Ubalozi wa Marekani Kenya watoa tahadhari ya kuwepo kwa shambulio la Kigaidi Jijini Nairobi wakati wowote kuanzia sasa

Ubalozi wa Marekani Kenya watoa tahadhari ya kuwepo kwa shambulio la Kigaidi Jijini Nairobi wakati wowote kuanzia sasa

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetoa onyo kwamba magaidi huenda wakashambulioa hoteli moja kubwa nchini Nairobi.

Kulingana na ubalozi huo, hoteli iliolengwa ni maarufu kwa kuwa hutemebelewa sana watalii na wanabiashara.

''Makundi ya kigaidi huenda yanapanga njama dhidi ya hoteli moja kubwa mjini Nairobi. Hoteli inayolengwa haijatambulishwa lakini inaaminika kuwa hoteli ilio maarufu sana na watalii na wafanyabiashara wa kigeni'', lilisema onyo hilo.

Wakenya wameshauriwa kuwa waangalifu wakati wanapotembelea ama kuishi katika hoteli mjini Nairobi.

''Unapokuwa unaishi katika hoteli jifahamisheni kuhusu njia za kutorokea . Panga mapema jinsi utakavyoweza kutoroka katika hoteli iwapo kutakuwa na dharura yoyote'', liliongezea onyo hilo.

Wakati huohuo Inspekta jenerali wa polisi nchini Kenya Hilary Mutyambai amewaomba Wakenya kuwa watulivu , akisema idara ya polisi imeimarisha usalama nchini kote mbali na kulinda mipaka yote.

Hatahivyo amewataka Wakenya kuwa makini na kushirikiana na polisi pamoja na vitengo vingine vya usalama dhidi vitendo vyovyote vinavyozua shauku.

''Kufuatia kuimarishwa kwa usalama kote nchini Wakenya wametakiwa kuendelea na shughuli zao za kila siku bila ya hofu''.

''Vilevile amewataka kuripoti chochote wanachokishuku kupitia nambari ya 999,911 na 112'', alisema mkuu huyo wa polisi katika taarifa yake.
******

Wakenya chonde chonde msipuuzie hizi taarifa, hamkawii kusema tunachekelea mnapotandikwa na Alshabaab
 
Kanunue mbuzi basi, awe tayari ndio maafa yakianza na damu ikimwagika usherehekee ukijivinjari na wali kwa nyama choma na kachumbari. Ndio kawaida yenu nyinyi wachawi na roho zenu nyeusi.
 
Leo ndio umenena kitu cha maana, badala ya kusifu shabab kama mazoea yako. Polisi wa Kenya wasikilize Marekani maana Marekani huenda wana informers ndani ya kundi hilo.
 
Kutoa tahadhari ni jambo moja, lkn mbona hawaelekezi hatua za kuchukua katika maeneo husikaa?

binafsi nitawasifu wamarekani pale watakapotoa tahadhari kabla ya kutokea mass shooting(s) nchini kwao.
 
Kutoa tahadhari ni jambo moja, lkn mbona hawaelekezi hatua za kuchukua katika maeneo husikaa?

binafsi nitawasifu wamarekani pale watakapotoa tahadhari kabla ya kutokea mass shooting(s) nchini kwao.
Huwa wanatoa tahadhari za kipuzi sana. Ile Garissa university walisema attack itatokea katika university moja Kenya. Hawakutaja ni university ipi. Sasa hivi wanasema ni hoteli moja bila kufafanua ni hoteli ipi haswa.

Zamani nilikuwa napuuza hizi tahadhari zao lakini kila wanapotoa tahadhari, mashumbulizi lazima yatokee baada ya wiki moja hivi. Kwa hivyo Kenya tuwe makini, Marekani hadanganyi.
 
Chatter is a signals intelligence term, referring to the volume (quantity) of intercepted communications. Intelligence officials, not having better metrics, monitor the volume of communication, to or from suspected parties such as terrorists or spies, to determine whether there is cause for alarm.
 
