ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,938
- 6,942
Wakuu salamu.
Tayari nakala za katiba pendekezwa zimefika katika mamlaka za serikali za kata. katika kata ninayoishi ambayo ndo inatengeneza makao makuu ya wilaya, mtendaji kata pekee ndiye kapewa nakala 900 za katiba inayopendekezwa.
Ni vigumu kila mtu kupata nakala yake hivyo mtendaji alicho kifanya amegawa katiba hizo kwa taasisi za serikali, ngos, mashirka ya dini, vikundi vilivyosajiliwa, wenyeviti wa vitongoji na makundi mengine. lengo ni kuwasaidia makundi hayo kama watakuwa na mijadala basi wasikose japo nakala tano za kufanyia rejea.
Sasa wasomi wa JF na hasa wale wanaotengeneza makundi mawili ya kuikubali au kuikataa katiba hii tunaomba mtupe mwongozo.
1. Wanaotaka tuikatae, kwa nini tupige kura ya hapana?
(a) Ni maeneo gani ambayo labda yamechakachuliwa ili yatusaidie kujua hila za waliochakachua?
2. Wanaosema tupige kura ya ndiyo, kwa nini tupige kura ya ndiyo?
(a) Kwa nini baadhi ya vipengele vilivyopendekezwa na wananchi kama sehem ya kusimamia uwajibikaji mlivitoa? mfano kumpuzisha mtu ubunge
(b) Kwa nini mlifuta kuanzishwa kwa tanganyika huru na kuamua kuianzisha Zanzibar huru yenye mamlaka kamili?
Hayo ni maswali chokozi ambayo naamini mkitupa ukweli itatusaidia kuijua katiba kwa haraka na hivyo kuandaa kura ya ndiyo au hapana.
Karibuni mtuelimishe. ni vizuri kutumia ulinganisho wa rasimu ya katiba na katiba pendekezwa ili kurahisha kuelewa.
Wabheja sana.