OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Ubidhaishaji (Commoditification)
Mbali na kitu hiki kuonekana kuwa kinawafanya watu wakae mbali na utu lakini tunapoendea tunapaswa kujua kuwa ubidhaishaji ni chanzo kikuu cha ajira kwa kipindi chetu hiki chenye ongezeko kubwa la watu huku kazi za viwandani na maofisini zikiwa hazitoshi.
UBIDHAISHAJI unapigwa vita na watu wachache huku wale positive economists na mabepari wakiona hili ndio swala suluhu,
Labda nionyeshe jinsi ubidhaishaji unapokuwa chanzo cha kipato na ajira nitatumia vitu vichache vingine mtaongezea wenyewe.
MUZIKI, Zamani muziki ulikuwa ni ugangwe haukutoa hela kwa wanamuziki wake, kwa Nchi za wenzetu mtawajua kina beethovens, Mozart nk ambao walikufa kawaida kipindi kile ilikuwa kawaida ila muziki ulipokuwa bidhaa mkawaona watu wenye mafanikio kama kina Michael Jackson nk, kwa Tanzania tunawajua wazee wetu ambao walifanya muziki kwa kujitolea hata kwa mziki wa kizazi kipya wakapata umaarufu bila pesa hivi sasa mnawaona kina Diamond, Alikiba nk wakipata hela nyingi kupitia muziki ambao wazee wetu waliofanya kwa muda mrefu.
Hapo utaona muziki umekuwa bidhaa na umekuwa chanzo cha kipato kwa walio wengi na watu wanaweza kuishi kupitia muziki, ila fikiria muziki ungekuwa kama ulivyokuwa awali je wangapi wangebaki kuwa masikini?
USHAURI (CONSULTATION), Kabla ya kitu hii kuwa bidhaa ilikuwa unaweza kumfuata yeyote ukamuuliza akakujibu bure kabisa, lakini leo hii watu wamejiajiri kutoa ushauri wa masuala mbali mbali kama ya kisheria, kibiashara, kimahusiano nk. Hii inamaanisha USHAURI umekuwa bidhaa, na ndio sababu watu wamejikuta wakipata ajira kupitia hilo
SEHEMU YA KULALA(Malazi), Zamani zetu sisi ilikuwa ukiwa mgeni kijiji furani unaweza kumuona yeyote na ukalala kwake bila malipo na ukakirimiwa vizuri, lakini huduma hii siku hizi imekuwa bidhaa na watu wanajiajiri kwa kujenga nyumba za wageni, unalipia unalala na kuendelea na shughuli zako
Haya ni machache kati ya mengi ambayo yamekuwa bidhaa na yanawapa vijana kipato kizuri kwa kiasi kikubwa.
Kwa wale wanoona ubidhaishaji kama ni kitu kibaya, waangalie kwanza ukuaji wa idadi ya watu na waangalie watu watapata kipato.
Watu wengi watadhani ubidhaishaji ni shida kwa kuwa leo chakula kinauzwa tofauti na enzi zetu chakula kilikuwa hakiuzwi, maji yalikuwa hayauzwi, wala choo tulikuwa hatulipii, unaenda kwa yeyote unaomba maji ya kunywa unapewa leo ukienda kuomba maji unaulizwa ya mia tano au buku nk, kwenye upande wa chakula ni hadi ukianguka ndio utapewa vinginevyo unaacha upate adabu na njaa yako, hapo ndio wengu huona ubidhaishaji umefanya utu kupotea, lakini ubaya wao hawatoi suluhu ya namna gani ya kuongeza kipato huku ukipinga ubidhaishaji.
Hali ya ubidhaishaji ni kwa dunia nzima, lakini kwa Afrika tuko nyuma ya muda ndio maana tumechelewa kufanya ubidhaishaji na tumechelewa kupata pesa, wenzetu walishatoka zamani kiasi
Kwa leo!
Signed
Oedipus