoa na kushauri Kwa stays kupitia majukwaa Kama haya..

Hatupaswi kuishia kulalamika kwenye mitandao na kuwaachia wasio na uwezo wa kuona mbali (Waliochoka kifikra,mbinu) wakifanya maamuzi au kutunga sheria wasizojua athari zake Kwa Taifa na kuishia kudumaza maendeleo endelevu..
 
Hata ukikosoa kwani wana sikia?
 
Kama wananchi hawajui haki zao dawa yao ni kuwabambika kodi zaidi

Si sawa ndugu

Kwa faida ya nani?

Ili iweje?

Tunajenga au kubomoa?

Tutakopa na kupewa misaada mpaka lini ?mchele/Kondomu/Vyandarua/Magari/Manunuzi ya dawa…

Tumepata uhuru lini?Nini faida ya uhuru?Lini tutajitegemea..
 
Hata ukikosoa kwani wana sikia?

Wanayo masikio tena makubwa..

Yamkini kuna ganzi tu..

Tufanye dua,Sara,Toba,Maombi Kwa ajili ya mioyo Yao kufunguliwa na kutenda Kwa haki,Hofu ya Muumba,Weredi..

Siku Za mwanadamu hapa duniani zinahesabika..Hatuishi milele..Tutatoa hesabu ya matendo yetu..Nafasi zetu..Historia zitatuhukumu/Zitawahukumu..

Wema na haki haviozi..Mwisho wa ubaya-Aibu
 
Shida ni nani wa kumfunga nani kengere,kila mtu anataka green light katika maisha,kila mtu anataka maisha murua,Kazi iendelee

Tusichoke kusema Kwa nia njema..
Tusichoke kukemea pasipo kuonea
Tusichoke kushauri hata tukipuuzwa
Tusichoke kutumia baraka ya ufahamu kidogo kusaidia wengine wasioweza
Kila lenye mwanzo Lina mwisho..

Never Give Up💪🏿
 
TRA wanaweza nifanya nikatoa hela yangu kwenye uwekezaji bongo, niende nikatafute maisha hata Zambia mwakani
 
Ikiwa kuna mtumishi TRA haweki chake kwanza na mapato ya serikali baadae basi labda itakua ni asilimia moja tu..
Na kuna mfumo wa walaji wanashirikuana kuto chini hadi ngazi ya juu wako kazini kugawana chao.
Huwa sipati jibu hawa TAKUKURU nini wanafanya? Ikiwa mambo ya rushwa na ubadhirifu uko wazi hivi
 
TRA wanaweza nifanya nikatoa hela yangu kwenye uwekezaji bongo, niende nikatafute maisha hata Zambia mwakani

Usiwe mwepesi wa hasira

Nchi inakutegemea

Mwenyezi Mungu kakujalia alichokujalia ili ufanyike baraka kwa mamilioni ya maskini wa nchi hii..

Tuna tatizo kubwa la ajira..Influx ya graduates ni kubwa mnoo kwenye soko..Absorption ni ndogo mnoo..

Mliopata neema ya kujenga mitaji na biashara ni wachache mnoo ktk taifa..Nchi inawategemea sana hata Kama kuna wapumbavu wachache wasiojua thamani yenu na kutamani mfirisike na kurudi kwenye umaskini..

Tuendelee kupiga kelele kuomba hekima,busara na huruma ya waliojaariwa kupewa madaraka na Mwenyezi warekebishe kasoro..

Hakuna lisilowezekana..Hata Mbuyu ulianza Kama mchicha..Nina Imani wakubwa wana mtazamo na fikra tofauti..

NEVER EVER EVER GIVE UP!
 

Mfumo ni kitu Complex
Mfumo wa hewa,damu,fahamu
Watumishi wengi wa TRA ni mfumo..Kuna watoto wa Wakulima,Wafugaji,wafanyakazi(TRA,Wanasiasa,Vigogo wastaafu,Watumishi waandamizi,etc)..Nani anatamani mwanae apate kazi isio na makandokando ya mapato..

Mshahara wa Baba/Mama milioni 5 lakini anamoriki Mali Za Bilioni 30..Kwa nini Mtoto asitamani kufanya kazi anayofanya baba/mama? Report Za Rushwa zinaonyesha wazi taasisi zinazoongoza Kwa rushwa..Polisi/Mahakama/TRA..etc..Nini kinafanyika

Mkuu wa Takukuru ni Afisa Mwandamizi wa Polisi.Kachero mbobevu haswaa...Hakuna asichojua kuhusu michakato/mizizi ya rushwa ktk nchi..Inshu ni je akisema aishughurikie rushwa kisawasawa unadhani atapona?..Atagusa Familia,Marafiki,Ndugu na Jamaa wa vigogo..Zitalipuka fitina,Shutuma..Skendo..mwisho atatumbuliwa..Tatizo Lipo kwenye Katiba..Kuna vyeo vinapaswa kulindwa kikatiba sio kwa utashi wa wanasiasa.
 
Wafanyabiashara na wenye viwanda wanapaswa kulipa kodi stahili kwa uhai wa Taifa letu.

Kodi zinazolipwa zinapaswa kutumika vema,Kulindwa na kusimamiwa vema na si kufujwa.

Mchakato wa kukusanya kodi stahili unapaswa kufanyika kwa kuzingatia uhalisia wa kibiashara na kulinda mazingira bora ya uendelezaji wa biashara.

Wigo wa walipa kodi bado ni mdogo mnoo ukizingatia idadi ya raia wa nchi ama wanufaika wa matunda husika.

Tunakopa kufadhiri miradi lukuki..Tutalipa,Lazima tulipe..Kwa miaka mingi ijayo..Lazima tukuze shughuri mbalimbali za kiuchumi sasa na baadae..

Hatupaswi kuua biashara kwa msingi wa kukusanya mapato ili kuvunja rekodi..Hatupaswi kunyanyasa wafabiashara na wenye viwanda kwa kivuli cha kufurahisha wanasiasa..Hatupaswi kuziba masikio lundo la biashara likifa kwa sababu ya ukatiri wa maafisa kodi..

Dunia inapita ktk changamoto nyingi za kibiashara kimataifa..Tujifunze na kuchukua hatua stahiki kuchukua hatua stahiki kulinda sekta binafsi na wenye viwanda..

TUACHE:-
UBABE
KIBURI
DHARAU
UKATIRI
 
Umeongea vyema, TRA ni wavivu kwa kutoongeza wigo wa wafanyabiashara badala yake wanawagagania walewale wa miaka nenda miaka rudi mfano ni lini uliona wamiliki wa shule wanalalamika kuhusu kodi, je kipato chao ni kidogo? Je ni lini uliwahi kuona wamiliki wa gereji wanalalamika kuhusu kodi je kipato chao ni kidogo? Wapo wajasilia mali kibao wa hivyo lkn hawaguswi na TRA badala yake utagaganiwa wewe uliyefungua kifrem cha nguo au stationery au kiduka flani ndio unaonekana unahela nyingi.
 
Mlipa kodi si adui
Mlipa kodi ni development partner
Mlipakodi ni mdau wa thamani pana
Mlipakodi ni mdau wa mapato leo,kesho na mtondogoo
Mlipakodi sio jambazi,Mwizi,Taperi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…