Maneno ya hekima sana. Ila watu wengi wanafikiri kwamba ukitenda mema, mema yatakurudia kesho au keshokutwa yake,ambavyo sivyo.Mema yatakurudia baada ya muda mrefu sana pengine kwa watoto au wajukuu zako. Hii nimeshaiona. Ndo maana watu wengi wanashindwa kutenda wema kwa sababu malipo ya mema hayarudi haraka. Katika forum hii natarajia kuwaletea kisa cha Tenda wema tarajia mema kichomtokea mtu mmoja dar.Mambo mawili na makubwa hapa duniani kwetu wanadamu na yanakungoja kwa busara zako ili uchague. Kuna MAOVU na MEMA hayo yote ni kwa ajili yako ila kumbuka WEMA hauozi na UBAYA haulipi kwa hiyo kabla ya kutenda jambo KWANZA tafakari matokeo yake kwani ukipanda mbegu ya MAOVU na MAVUNO yake ni MAOVU pia. Mungu kakupa kila kitu akili unayo ufikirie na ndio maana Mungu alituumba wanadamu tofauti kabisa na Wanyama hivyo basi kumbuka mshahara wa dhambi ni MAUTI na Mtenda MEMA MUNGU humlipa kwa MEMA.
Note:
Ubaya hauna Cheo na Wema nao Hauozi, UKITENDA MEMA TARAJIA MEMA.
Maneno ya hekima sana. Ila watu wengi wanafikiri kwamba ukitenda mema, mema yatakurudia kesho au keshokutwa yake,ambavyo sivyo.Mema yatakurudia baada ya muda mrefu sana pengine kwa watoto au wajukuu zako. Hii nimeshaiona. Ndo maana watu wengi wanashindwa kutenda wema kwa sababu malipo ya mema hayarudi haraka. Katika forum hii natarajia kuwaletea kisa cha Tenda wema tarajia mema kichomtokea mtu mmoja dar.
Thanks TUMYUr right HYGEIA, Am looking forward kwa kuja kusoma kisa hicho, umeanisha vema sana ni kweli watu wengi wanataraji wakitenda mema basi kesho yake avune matunda yake, umenifurahisha sana uliposema sio lazima mema uyavune wewe mtendaji hata watoto wako wanaweza kuja kuvuna mema uliyoyatenda wewe baba yao, ama mama yao. Much respect to you.
Siku zote jitahidi kufanyia wenzako vile ambavyo ungependa kufanyiwa wewe. . .
Hii ni hadithi au?
Binadamu awe mwema siku zote mbona itakuwa kazi .....sasa shetani atabaki kufanya kazi gani duniani tukitenda mema siku zote.