Ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi ya Hifadhi ya Ngorongoro

Ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi ya Hifadhi ya Ngorongoro

BITALA

Member
Joined
Jan 10, 2015
Posts
26
Reaction score
26
Mheshimiwa Rais shikamoo,

Awali ya yote nikupongeze sana kwa kazi nzuri unayoifanya ya kulijenge Taifa letu. Hongera sana na Mwenyezi Mungu aendelee kukupa nguvu na ujasiri kulifikisha taifa hili kwenye nchi ya Kaanan.

Pamoja na juhudi kubwa unayoifanya ila bado kuna Watanzania wachache ambao ni watumishi wa umma hawataki kukuelewa wewe pamoja malengo yako chanya ya kujenga nchi hii.

Kwa kuwa huwezi kufika kila mahali sisi tumeendelea kuwa watu ambao tunakupa taarifa zozote zinazoonekana kuzorotesha mahusiano baina ya watumishi wa umma ama zenye harufu ya ufisadi. Naomba niendelee kukupa taarifa zinazohusu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kama inavyojieleza hapa chini:

UOZO WA KUTISHA KATIKA IDARA YA UTUMISHI KWENYE TAASISI HII YA UMMA

Mheshimiwa Rais, idara hii imeoza haifai kabisa na kama nilivyosema awali uwezo mdogo wa mkuu wa idara Bw. Ntunga ndiyo chanzo cha migogoro na kunyima watumishi stahiki zao za msingi. Ajira zimekuwa za upendeleo sambamba na mishahara isiyoendana na elimu na uzoefu za watumishi husika. Baadhi ya maofisa wa idara hii wamekuwa wakijihusisha na utoaji wa ajira kwa kupewa hongo ya pesa pamoja na ngono. Mfano yupo mtumishi mmoja anayeitwa Carlos Mbiro ambaye anajimwambafy na kujiona yeye ana mamlaka makubwa kuliko mkuu wa hifadhi hiyo.

Mtumishi huyu ameshafanya mambo mengi sana ya hovyo lakini hakuna hatua zozote alizochukuliwa. Mfano, alianza kwa kutoa ajira ya upendeleo kwa watumishi wa kike ambao ni wafanya usafi alionao kwenye mahusiano ya mapenzi na alisababisha kutokea ugomvi mkubwa baina ya watumishi hawa na kupelekea kuzorota kwa ufanisi.

Changamoto hizi zilifikishwa kwenye kikao cha ajira na nidhamu akaonywa na kuahidi hatorudia kosa. Kama ilivyo ada, sikio la kufa halisikii dawa baada ya hapo alimfanyia mpango mdogo wake na kumpa maswali ya usaili na kupelekea kufaulu kwa kiwango kilichowastua wengi ambapo ilibidi aitwe tena akaonywa na kuahidi kutorudia kosa.

Haikuchukua muda mrefu akaja kufuta ajira ya mtumishi mmoja wa Idara ya Utalii na kumuajiri mpenzi wake bila kufuata utaratibu halali wa vikao pamoja na kutomshirikisha mkuu wa taasisi. Ila kwa busara za menejimenti ajira ya mwanamke yule ilifutwa na mtumishi aliyefukuzwa akarudishwa kazini.

Vilevile, ameajiri watumishi wasiokuwa na sifa mfano wako watumishi watatu waliotoka timu ya mpira ya Geita Gold Mining (majina yao nimeyahifadhi) walioajiriwa Idara ya Uhifadhi kwa kigezo cha kucheza mpira. swali la kujiuliza, je malengo ya hifadhi hii yamebadilika kutoka kwenye uhifadhi mpaka michezo? Unaacha kuajiri watu wenye sifa stahiki unatumia vigezo vya kitoto visivyo na manufaa na hifadhi.

Hakuishia hapo, wiki mbili zilizopita kijana huyu mpenda ngono aliamua kutoa tangazo la ajira la Afisa Utumishi Mwandamizi kwa masharti awe mwanamke bila ridhaa ya mkuu wa taasisi wala kikao chochote cha menejimenti. Jinsi alivyo mpumbavu alipoulizwa na mkuu wake wa idara alikiri ni kweli alifanya hivyo kwa maelekezo ya uongozi wa juu bila kuweka wazi. Swali la kujiuliza, je ni uongozi gani huo unaomzidi Dr. Manongi?

Cha ajabu zaidi menejimenti yote imekiri kutokuwa na taarifa wala haikutoa baraka ya tangazo hilo. Sasa swali la kujiuliza, je alifanya hivyo akiwa hajui taratibu halali za kutangaza ajira? Ni watumishi wangapi wameshanyanyasika kwa ajili ya upuuzi wa kijana huyu? Dr Manongi na menejimenti yako, kwanini mnaruhusu hali kama hii ijitokeze na nyie mmekaa kimya tu?

