Ubalozi wa TANZANIA inchini UJERUMANI

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Nimepitia ktk website yao ktk kipengele cha utalii ambapo nimekuta hii information hapo chini
Je embassy zetu zote zinatangaza utalii wetu? au ni kwenye website tu au kuna mbinu anuai zingine kutolea mfano wa ubalozi wetu pale London?
Wadau mlioko konambalimbali tupeni infos ili tujue kama kweli wakenya wanatupiga bao kwa ugoigoi wetu au basi tu
 

Msanii, umenikumbusha, hivi karibuni nilipanda KLM, mle kwenye free magazine za mwenye madege wakenya wamejitangaza kama kurasa tano hivi, na wakachomekea kutangaza aliko zaliwa Obama, utalii hadi kilimanjaro wameiweka humo, yaani niliwaonea wivu mtakatifu, nikabaki tu kujiuliza hivi wabongo tumerogwa na nani? hatuwezi hata kudesa ya wenzetu tunayo ona yana faa kwa mustakabli wa taifa letu? yaani tunabakia kuwa wachumia tumbo tu bila kuangalia mbele yetu kuna ninini?

Tulivo fika amstadam tukisubilia kuunganisha ndege, nikasikia watasha wakiambizana walikuwa Kenya na kwamba wamespend 4 weeks na wakisifia kwamba ni kuzuri na wakipeana story za hapa napale kuhusu waliyo yaona huko!

Pamoja na watani zetu kuchomana moto na kuuana kama sisimizi kwenye uchaguzi wao, watatupiga bao la kisigino hivi hvi nasisi tutaendelea kubaki pale pale kama kapeto!

Hivi kweli hatuna vichwa safi Tz vya kututoa tulipo? tufanyeje jama?
 
Ni Kweli wamejitaidi kutangaza ila kingereza walichotumia hakivutiii kwa msomaji
neno THE SEALDUS GAME RESERVE, linatakiwa liwe "Selous Game Reserve" jina hili liliitwa baada ya Sir Frederick Selous Mwingereza na mtunza mazingira!
 
mfumo mbovuuu uliopo umeweza pia kuwafanya hata wenye nia njema kuwa wabovuuu...

hiyo mzee ni marketing strategies zilizotulia tuu amabazo nakiri wakenya wametuzidiii...

wabongo kazi ipooooo...TTB nasikia hata kichefuchefu kuitajaaaa...niliumia sana roho kuangalia taarifa ambayo KQ na TTB wamelaunch marketing campaign ya kupromote utaliii kenya...very smart move
 
Ni Kweli wamejitaidi kutangaza ila kingereza walichotumia hakivutiii kwa msomaji
neno THE SEALDUS GAME RESERVE, linatakiwa liwe "Selous Game Reserve" jina hili liliitwa baada ya Sir Frederick Selous Mwingereza na mtunza mazingira!

..Hicho pia ndicho kilichonivutia kuimwaga hapa jamvini maana hiko kiingereza ni maimuna. Ila wamejaribu maana najua kama wangefuata utawala bora wange wasiliana na BAKITA wawatafsirie kisha wabandike ktk website.

Mimi nashauri wasaidiwe ktk hilo pia (ingawa tunawalipa mishahara kwa kodi zetu)
 

Miaka ya hivi karibuni Tanzania imejitahidi kutangaza vivutio vya utalii ukilinganisha na miaka ya nyuma.Watalii wasiojua kwamba mlima Kilimanjaro uko Tanzania na si Kenya wamependa wenyewe kutojua.
Bodi ya utalii kwakushirikiana na balozi zetu waongeze juhudi zaidi kuhakikisha huu upuuzi wa nchi ya Kenya kuendelea kudanganya wageni vivutio wasikuwanavyo unadhibitiwa mara moja.
 

Yeah ni kweli! wanajitahidi these days kuitangaza Tanzania. Nimepita kwenye balozi mbili tatu Europe, nimeona jinsi wanavyojituma kututangaza. Kuna balozi moja wameweka mpaka TV screen kuubwa reception kwa ajili ya matangazo ya kitalii. Ila juhudi zaidi zinahitajika coz tulipo sasa BADO SANA!
 

Juzi juzi nilikuwa Disney land kupeleka familia yangu, nilichokutana nacho huko ni.....matangazo yahusuyo Kenya ni mengi mno, nilipoenda kwenye mbuga ndio kabisaa....kila kitu Kenya........nilipoingia dukani nilipata shida sana kuwa-convince jamaa (wauzaji) kuwa Mlima Kilimanjaro uko Tanzania.......confidently walikuwa wakiwaambia watu kuwa Mlima Kilimanjaro uko Kenya!!....well finally nilifanikiwa kuwa-convince.....very easily.....just "Google Earth na ku-point out the Mt kilimanjaro".......na wakakubali na hata waliniomba contacts zangu ili niwatumie informations zaidi kuhusu utalii Tanzania........mwenye informations please naomba uziweke hapa ili na watu wazisambaze

Well, tutaendelea kupiga kelele wee.........hazitatusaidia.......inabidi tuamke kweli kweli (aggresiveness).........

Rwabu ndugu yangu hauko peke yako.......yaani inatia uchungu sana kuwa hatuko serious............

Lile tangazo linalotoka CNN inabidi wawe wanabadilisha badilisha sasa na watume pia clip nyingine
 
Tatizo TTB na serikali wanataka vitu kwa bei rahisi na kwa njia fupi. Nilitengeneza DEMO ya tangazo la Tanzania liko kwenye jukwaa la burudani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…