Uber na Bolt zijifunze kutoka kwa Indriver

Uber na Bolt zijifunze kutoka kwa Indriver

mkadiriajimajenzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2015
Posts
549
Reaction score
614
Indriver ni app bora kuwahi kutokea katika teknolojia ya usafiri nchini Tanzania kwa sababu zifuatazo:-

1). Abiria anapendekeza bei ya safari kulingana na uwezo wa mfuko wake na Inatoa mwanya wa majadiliano ya bei na dereva mpaka kufikia muafaka. (Ukizingatia Wabongo kwa kupenda ku-burgain, hii app inawafaa zaidi)

2). Usajili wake ni rahisi hasa kwa madereva,haiitaji kubadili card ya gari kuwa commercial na kubadilisha plate number, inahitajika dereva awe na leseni hai na gari iwe imekatiwa bima tu. (So, dereva yeyote anaweza jisajili na kuanza kupiga hela chap)

3). Ina option ya kukodi gari kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

App hii inapatikana kwenye Appstore (ios) na playstore (Android).
 
Uber atabaki kwa muda mrefu kuwa namba moja hapa nchini kwa huduma zake Bora japo Bei zao si rafiki kwa sie wenye kipato kiduchu
 
Back
Top Bottom