Mnajipambanua mmeingia kwenye jeshi usu, mbona mmelegea kama mlenda? Wakaguzi wa ndani mnafanya nini hapo kwenye shirika au na nyie ni sehemu ya wanaofaidika na maovu haya? Nawakumbusha tena timizeni majukumu yenu bila kumuonea mtu maana mkiendelea kufumbia macho upuuzi kama huu ipo siku mtawajibishwa.

Kijana huyu amegeuza taasisi hii ni danguro kwamba mwanamke yeyote mpenzi wake anamuajiri. Cha kushangaza zaidi, boss wake Bw. Ntunga anamuombea msamaha akijua kabisa kijana huyu hawezi kubadilika maana ni mara ya nne anarudia makosa na jinsi ilivyo inawezekana kabisa boss wake Ntunga anajua hili ndiyo maana anamtetea na kumpa kiburi?

Profesa Kaswamila, Dr. Manongi na menejimenti yako naomba mtende haki. Acheni double standards zisizo na tija na kuleta majonzi kwenye mioyo ya watu, mtumishi huyu amepoteza credibility ya kuendelea kuwa kwenye idara hii nyeti. Huyu mpuuzi amekuwa ni tatizo kwenye idara hii ndiyo shida ya kuchukua watumishi kupitia viti maalumu.

Nakumbuka mlimchukulia hatua Bw. Fabian Budodi kwa kumuhamishia Kasulu kwa kosa la kumuonea eti kuajiri bila kufuata utaratibu, kwanini huyu msimchukulie hatua na ametenda kosa hilo zaidi ya mara moja? Ntunga unamtetea kwa kuwa unajua wewe ni kilaza ili akufichie mapungufu yako? Hifadhi ya Ngorongoro sio shamba binafsi la mbaazi ni shirika la umma. TAKUKURU naomba mumsadie Mheshimwa Rais kwa kufuatilia mambo haya maovu yasiyo na maana kwa taasisi hii. Kwa kuanzia ombeni list ya wafanyakazi wote walioajiriwa kuanzia mwaka 2017 mpaka 2019, mafaili yao pamoja na payroll mjionee madudu waliyoyafanya watumishi hawa then ikithibitika sheria ichukue mkondo wake kwa watumishi hawa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Nimepata taarifa wakaguzi wa nje kutoka PWC mpo hapo kwa zoezi la ukaguzi naomba mfuatilie ajira zote na mafile sambamba na payroll kama itawezekana kuanzia mwaka 2017 mpaka sasa mtabaini upuuzi mwingi uliyofanywa na idara ya utumishi.

Vilevile, ombeni ripoti ya tume iliyotoka utumishi kushughulikia tatizo la stahiki za wafanyakazi ili iwasaidie katika kazi yenu ya ukaguzi maana ipo hapo ofisi ya utumishi.

Ntunga, nilisema awali kwamba uwezo wako ni mdogo ukabisha sasa je timu ya wataalamu walioletwa kwa juhudi za Mr. Bangu ambaye kwa kweli amebadilika na anapambana sana kutoka utumishi kuja kupitia mafaili ya wafanyakazi kubaini upuuzi wenu wamekuta madudu mangapi mpaka wanawashangaa mlivyo vihiyo.

Acheni ubabaishaji wakati timu hiyo wamewashangaa hata sheria hamzijui someni mzielewe badala ya kuwa wazushi msio na haya. Unahangaika na jeshi usu kuficha udhaifu wako na kuminya haki za wafanyakazi na kusahau majukumu yako ya msingi tutakufunga serikali haijalala. Wapeni wafanyakazi stahiki zao kama ripoti inavyosema acheni kukalia ripoti hiyo vilaza wakubwa nyie.

KUTUMIA JESHI USU KUMINYA HAKI ZA WAFANYAKAZI

Ntunga, napenda kukukumbusha hiyo ni hifadhi na siyo magereza ulikotoka. Nasikia unasema wazi kwamba mpango wa serikali kuanzisha jeshi usu ni vizuri maana wafanyakazi hawataweza kuwa huru kudai haki zao za msingi. Acha kujidanganya na akili yako ya panzi utakopokosea tutaendelea kukuchapa waziwazi sisi hatujaanza leo na tunaendelea kutembea kwenye suruali yako kwa hiyo ili uwe salama fanya kazi kwa kutenda haki badala ya kuishi kwa kudhani dunia ya leo huo mwanya wa kunyanyasa wafanyakazi bado upo.

Wafanyakazi achaneni na hawa wapuuuzi wanaodhani wao ndiyo wenye mamlaka ya mwisho kwenye nchi hii wanasahau viongozi wetu wa juu wa nchi yetu ni wasikivu na wanapatikana muda wowote kusikiliza shida zetu. So muwe na amani hao ni wababaishaji tu wasiojiamini. Mbona Dr Manongi ana nafasi kubwa ila havimbi wala hanyanyasi mtu ila nyie msio na nafasi yeyote ndo mnanyanyua pua kama za ngiri.

