Ubalozi wa Marekani kuwaondoa raia wake Tanzania kwasababu ya Corona na kuwarudisha kwao

Kwani kwetu huwezi kupata maji ya moto ukaweka kipande cha limau ukanywa au ukala machungwa kwa wingi,sema wenzetu ni wavivu wa kula matunda!!!!
tehe tehe tehe tehe tehe tehe tehe ,yani kwetu bhana kuna wataalamu wa magonjwa mengi sana,kiujumla wataalamu wa kila kitu,hadi muuza machungwa katumia fursa.
Natumai muuza mabati wa JF ya Facebook na yeye atangaze kuwa mabati yake yanazuia Corona.
 
Waharakishe wawaondoe Marekani wote wanaokuwa nchini, pamoja na maofisa wote kabisa wa ubalozini, ambao wengi ni majasusi. Na Tanzania isiruhusu Mmarekani yo yote kuingia nchini mpaka hapo kitakapoeleweka. Wangojwa wa corona nchini kwao ni mara kadhaa ya idadi ya wagonjwa walioko Tanzania. Sasa Tanzania imekuwa nongwa.
 
akili zingine za kijinga sana. Marekani haisemi kwamba kwao hakuna Corona. Wanachosema watu wao warudi kwao ambako itakuwa rahisi kuwahudumia.

wanaogopa mipaka ikifungwa na hali ikawa mbaya kwao wakiwa Tanzania itakuwa mgumu kuwasaidia.

wakati wa majanga unataka familia yako irudi nyumbani kwako ambako unaweza kuwasaidia.

Hivyo ndivyo nchi zinazojali watu wake hufanya.
 

Wanangu Elimu. Elimu. Elimu. English ngumu au.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swadakta !
 
Ila swali la kujiuliza ni kwamba,kwao kuna maambukizi zaidi,lakini kwanini bado wanataka watu warudi makwao ?
 
Labda wameona hatuko serious na ugonjwa wa corona, wakati mwingine tunaingiza siasa.

Yani. English tatizo au. By the way Siasa kwao ndo nyumbani Labda kama husikilizi News. Usipende sana kuleta Shida zako za kisiasa kila mahali. Hiyo barua Ni ya kawaida sana kwa kuwa wanatimiza wajibu wao Kwa wananchi wao.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…