Ubalozi wa marekani umetoa tahadhari kwa raia wake waishio Kenya juu ya uwezekano wa kutokea shambulizi la kigaidi katika hoteli kubwa mjini humo katika siku za karibuni, Hotel hiyo ambayo haijatajwa inasemekana kuwa inaidadi kubwa ya watalii wafanyabiashara na wasafiri. Watu wote waliokaribu na maeneo ya Nairobi wameaswa kuwa makini na dalili za mashambulizi na kufuata maelekezo yote yanayotolewa na vyombo vya ulinzi na usalama.

====
For English Audience

The US Embassy issued an advisory to its citizens on Thursday, February 27, warning that terrorists may be planning to carry out an attack against a major hotel in Nairobi over the near term. The unidentified hotel is believed to be popular with business travelers and tourists.

Source: Gardaworld Security.
 
Taasisi za intelijensia za waafrika bado sana. Bado mno.

Kuna mlevi mmoja aliibuka akasema eti "TISS ni the best intelligence agency in the world". Nikasema hiiiiiii!

Hivi vitaasisi vyetu uchwara vya intelligence si ajabu viko under intelligence monitoring ya intelligence agencies za wenye dunia yao!

Vitaasisi vya akina musiba na sarakasi za kichadema hakuna kitu pale. Ujinga mtupu!

Lakini tunajitahidi. Nasikia tuna undercover agents huko kwenye stendi za mabasi!
 
Tahadhari bila kutoa msaada wa kukabiliana na janga wakati anamjua adui huo ni ujanja wa kupora mali za jirani zetu. Hapo beberu anachokoza ili Mkenya akubali mkataba wa kibiashara. Muda si mrefu utasikia deal la biashara mpya limesainiwa white house.
 
Kanunue mbuzi basi, awe tayari ndio maafa yakianza na damu ikimwagika usherehekee ukijivinjari na wali kwa nyama choma na kachumbari. Ndio kawaida yenu nyinyi wachawi na roho zenu nyeusi.
Kwanini unaweweseka? Ni onyo tu kwa jeshi dhaifu na wazembe..Walinde wananchi wa kenya sio kukesha bar wakila malaya
 
Kwanini unaweweseka? Ni onyo tu kwa jeshi dhaifu na wazembe..Walinde wananchi wa kenya sio kukesha bar wakila malaya
Hahahaha, nimecheka sana jinsi ulivyompa za uso, hiyo ni dalili ya mtu asiyejiamini na aliyekata tamaa, hata pale anapopewa mawazo mazuri yeye hudhani anadhihakiwa. Mungu shuka usaidie wakenya wanateseka sana
 
Kwanini unaweweseka? Ni onyo tu kwa jeshi dhaifu na wazembe..Walinde wananchi wa kenya sio kukesha bar wakila malaya
Eti jeshi? Tishio la shumbulizi la kigaidi na intelligence kuhusu hilo sio jurisdiction ya vikosi vya kijeshi, acha ushamba. Usijali lakini wape wenzako tahadhari ya kutumia KShs kwasababu sarafu hiyo itaporomoka na thamani ya Tzshs itapanda. Kama ulivofanya, sijui ilikuwa ni mwaka jana?
 
Mleta uzi kaleta taarifa vizuri tu wala hakuna alipochekelea,
Kwa hiyo na sisi tuwaambie mlikuwa mnachekelea mwaka jana Tz ilipopewa security alert halafu mkafungua nyuzi humu,
Hivi huwa mnadhani kila Muda ni mshindano humu,
Tapala emodai grow up.
 
Eti jeshi? Tishio la shumbulizi la kigaidi na intelligence kuhusu hilo sio jurisdiction ya vikosi vya kijeshi, acha ushamba. Usijali lakini wape wenzako tahadhari ya kutumia KShs kwasababu sarafu hiyo itaporomoka na thamani ya Tzshs itapanda. Kama ulivofanya, sijui ilikuwa ni mwaka jana?
Alshabaab ni adui toka nje ya Kenya, kama ilivyo kwa Boko Hatshi, ISIS na Alqaeda, wahusika wakuu katika makundi yote haya ni majeshi sio polisi, Acha kutetea jeshi lenu dhahifu sana, KDF ilikwenda Somalia ili kusambaratisha Alshabaab wasiweze kuishambulia Kenya, kilichotokea ni kinyume na malengo, sasa hivi Alshabaab inashambulia Kenya mara nyingi kwa mwaka kuliko kabla ya KDF kuingia Somalia.
 
Back
Top Bottom