Ubinadamu kazi sana ungekuwa wewe ungefanyaje

Duduke

Senior Member
Joined
Jul 12, 2020
Posts
112
Reaction score
104
Maisha ya shule jamani!

Nipo hostel room tupo wawili wawili jamani mwezangu hajui kununua ndala za kuogea.semister ilopita tumetumia zangu hadi zikakatika zilivyokatika akawa anaazim next room badae mi nikaamua kununua nyingine akaachananaz zile za next room akaendelea tena kutumia zangu semista nyingine tena amefika bila ndala anaendelea kuogea zangu.

Yaani tunangojeana mtu akienda kuoga amsubiri mwezake nae akaoge imefika muda nimemzoea tu sasa Leo nilivaa sendo zake kuna mvua mvua bahati mbaya zimekatika nimemwambia samahani sendo zimekatika jamani katoa mshangao kiasi kwamba nimemwambia tu nitaenda kuzishona

Je, nikizishona si ataona aibu kuendelea kuvaa ndala zangu za kuogea dah yani nimejisikia vibaya nimejilaum kwanini nilizivaa
 
Rafiki yako sijui room mate wako ni mbinafsi na roho ya umasikini inamsumbua, mwambie kila mtu atumie vitu vyake kama anaweza kulipa ada anashindwaje kandambili?
 
Ni katika stage tu ya maisha hapo ndio unajifunza kuishi na watu wa tabia tofauti.
 
Rafiki yako sijui room mate wako ni mbinafsi na roho ya umasikini inamsumbua, mwambie kila mtu atumie vitu vyake kama anaweza kulipa ada anashindwaje kandambili?
Yan sijui ana shida gani anataka sharing kama home in relative
 
Niliwahi kaa na huyo dada anajua kununua viwalo tu lkn kuanzia dawa ya meno, lotion, sabuni hadi taulo za kike mpaka atumie zangu. Sikuwah msemesha ila nilinunua hilo begi jaza kila kitu na kufuli juu akahamia kutumia vya wengine.
 
Pole, watu hawafanani. Mnunulie sandles za migogo (za mipira ya matairi ya gari) kisha mpe kama zawadi.
 
Mkuu njia rahisi....chomeka zile office pini kwenye tundala kwako afuu,mtegee saa ya kuogaa hataridia tenaa.ila na wewe unaroho mbayaa ndalaa tu ingekuwa gari siunge sema mpaka asubui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…