Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania waagiza takwimu za wagonjwa wa korona na chanjo vitolewe

Sijawekwa kwenye bajeti ya Kenya. Mimi ni raia wa Tanzania.
Kama ni raia wa Tanzania basi heshimu taratibu, miongozo, na maelekezo yatolewayo na serikali ya Tanzania. Tanzania kwa sasa hatuhitaji chanjo!! Kwa sababu hakuna uhakika kama hii chanjo ni salama na inakinga mtu kwa muda mrefu kiasi gani. Ikizingatiwa kuwa virusi vipya vya Corona vinapatikana Mara kuwa Mara kutokana na corona kujibadilisha (it mutates)!
 
Sawa Nyanda na mteuliwa wa mkuu.
 
Acha uboya nikichanjwa mimi nikafa wewe utapata hasara gani?
 
Nenda ulaya na familia yako ukachanjwe, au beba ukoo mzima . SISI Kwetu Chnanjo NO....................
Nani ana kulazimisha si muache iwe hiari kama ilivyo kwenye malimao yenu na tangawizi lakini watu wakiungua wana kimbilia mitungi ya gesi badala ya kujifukiza.
 
semeni hamna hela kwisha,kwani ni mara ya kwanza kupokea chanjo hapa nchini? mliwahi kufanya utafiti wa kuthibitisha hizo chanjo zote hapo kabla? wapi na lini? ndio kusema mwaka huu ndio mmekuwa makiini kuliko wakati wowote toka tupate uhuru? tupeni chonjo hili sio ombi ni haki yetu.
 
Upotoshaji mkubwa. Eti "Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania waagiza takwimu za wagonjwa wa korona na chanjo vitolewe". Niliposoma kichwa hicho cha habari nilijaa hasira na kuanza kujiuliza huyo Balozi anajiona yeye ni nani kiasi cha kuweza KUIAGIZA Tanzania ifanye kitu fulani. Baada ya kuisoma taarifa yenyewe ya Balozi nikagundua kwamba Balozi wala 'hakuagiza' cho chote na sina tatizo kabisa na aliyoyasema. Mtoa mada, kwa kujaa jazba ya kuikosoa Serikali, anatafuta kwa udi na uvumba tamko lo lote linalounga mkono fikra zake ili kuzipa uzito hoja anazozitoa.

Aliyoyasema Balozi ni yafuatayo:

Paragraph 1: Napenda kuzungumzia korona na jinsi tunavyoweza kushirikiana kuzuia ueneaji wake ili sote tubakie salama.

Paragraph 2: Balozi anaanza kwa kutoa historia ya ugonjwa huo, hasa nchini kwake, na anamalizia kwa kusema kwamba ametiwa moyo na matamko ya hivi karibuni ya Wizara ya Afya ya Tanzania yakitambua korona kuwa ni suala la kipaumbele kiafya nchini na hatua za Wizara kuwaelekeza wananchi kuchukua tahadhari muafaka kama vile kuepuka misongamano, kuvaa barakoa na kutokaribiana. Balozi anaendelea kusema kwamba huo ni ushauri mzuri wa Wizara na anawahimiza watu wote wautii.

Paragraph 3: Balozi anasema kwamba mbali na tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo, kuna vitu viwili muhimu katika kuzuia ugonjwa huo.

Paragraph 4: Kwanza, ili kujua kama juhudi zinazochukuliwa zinaleta matokeo yaliyotarajiwa, ni muhimu kukusanya na kutoa taarifa kuhusu wagonjwa na upimaji. Ndiyo maana ni muhimu kwa kila serikali ulimwenguni kulijuza Shirika la Afya Ulimwenguni idadi ya wagonjwa wake.

Paragraph 5: Nyenzo ya pili ni chanjo........Chanjo zimesaidia kuondosha baadhi ya magonjwa mabaya zaidi duniani...... Naihimiza serikali ya Tanzania kuitisha kongomano la wataalamu wake wa afya kuupitia upya ushuhuda wa chanjo.

Paragraph 6: .....Hapa Tanzania tulitenga Dola 16.4 milioni kupigana na korona tangu mgonjwa wa kwanza alipothibitishwa mwezi Machi 2020. Marekani iko tayari hata kuongeza zaidi ya juhudi hizo na tuko tayari kushirikiana na Tanzania kuushinda huu ugonjwa.

Paragraph7: Namaliza kwa maoni yangu binafsi. Mimi ni daktari ... niliyefanya kazi katika kitengo cha afya ya jamii kwa zaidi ya miaka 30 kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi. Nathibitisha kwamba hayo niliyoyasema yanafanya kazi. Ninawaasa Watanzania wote kuunga mkono hatua hizo ili tujilinde sote kiafya na wale tuwapendao.

Nimechukua muda kutafsiri aliyoyasema Balozi kwa kuwa nilipandwa na gadhabu kusoma yanayosemwa yalitamkwa na Balozi. Kumbe ni uzushi tu wa mwandishi anayekuwa na ajenda zake. Hakuna AGIZO lo lote alilotoa Balozi.
 
So you mean the weak, poor, have nots, women and childre, they can go to hell!
 
Hiyo elimu nikuonyeshe wewe?
Najua hujui nilichoandika hapo!

Tangu siku ya kwanza nilipokusoma hapa JF upo vile vile, huonyeshi maendeleo yoyote, ndiyo ilikuwa hoja yangu.

Ngoja nikukumbushe. Unaukumbuka ule mjadala wa Marehemu Sokoine, tulianzia hapo..., hadi leo ni disappointment tupu!
 
Reactions: Ole
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…