Ubaguzi Katika Kazi Tanzania

Ubaguzi Katika Kazi Tanzania

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Tanzania tunajua sana ubaguzi wa rangi, ukabila na udini. Hata hivyo kuna ubaguzi wa umri, jambo ambalo inaelekea tunalikubali, na hivyo kuwa ndumila kuwili. Kwa Marekani kuna sheria hii, ambayo nitaikuu:

(a)It shall be unlawful for an employer-
(1) to fail or refuse to hire or to discharge any individual or otherwise discriminate against any individual with respect to his compensation, terms, conditions, or privileges of employment, because of such individual's age;
(2) to limit, segregate, or classify his employees in any way which would deprive or tend to deprive any individual of employment opportunities or otherwise adversely affect his status as an employee, because of such individual's age; or
(3) to reduce the wage rate of any employee in order to comply with this chapter.
(b) It shall be unlawful for an employment agency to fail or refuse to refer for employment, or other-wise to discriminate against, any individual because of such individual's age, or to classify or refer for employment any individual on the basis of such individual's age.

Kwa Tanzania ni kawaida sana kuona matangazo yanayoonyesha kutenga umri fulani, hasa mengine yakitoka serikalini, kwa mfano Tangazo hili hapa lililotolewa na uhamiaji.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Kamishna Mkuu wa Uhamiaji anatangaza nafasi za kazi katika Idara ya Uhamiaji. Nafasi hizo ni Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Koplo wa Uhamiaji na Konstebo wa Uhamiaji.

A. MKAGUZI MSAIDIZI WA UHAMIAJI (Nafasi 70)

SIFA ZINAZOHITAJIKA


Awe na Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali katika fani zifuatazo:
Sheria, Uchumi, Biashara, Utawala, Uandishi wa Habari, Ualimu, Usafirishaji, Raslimali Watu, Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Takwimu, Uchapaji, Uhandisi Majengo na Uhandisi Mitambo.

Awe na umri usiozidi miaka 35


Tanzania inabidi tubadilike. Umri ni namba tu; kuna watu wanaishi hadi kufikia umri wa miaka 100 na kuna wanaoishi miaka mwili tu. Iwapo tutakataa kuajiri watu wenye miaka 35 na zaidi, lakini watu hao wakaishi hadi miaka 100 je kweli tutakuwa tumewatendea haki? Tujue kuwa umri pia unaambatana na kitu kinachoitwa uzoefu, ambao ni elimu kubwa sana zaidi ya ile ya darasani. Umri ungetumika katika kazi zinazohusisha nguvu tu kama polisi na jeshi, lakini siyo kazi zinazohitaji busara kama ukaguzi.
 
Back
Top Bottom