Ubaguzi wa rangi Urusi: Hadithi kuhusu dhana potofu za ubaguzi wa rangi

Ubaguzi wa rangi Urusi: Hadithi kuhusu dhana potofu za ubaguzi wa rangi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Ubaguzi wa rangi Urusi: Hadithi kuhusu dhana potofu za ubaguzi wa rangi​

Student Roy Ibonga
Roy Ibonga's personal archive
Kuna takriban maelfu ya watu weusi wanaoishi nchini Urusi- wakiwemo waliozaliwa nchini Urusi na baadhi wakiwa na mchanganyiko wa vizazi (machotara) ,Waafrika na wengine kutoka mataifa ya Caribbean wanaofanya kazi au kusoma nchini Urusi.

Hizi ni baadhi ya hadithi zao kuhusu ubaguzi wa rangi nchini Urusi.

Roy Ibonga, Mwanafunzi wa uchumi, 21

Video ya hivi karibuni ya dereva wa teksi akikataa kumchukua mwanaume mweusi katika gari lake ilisambazwa sana katika intaneti nchini Urusi.

Mtu aliyeachwa akiwa amesimama alikuwa nikijana huyu Roy Ibonga mwenye umri wa miaka , kijana wa Kikongo anayesomea masomu ya uchumi katika Chuo Kikuu cha jimbo la Bryansk - Bryansk State University.
Katika video yake, iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, dereva anasikika akisema " Kama simpendi mtu , Siwezi kumuendesha. Ni gari langu". Wakati Roy alipomuuliza ''kwani wewe ni mbaguzi''?" dereva alijibu , "Ndio, bila shaka."

Baadae kampuni ya teksi hiyo Yandex taxi , ambayo ni sawa na Uber ya Urusi, iliomba msamaha kwa Roy.
"TAsante kwa kupata jinsi ya kuhusu tabia hii isiyoweza kuvumilika. Naomba msamaha kwamba ilitokea kwako ," aliandika muwakilishi wa huduma za wateja.

Kwa mujibu wa taarifa za habari, dereva alifutwa kazi siku hiyo hiyo. Kampuni ilisema " madereva wakatili na wabaguzi wa rangi hawana nafasi katika Yandex Taxi".

Roy aliandika kuhusu tukio hilo kwenye mtandao wa Instagram. Baadhi ya watu walielezea kumuunga mkono, lakini wengine waliandika matusi ya kibaguzi. Baadae Roy alifunga akaunti yake . Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii waliikosoa kampuni ya Yandex kwa kumfuta kazi dereva wa teksi na hata wakatoa wito wa kuisusia kampuni hiyo.

'Wakati mmoja hawakuniruhusu kuingia katika mgahawa '
Roy anaishi Bryansk, jiji lililopo kilomita 380 (au maili 236 ) kusini mwa mji mkuu Moscow, ambako sio mwafrika pekee anasomea, lakini wote , anasema wanakabiliwa na ubaguzi wa rangi.

" Tukio hilo la dereva wa teksi-hutokea sana .Niliamua tu kuchukua video wakati ule ili kuwaonyesha watu. Huwa inatokea hivyo kila wakati. Hutokea kwa marafiki zangu pia, lakini hawawezi kulizungumzia kwasababu hawazungumzi Kirusi.

Roy Ibonga

Roy Ibonga​
Presentational white space

"Wakati mmoja mmoja mwaka jana hawakutaka niingie kaytika mgahawa. Mlinzi aliniambia , 'Huwezi kuingia kwasababu mara ya mwisho Waafrika walipoingia kulikua na mapigano '. Hiyo inanihusu nini mimi? Niliuliza. Lakini hakuniruhusu niingie. Nilimuita hata meneja, lakini waliniambia sitaruhusiwa kuingia.

"Labda ni kwasababu hatuko wengi na hatujawa hapa kwa muda mrefu, kwahiyo watu hawajatuzowea. Kuna tofauti kubwa baina ya Bryansk na Moscow. Moscow ni kama nchi tofauti. Sikuwahi kuhisi kubaguliwa pale ."
Alisema "hakuwahi kumuona kamwe polisi akimpiga mtu nchini Urusi" na "Sikuwahi kusikia lolote kumhusu polisi pale".

Isabel Kastilio, meneja masoko, 27

Isabel Kastilio
Isabel Kastilio
Maelezo ya picha,Isabel aliota akitembea mtaani bila watu kumkodolea macho
Presentational white space

"Ninaishi Moscow, lakini nilikwenda katika chuo kikuu St Petersburg na nilizaliwa katika Yuzhno-Sakhalinsk [mashariki zaidi mwa Urusi]."

Isabel anasema alionewa na watoto wengine alipokua shulenina kukumbushwa kila siku kwamba rangi yake ya mwili ni tofauti.

