Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania waagiza takwimu za wagonjwa wa korona na chanjo vitolewe

US na UK walivyo hamia Irak walishirikiana na Dunia na kuna mambo mengi tu , hata vita vya kibiashara na Russia , China na Nchi za Kiafrika , je wana act in a modern way au primitively
Kuna mambo ambayo ni lazima yashughulikiwe collectively. Mgogoro wa biashara kati ya China na US, na kati ya Ulaya na Russia, ni masuala binafsi ya mahusiano ya mataifa husika. Na athari zake, kimsinhi zitayagusa mataifa hayo kwa kiasi kikubwa. Na kuna sababu ambazo US walieleza wakiituhumu China kukiuka, na siyo mara ya kwanza.

Suala la Iraq, lilifuatia azimio la Umoja wa mataifa, japo halikuleta matokeo yaliyotarajiwa. Lakini ni kweli kuwa Sadam Hussein, kama alivyo Gadafi, hakuwa kiongozi mzuri, aliwaua wapinzani wake, alilipendelea kabila lake, aliwahi kuwaua watu wa kabila lisilo lake kwa kuwapulizia hewa ya sumu - aliua hata watoto ambao hawaelewi hata mambo ya siasa.
 

Wasiwasi ndo akili
 
Tatizo mojawapo ni kufikiria kuwa huu ni ugonjwa wa kipindi kifupi.

Virusi vya mafua ambavyo ni jamii ya corona vimeendelea na maambukizi kwa watu miaka nenda rudi na hivi vipya vya uviko 19 itakuwa hivyo hivyo kama mkakati wa kinga wa kitaalamu usipotekelezwa.

Tofauti ni idadi kubwa ya maambukizi na vifo kwa upande wa uviko ukilinganisha na haya mafua ya kawaida.

Tusipokubali suluhisho la kitaalamu yaani chanjo, huu ugonjwa utaendelea kutesa hii nchi muda mrefu ujao.

Miaka kumi ijayo, wengi ambao wana kinga ya ujana leo watakuwa hatarini na baada ya hapo yatafuata marika ya chini.

Na bado kuna yumkini kuwa inaweza ibuka mutant variety itakayo ambukiza na kuleta kifo kwa mtu wa umri wowote.

Kwa ujumla mimi binafsi naona baadhi ya watanzania watu wazima tunachukulia huu ugonjwa kwa mtazamo wa umimi uliojaa ujinga mwingi ukichochewa na siasa za kijinga pia,bila kufikiria kuwa hatima ya nchi hapo mbeleni itabebwa na kizazi kichanga ambacho hakina maamuzi yoyote juu ya yanayotokea leo.

Nawasihi viongozi wetu wasiweke maisha ya watoto wetu rehani kwasababu tu wao wanaishi nyakati ambazo wengi wameaminishwa kuwa siasa ndiyo maisha.

Tatizo la kisayansi linahitaji suluhisho la kisayansi.

Uviko 19 ni ugonjwa unaosababishwa na virusi na suluhisho lake ni kinga ya kutumia chanjo na sio kukemea kama hizo ziitwazo pepo au kunywa dawa zisizothibitishwa.

Acheni sayansi ichuke nafasi yake kwa ajili ya hatima ya taifa letu na vizazi vijavyo.
 
Viongozi wa Tanzania, wanatakiwa kushirikiana na Dunia. Hata kama unasema una njia zako zinazotibu Covid 19, unatakiwa uishawishi Dunia, na Dunia ithibitishe.

We are acting primitively by not cooperating with globe community.
Says the Globalists [emoji3][emoji3]
 
Rwanda na Malawi na uganda na Kenya kuna chanjo wahi mkuu...

TZ tutachanjwa mwisho baada ya kumaliza tests zao
Ingekuwa enzi ya JK Sasa hivi wote tungekuwa tumechanjwa chanjo ya COvid-19.

Na alivykuwa sharp tungekuwa Taifa la kwanza Afrika kuchanja. Bahati mbaya tuna "Mchunga ng'ombe'. Kuficha malazi na takwimu sahihi anaita uzalendo Wakati watu wanaangamia.
 
Hoja pumba kuliko...

Hawajawahi kutu colonize

Wanasingiziwa kuua watu Congo wakati wa King Leopold

Wazungu hawana nia hiyo kabisa
 
Inaelekea penda tusipende tutachanjwa tuu na takwimu za maambukizo tutazitoa hakuna jinsi. Wazungu wanaanza kuogopa virusi vya covid vinaweza ku mutate hapa tukapata variant ambayo ni kali zaidi na inakataa matibabu halafu ikasambaa dunia nzima. Pili, chanjo ni biashara ambayo makampuni ya dawa wanatafuta wateja kwa hiyo wata lobby serikali zao wasisitizie kila mtu achanjwe.
 
Viongozi wa Tanzania, wanatakiwa kushirikiana na Dunia. Hata kama unasema una njia zako zinazotibu Covid 19, unatakiwa uishawishi Dunia, na Dunia ithibitishe.

We are acting primitively by not cooperating with globe community.
Wanaingilia mamlaka yetu wao kama nani
 
We are sovereign state, who are they to decide our fate? Wakafie mbele
 
Mnaficha nini ? au ni kweli kwamba mnaongoza kwa vifo africa ?

ili wajue biological weapon yao imefikia wap? its a shame the uS inataka kutoa advice while bado wapo kwenye battle na china kujua ukweli ni nani alitengeneza huo ugonjwa
 
Aksante Balozi; with a piece of note that: None heeds to your superb advice.
 
Nmekuja na sampo spesi moja hapa naona itawafaa
 
ili wajue biological weapon yao imefikia wap? its a shame the uS inataka kutoa advice while bado wapo kwenye battle na china kujua ukweli ni nani alitengeneza huo ugonjwa
Umeni quote tu ili upate elfu 7 za chama , lakini kiukweli huna hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…