Duh sasa mm nilikuwa natoa 70,000/= kwa wiki huduma ya nywele bado naambiwa bahili unaichukuliaje hili? Maana nilikuwa najinyima kunywa Safari nikawa nakunywa Bingwa ili kumfurahisha yeye lakini nimeambulia patupu.
naomba nikae upande wa kiume leo though I am a woman. Mwanaume anapenda sana mkewe apendeze katika kila hali. kwa mfano: huyu mdada anayelalama hapa ana kazi nzuri kama ya mumewe kwa nini msikae chini kufanya mahesabu mjue mtachangia nini kwenye matumizi yenu ya kila siku?
Wanaume wanafikia kufanya hivyo kwa sababu wakishajua vipato vyao utashangaa anaenda kwa jirani kuchuku kadi za michang kila siku ili achangie harusi,kitchen party huku mwenzie amebudget. Maisha ya ndoa ni kuzungumza, kusaidiana katika shida na raha siyo kusaidiwa. kama kuna biashara na kazi za pembeni basi kinachopatikana kigawanywe siyo kutaka tu mwanaume akufanyie kila kitu ndiyo ujue anakupenda. Wanawake ACHENI KULALAMIKA HATA VISIVYO VYA MSINGI.
FANYA NA WEWE AFUATE MFANO WAKO. Wanawak hao hao ndiyo wanakuwa wa kwanza kuwa nyanyasa kama waume zao hawana vipato.
Endeleeni kutegemea waume zenu bila kujishughulisha akifilisika familia inateteleka na wengi wenu ndo hapa napo wachukia wanawake ukisha fulia tu basi mwanaume unakimbiwa na mke na ndo kama ni mzuri basi inakuwa balaa anahamia kwa wenye fweza wewe unabaki kukomaa sura tu.
eeeeh jamani huyo mwanaume ana matatizo ya kisaikolojia hivi haoni hata bible imeandikwa enyi wanaume watunzeni wake zenu na enyi wanawake wapendeni waume zenu..hayo maneno yana utofauti kabisa ingawa sometimez tunasaidiana kukidhi maisha
Huyu dada hatakiwi kukaa kimya kwani tatizo litakuwa sugu na atakapoamua kusema itakuwa too late ..itabidi amuite mme wake na aongelee hayo yanayomkwaza ili wapate muafaka amwambie mmewe vile anavyojisikia na anaona kama hatendewi haki
Kuna watu wengine wanafumbuliwa macho kwa kuambia..Je anamuogopa mme wake ???????
Si ni bora mkaweka utaratibu wa kutoa pasu kwa pasu? wengine wamezoea kunyonya tu utakuta mkitu unamlisha, wewe unajituma kumnunulia zawadi kama ngou, pants n.k lakini bado linakuuliza mshahara wako unatumia vipi wakati linajua haliachi hata senti tano nyekundu ya zamani kwa ajili ya matumizi
Huyo jamaa ametuaibisha wanaume wote hapa. In fact hakuna mpwa mwenye tabia hizo, tukizigundua tutahoji uanaume wake....
Umesema neno mpwa!
kasheshe!Waungwana hii issue ni kweli kabisaa mimi naifahamu, maana kuna wakati ilimtokea mtu wa karibu yangu, lakini yeye alijaribu kumnyima nani hii kila mzee alipohitaji, akadai kuwa anaonewa, mzee ilibidi aanze kubadilika taratibu, na hadi sasa hakuna kitu kinachoitwa ubahili kwa wanandoa hao. Mimi namshauri huyo bibi ajaribu hiyo anaweza kuwini, lakini atumie mbinu hasa maana mzee anaweza kumpoteza jumla, na wajanja wakamdaka nje!
una hasira, i understand!Si ni bora mkaweka utaratibu wa kutoa pasu kwa pasu? wengine wamezoea kunyonya tu utakuta mkitu unamlisha, wewe unajituma kumnunulia zawadi kama ngou, pants n.k lakini bado linakuuliza mshahara wako unatumia vipi wakati linajua haliachi hata senti tano nyekundu ya zamani kwa ajili ya matumizi