" Ilikua ni vigumu sana kuyakubali yote hayo kila siku , hata kama nilisomea moja ya shule nzuri sana mjini, hasa kwa masomo ya hisabati na fizikia. Sikuweza kujisimamia mwenyewe. Sikuwaambia wazazi wangu niliyoyapitia. Kaka yangu mkubwa alinilinda shuleni. Wakati mwingine ilibidi apigane kwa ajili yangu ."

Isabel aliota kuhusu kuhamia Yuzhno-Sakhalinsk mahali ambapo ataweza kutembea mtaani bila kukodolewa macho na watu wanaomshangaa. Kwa pamoja yeye na baba yake kutoka Dominican walikua wakiuangaliwa na watu kwa mshangao

"Nilipohamia St Petersburg kila kitu kilikua bora zaidi, nilianzaq kusahau kwamba ninamuonekano tofauti. Lakini baadae nilipoanza kazi na kuhitaji kukodisha nyumba ya kuishi, nilihisi ubaguzi wa rangi tena ."

Hali ilikua mbaya zaidi hususan Moscow, anasema Isabel. Matangazo yote ya kukodisha nyumba yalisema "Slavs only", ikimaanisha watu wanaotoka Ulaya ya kati na mashariki tu.

"Wakati wenye nyumba waliposikia majina yangu kwenye simu, ingawa nilikuwa na kibali cha kuishi Moscow, hawakuamini ningeweza kulipia nyumba. Ilinibidi nipange nikutane nao ana kwa ana, ili waone kuwa nilikua mtu wa kawaida mwenye kazi ya kawaida na nisingeweza kugeuza nyumba zao kuwa kitovu cha madawa ya kulevya.

" Kila ninapokutana na watu hawa , wanapotulia huanza mzaha. Huwa ninawapuuza au ninaendelea kufanya mzaha nao, iwapo utakua na hasira kila wakati inaweza kukuathiri ."

'Adui wa watu '
Mama yake Isabel anatoka katika kisiwa cha Sakhalin na baba yake ni kutoka Dominican Republic. Walikutana miaka ya 1980, walipokua wakisoma katika Kyiv, mji mkuu wa Ukraione iliyokuwa Usovieti.

Baba yake Isabel alikuja kupitia Muungano wa Usoviet katika mpango wa elimu wa kubadilishana wanafunzi. Isabel anasema kwamba wakati wazazi wake walipooana, walipokua wanasoma , Chuo kikuu hakikufurahi. Mama yake alinyanyaswa na akaitwa'adui wa watu''

"Katika chuo kikuu walianza kumpa maksi ndogo, ingawa wakati wote alikua wa kwanza darasani. Siku moja baada ya kujifungua kaka yangu alikua na mhihani. Chuo kikii kilikataa kumruhusu aahirishe mtihani.

Hakuruhusiwa kutetea mradi wake wa kumaliza ipasavyo masomo.Kila wakati alipata alama za juu zaidi, lakini hawakumpa zaidi ya shahada ya daraja la tatu.

Maxim Nikolsky, mwandishi wa habari, 24
Maxim Nikolsky

Maxim Nikolsky
Maxim alipata uzoefu wa kubaguliwa alipokua mtoto
Presentational white space

"Nimepata uzoefu wa ubaguzi wa rangi wa kawaida mjini Moscow. Wakati mwingine watu walikua wananiangalia kwa kunishuku au wakati mwingine wanahamia kiti kingine kunikwepa tulipokua katika treni. Lakini sijashuhudia chuki mbaya ya ubaguzi. Sio wakati huu nikiwa mtu mzima.

"Nilikabiliwa na ubaguzi wa rangi nilipokua shule ya msingi na sekondari. Ninadhani ubaguzi umeniachia kofu. Ninaishi viungani mwa mji wa Msocow. Haikua ni watoto tu, bali wazazi wao ambao waliwalea kuwa wabaguzi wa rangi.

" Wakati mama yangu alipokuja kwa wazazi na kulalamika kuwa watoto wengine walikua wanakwaza, walimwambia, 'ni kosa lako kwa kumzaa'. Baadae nilikwenda katika shule nzuri. Watoto na hasa wazazi wao walikua na uelewa na mawazo yaliyopanuka zaidi''.

"Iliniudhi sana wakati nilipokua mtoto na mara kwa mara sikutaka kwenda shuleni.Sasa hainisumbui sana , lakini kuna nyakati ninakasirika .

"Wakati mmoja, katika kitivo cha Utangazaji habari cha chuo kikuu, nilimshikia mlango mwanafunzi mwenzangu wa kike aweze kupita na mtu mwingine nyuma yake akasema , 'Oh! Kitivo cha Wanahabari siku hizi kinamlindalango mweusi!' Viti kama hivyo vinanikasirisha sana lakini kwa ujumla vimepungua kuliko ilivyokua awali . Nimejifunza kuwa na mtizamo hasi kwangu na ninadhani muonekano wangu ni faida.

