Kashaijabutege
JF-Expert Member
- Oct 20, 2010
- 2,696
- 740
1.Mwanaume akiagiza kuku mzima, chipsi sahani tano, mayai kumi, na soda kubwa (2ltrs) mbili, miwa, ndizi mbivu, n.k na akala na kuvimaliza watu wanamsifia kuwa mwanaume anafukia. Akifanya hivyo mwanamama, mtaa mzima utajua na hata mmewe atapigiwa simu kama wadaku wanamjua. Kwa nini iwe hivyo?
2. Mwanaume akitembea na wanawake 6 kwa siku, sio ajabu sana kama akifanya hivyo mwanamke. Kwa nini inakuwa hivyo?
3. Mwanaume akioa wanawake wengi na kuacha haiwi kituko kama mwanamke akiachika mara nyingi. Kwa nini?
4.Mwanamme akila ulabu akajiegesha barabarani, haiwi kituko kama akifanya hivyo mwanamke. Kwa nini?
si kweli
Mwanaume na mwanamke wako sawa kwamaana ya ubinaadamu na haki sawa kwa wote, but in reality they not the same.
1 Ukiwa lets say kwako majambazi yakavamia au hata nyoka tu akaingia ni wazi kidume ndio unapaswa ukapambane.
Kazi zote ngumu ngumu nz dhoruba zote hufanywa na wanaume na sifa mojawapo ya dume imara ni yule alie'' shiba" , ndio maana dume anatakiwa awe mlaji zaidi ya mke.
2 na 3 ni kuwa kwa mujibu wa imani ya dini zetu kubwa mke ni kwaajili ya mume mmoja, lakini mme ni kwaajili ya wanawake wengi, enzi hizo akina sleiman mfalme alikua nao kama 40 na mtume mohd kama 9.
pia mwanamke anaachwa na mwanaume anaacha, so mke akiachika sana anaonekana si bora ndio maana anaachwa.
4 mwanamke badala ya yale majukumu ya nguvu nguvu na dhoruba anategemewa kuwa nyumbani kutunza nyumba kulea watoto nk, lkn dume baada ya mihanjo hujipumzisha kwa ulabu na ndio maana ikitokea kwa mke ni kituko.
ZAT IZ NECHA BANA
Kwa hiyo sio ubaguzi?