Hakuna asiyejua kuwa Katiba Mpya ni majumuisho ya mustakabala ulio bora zaidi katika uendeshaji wa nchi kwa wakati husika.
Hayupo mwenye akili timamu anayeweza kupinga matumizi au ujio wa mustakabala kama huo.
Taabu gani makwetu Tanzania basi?
Kwa hakika ubinafsi uliopitiliza ndiye aliye mchawi wetu mkuu.
Kuangalia tu yaliyo maslahi binafsi na kujiweka kando kwa lolote lisilokuwa na maslahi ya moja kwa moja kwetu ni kikwazo kikubwa. Kama hatushiriki shughuli za wengine, kwa nini wao washiriki zetu?
Yaliwakuta kina Lissu, Mbowe, Mdude, Ben Sanane, Azory, Lijenje, Mawazo nk.
Yakawakuta kina Polepole, Ndugai, nk.
Hivi yuko wapi Job Ndugai? Yuko huru, hai au mfu?
Kwanini tusitake kumwona Ndugai kwa juhudi ile ile kama tuliyo nayo kwa wenzetu akina Ben, Lijenje, Azory na wote waliopotezwa?
Kwa mwendo huu yatawakuta kina Mpina.
Yanawakuta Ukraine na pia Palestina.
Yanatukuta kwenye bei za mafuta.
Mwendelezo ni kila mtu kula na wa kwao.
Batili ni batili tu. Bila ya kuzikabili batili zote kama zinavyokuja, tuupate wapi umoja wetu muhimu wa kushughulikia ya halali yote yakiwamo ya Katiba Mpya?
Maneno mazito toka kwake Askofu Bagonza ni ya kuzingatia:
Wapinzani si wamoja. Kuna wapinzani-Katiba Mpya na Wapinzani-Nusu Katiba Mpya. Kuna wapinzani-Mtungi na Wapinzani-Mahela. Kuna Wapinzani-Zanzibar huru na Wapinzani-Zanzibar Mkoa. Unahitajika muafaka kati ya wapinzani kabla ya muafaka wa kitaifa.
Tunahitaji muafaka baina yetu.
------------------
Source:
Askofu Bagonza: Taifa linahitaji miafaka, siyo muafaka