"Ni ubaguzi wa ramngi mdogo, huo ndio tatizo nchini Urusi na unatokana na ujinga. Sidhabi tuna ubaguzi wa rangi wenye misingi ya kikatiba wa Magharibi ."

Kamilla Ogun, mchezaji wa mpira wa kikapu, 21

Kamilla Ogun
Kamilla Ogun
Maelezo ya picha,Wakati Kamilla alipohamia Moscow akiwa na umri wa miaka 12 alikabiliwa na ubaguzi mdogo wa rangi

" Nimekua nikuatilia maandamano nchini Marekani kuanzia yalipoanza. Nimeshitushwa na ukatili dhidi ya watu weusi huko. Ubaguzi wa rangi ni tatizo nchini Urusi pia, lakini hapa kila kitu kwa kiwango ambacho sio kikubwa ."
Kamilla ana asili ya Urusi na Nigerian. Alikulia Stary Oskol,mji uliopo kilomita 600 kusini mwa Moscow. Hapakuwa na watu wengine wengi weusi.

"Ungeweza kuhesabu idadi ya watu weusi pale kwa vidole vya mkono wako mmoja. Nilikua na bahati kwasababu darasa langu lilikua na uvumilivu na tulifahamiana kuanzia shule ya chekechea. Lakini watoto katika madarasa mengine walinipachika majina. Huo ulikua ni ubaguzi wa wa rangi kusema ukweli na walinitusi ."

"Nilikuja kutoka Moscow kucheza kwa ajili ya timu nilipokua na umri wa miaka 12 na ubaguzi haukua mbaya sana pale. Bado ninaulizwa maswali ya dharau kama, 'Kwa hiyo unatoka Afrika?, au nini?' Baadhi ya watu hawatambui kuwa baadhi ya kauli hizi zinatuudhi. Mara nyingi hua ninawapa jibu lolote au ninaamua kuwapuuza.

"Klabu za mpira wa kikapu tayari zimezowea kuwa na wasichana weusi katika timu zai, kwa hiyo kuna ubaguzi mdogo.Lakini unapochezea timu ya Urusi pale kila mara kunakua na jumbe kwenye kurasa za mitandao ya kijamii : Ni kweli ni Mrusi?, Kumekua na mkanganyiko? Watu hufikiri ni kichekesho wakati msichana mweusi anapochezea timu ya Urusi ."

"Inaniudhi sana nilipokua mtoto,Iliniumiza sana. Lakini sasa ninapuuza. Kwanini waniite majina? Jibu ni rahisi: sio mini hilo ni kosa, ni watu wanaonizingira mimi ."

Alena El-Hussein, linguist, 25​

Alena El-Hussein
Alena El-Hussein's
Alena El-Hussein anasema alijihisi tofauti katika maisha yake .

Alena El-Hussein ana asili ya Urusi na Sudan, na alizaliwa Moscow. Katika maisha yake yote alihisi kuonekana mtu tofauti.

"Si jambo linalokera kila wakati. Inategemea hali . Mara chache sana nimeitwa chernaya - "mtu mweusi" -lakini mara kwa mara wanaoniita hivyo ni watu wajinga sana. Kumekua na malumbano, lakini za mara nyingi ni kuhusu watu na tabia zao kuliko ya rangi ya mwili. Kuna wakati ambapo watu wameniita 'chocolate' na mambo mengine kama hayo ."

Alena anamini tatizo la ubaguzi wa rangi nchini Urusi ni tofauti na Marekani.

" Wanaume wa Urusi na wanawake hujitambua kama wakoloni wa wazungu wa Ulaya. Ujinga wa kihistoria huwapotosha na kuwafanya wajione wa maana zaidi.

"Ubaguzi wa rangi hapa si mbaya sana dhidi ya watu weusi kama ulivyo dhidi ya watu kutoka jamuhuri za zamani za Usovieti

" Watu kutoka Asia ya kati ni walengwa wa ubaguzi mbaya wa rangi. Ni jambo la kushangaza kwamba hakuna maandamano yake. Labda jamii ya Warusi haijaliamkia suala hili bado ."

Chanzo: BBC
 
Western propaganda on its duty.
Sibishi kwamba Russia hakuna ubaguzi laah. Nakubali kwamba hali hiyo ipo na pengine ni kubwa kuliko sehemu nyingine za Dunia but Kwa wamagharibi jambo hili ni kubwa sana Kwa malengo maalumu ya kuichafua zaidi na zaidi Russia. Si kijamii tu katika maswala haya ya ubaguzi Bali kiuchumi, kiteknolojia, kijeshi, kisiasa nk.
Lengo ni kuhakikisha Russia is falling apart. Pengine itemgwe world wide. Wapi bwana. Hii haitatokea. bila shaka Russia is too strong now than yesterday.
 
Back
Top Bottom