Ubaguzi huu utagawa nchi yetu DRC

Ubaguzi huu utagawa nchi yetu DRC

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Kwanini serekali wanatumia nguvu nyingi kubagua sisi watu ambao tumetoka katika mikoa ya waswali.

Yaani kukitokea mtu yeyote ambaye ametoka katika mkoa wa waswali na akawa mpinzani anapewa uraia wa nchi nyingine.

Kila mpinzani ambaye anatoka kwenye mikoa ya waswahili kwa mujibu wao sio mkongo halisi

Katumbi = Zambia (Katanga)

Fayulu =Senegal (Nord Kivu)

Vital= burundi (Sud Kivu)

Muzito = Tanzania (Sud Kivu)

Matata mponyo =Tanzania ( maniema)

George = Kenya (maniema)

Joseph kabila = (katanga)

Tukutane 2024 alafu kusiwe uchaguzi ndo watajua kama tuna tafuta sababu ya kujikata na huu upumbavu wa kubagua watu

Si wanajiona wao wasema lingala ndo wakongo halisi?
 
Ni mbaya sana,ila kikubwa ni kuomba Amani juu ya nchi.DRC ikitulia ikapata kiongozi mkweli mwenye mapendo na ardhi yake,DRC itashika nafasi ya juu kwa uchumi imara.Hii ya kusema huyu Mmanyema,huyu ni Wa Luba,huyu ni Mtwa, au huyu wa katanga,yule wa Mbuji Mayi,huyu Kivu,huyu mkristo yule Muislamu haitasaidia.Watoto wa DRC maeneo ya vita hawasomi,hawachezi michezo kama watoto.Wapo wanakimbia huku na kule ili hali wamezaliwa juu ya ardhi ya Almasi.Mimi nawaoimbea Amani.
 
Interesting thread...

Kuna wanaotuhumiwa kuwa ni watanzania? Very interesting
 
Kuna uzi niliandika kwamba DRC huwa inapata viongozi wa kawaida sana watu wakanijia juu. Congo haijawahi kupata viongozi wa uwezo mkubwa, ni wawe wastani au wa uwezo wa chini.
 
Utajiri wa nchi ya Congo sawa na nchi zote za Arabuni, lakini nchi hii sijui ina laana gani??.
 
Congo si ya kutulia Leo au kesho isubiri miaka 20 mbele kipindi dunia imepata ustaarabu kote ila saivi ata aje malaika haitakaa itulie
 
Ubaguzi unaofanywa na mutu ya congo ni mubaya Sana niwaombe muje Ta-nzania mujifunze vile Bantu ya Ta-nzania bana mapendo jaribu kuangalia bile watanzania banapendana vile vile mutu ya Ta-nzania ina mapendo sana na mutu ya congo hata raisi wa Ta-nzania mutu muzuri.
 
Tukutane 2024 alafu kusiwe uchaguzi ndo watajua kama tuna tafuta sababu ya kujikata na huu upumbavu wa kubagua watu
Dunia hii sasa ni wale wasio na aibu wala chembe ya utu
 
Lakini Ni kweli kagame anasiponsa ba sodaa wa M23? ,Banyamulenge banasumbua batu ba mashariki ba Kongo lakini prezidaa Tshekedi yeye anacheka,watu banapigwa masasi mu kichwa na basodaa wa Rwamdese na M23. Batoto ba Kongo banakuwa bakimbizi ndani mwa inchi yao.
 
Ubaguzi unaofanywa na mutu ya congo ni mubaya Sana niwaombe muje Ta-nzania mujifunze vile Bantu ya Ta-nzania bana mapendo jaribu kuangalia bile watanzania banapendana vile vile mutu ya Ta-nzania ina mapendo sana na mutu ya congo hata raisi wa Ta-nzania mutu muzuri.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]nmesoma Kama namsikiliza nyoshi El saadat
 
Back
Top Bottom