Tetesi: Ubadhilifu wa pesa unaofanywa na Mwenyekiti wa Bodi katika shule ya Sekondari Buluba mkoani Shinyanga

Tetesi: Ubadhilifu wa pesa unaofanywa na Mwenyekiti wa Bodi katika shule ya Sekondari Buluba mkoani Shinyanga

mogesogwe

Member
Joined
Mar 17, 2017
Posts
65
Reaction score
29
Habari za mwaka mpya wanaJF!

Awali ya yote nimpongeze Rais Magufuli kwa uchapakazi wake uliotukuka na kuwa Rais wa Mfano Afrika. Pia Rais wetu amekua mstari wa kupambana na rushwa katika taifa letu ili kuleta usawa.

Kimsingi hoja hapa baada ya pongezi kwa kiongozi wetu wa nchi, niende kwenye hoja mahususi:
Buluba ni shule ya pili kwa ukongwe mkoani Shinyanga, ikiwa inamilikiwa na SHIRECU (1984) Ltd imepita vipindi tofauti tofauti!

Hadi Mei mwaka wa Jana ambapo yalifanyika mabadiliko makubwa na kumpata Mwenyekiti wa bodi kijana, Richard Luhende ambaye aliahidi kuboresha Ushirika pamoja na shule ya sekondari ya Buluba kwa kuanzisha ofisi ya meneja wa shule ambayo awali haikuwepo!

Mambo yageuka kilio baada ya Richard Luhende mwaka wa bodi na rafiki yake Maduhu Nkamakazi kuchota kiasi cha million sitini na ushee pesa ya kitanzania.

Pesa hizo zinajumuisha ada ya mitihani ya wanafunanzi kidato cha pili 2018 na kidato cha NNE 2018. Ada ya mitihani waliokula inakadriwa kuwa million tano! Hivyo ada ya mitihani ambayo imekwisha fanyika haijalipwa.

Luhende na wenzake wameisababishia shule hasara ya million 116 baada ya kuwafukuza walimu 8 ambao walienda kutafuta haki mahakamani!

Wito kwa mamlaka husika ya kusimamia Elimu na vyama vya ushirika nchini kuchukua hatua!
Wizara za TAMISEMI na ELIMU zimshauri Mh. Rais achukue Buluba iwe ya Serikali ili iendelee kutoa huduma kwa Watanzania wote!

TAKUKURU iwahoji Luhende na Rafiki yake Nkamakazi werejeshe pesa za shule!

Mwanaharakati!
Karibu sana mwaka 2019
 
HUYO LUHENDE ATAKUWA AMEKUFUKUZA KAZI WEWE MWALIMU. UMEKUJA HUKU KUMHARIBIA TU.
1.HELA YA MITIHANI INALIPWA KWENYE AKAUNTI YA BARAZA YAANI NECTA MOJA KWA MOJA, ANGEKULA HAO WATOTO WASINGERUHUSIWA KUFANYA MTIHANI.
2.HIZO HELA NYINGINE HUJATHIBITISHA WAMEKULAJE.
3.KAJIFUNZE MAANA HALISI YA UTAKATISHAJI WA FEDHA. HAO JAMAA NI WADOKOZI WA HELA ZA SHULE WALA USIWAPE KIKI.
 
"Amechota ada za mitihani ya wanafunzi wa kidato cha pili na cha nne".
Ina maana wanafunzi wameshindwa kufanya mitihani ya taifa? Ninachojua ada ya mitihani ya taifa inaenda baraza la mitihani. Naomba kueleweshwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ada ya mitihani si ilifutwa?.

Kila kitu afanye mr. President?. Huko hamna viongozi?. Acha kimbele mbele na kisebusebu.
Umbea waachie wazaramo, haipendezi kijana wa kisukuma na mwili mkubwa kuwa mbea mbea. Hebu kachunge huko.
 
Back
Top Bottom