Badilikeni maana mkileta jeuri hamtadumu hapo hifadhini. Na mjifunze wenzenu wa TANAPA ambao ni waanzilishi wa hili jeshi usu la hifadhi jinsi wanavyoendesha jeshi usu lao sio kila siku asubuhi gwaride hata kama hakuna hoja ya msingi na mnasahau hifadhi ina ina majukumu mama ya uanzishwaji wake.

Unawaweka watu parade kuanzia saa mbili mpaka saa tatu au nne asubuhi, je hizo kazi zifanyike muda gani? Ntunga mbona siku zinavyokwenda mbele uwezo wako wa ufahamu uanendelea kupungua? Jeshi usu ni zuri sana kama litatumika vizuri ila msidhoofishe majukumu ya msingi ya kila mtumishi kwa kudhani gwaride pekee ndio litakaloongeza tija kwenye hifadhi. Ndiyo maana TANAPA wametenga siku ya Alhamisi ndiyo siku ya gwaride ili kusiwe na kisingizio kwa watumishi kutokutimiza majukumu yao.

Jaribuni kuwaambia wanajeshi mliowaleta kwamba hamuandai watu wa kwenda kwenye vita Somalia ila jeshi usu ni kwa ajili ya kuhakikisha hifadhi na rasilimali zake zinakuwa salama bila kuathiriwa na majangili. Acheni pupa subirini sheria na miongozi ya jeshi usu ipate baraka za Bunge na Mheshimiwa Rais maana ikitokea mfanyakazi yeyote akapata tatizo bila uwepo wa hizo sheria mtapata taabu sana.

MATUMIZI MABOVU YA KASMA YA IDARA YA ULINZI

Kanali Kilugha naendelea kukumbusha kuwa makini sana na matumizi ya fedha za idara yako ya uhifadhi. Pesa ya umma si ya kuchezea leo unaweza kujiona uko salama sababu uongozi uliopo unakupa favor ila baadaye utalia. Malalamiko ni mengi maana ni watumishi wachache walio karibu yako wanaofaidika na fungu hilo. Achana na matumizi yasiyo ya lazima na safari zisizo na tija maana hata hao waliokwenda jela walidhani wako salama kumbe wanajidanganya. Mfano wapo askari waliotoka Mbulumbulu kwenye mafunzo mpaka leo hawajalipwa, wasimamizi wa askari kreta wamekuwa na tabia ya kuandika majina ya vibarua ambao ni hewa na kuchukua pesa kwa matumizi yao ambapo ni kinyume na utaratibu.

Kuwa makini acha kujisahau ukidhani serikali imelala mtafungwa. Ninavyo viambatanisho vya baadhi ya majina ya vibarua na pesa zilizochukuliwa na wafanyakazi waliofaidika. Vilevile, hakikisha jeshi usu halitumiki kama kichaka cha kupiga hela za umma wakidhani ni salama tunafahamu kinachoendelea na acha tabia ya kujaza wanajeshi wengi wasiokuwa na kazi ili tu wapate pesa za dili. Mbona taasisi nyingine kama TANAPA jeshi usu linaendelea vyema na hakuna wanajeshi wengi kiasi hicho kama hapo kwenu? Kumbeni tunahitaji watu wapate mafunzo ya kijeshi kuhusiana na uhifadhi na sio kujiandaa na vita vya Kagera.

Napenda kuwakumbusha wafanyakazi wa hifadhi ya Ngorongoro ili muwe salama acheni kucheza na fedha za umma na viongozi msijione nyie ni malaika hiyo kazi inayowapa jeuri inaweza isha muda wowote ule.

Ntunga na Carlos Mbiro hawafai kuwa Idara ya Utumishi, wamepoteza credibility na ninamkumbusha Ntunga kuendelea kumkumbatia mtoto mpumbavu kama huyu inajionyesha wazi mnashirikiana haya mambo, double standards za kipuuzi hilo shirika si mali ya mama zenu.

Menejimenti nina taarifa zenu wa ugawaji holela wa maeneo ya uwekezaji ndani ya hifadhi bila kuzingatia mwongozo wa GMP na kuwatoza tozo ndogo wawekezaji. Nitaziweka hapa wiki ijayo.

Leo naambatanisha ujumbe wa whatssap wa kipuuzi wa Carlos Mbiro ambalo alilisambaza kwenye magroup ya WhatsaApp kama tangazo halali la ajira na kuleta taharuki kubwa kwa Watanzania.

Wabheja sana.

BITALA
 

Attachments

Back
Top Bottom