Ubinafsi unaua taifa

Ubinafsi unaua taifa

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,095
Reaction score
4,632
Tabia ya ubinafsi inaliua taifa. Mali ya taifa siyo ya mtu mmoja,siyo ya familia moja. Na watu wengine wanatuambia kwamba hakuna mtu mwenye hati miliki ya nchi hii wakati tunaona wao wenyewe ndio wana hati miliki ya nchi hii.

Kwa hiyo awamu bàada ya awamu ya viongozi: kila kiongozi anakula urefu wa kamba yake. Hajali maendeleo ya wote. Hayo atamwachia kiongozi mwingine wa baadaye,ambaye alipokuwa mdogo hakulala ndani ya nyumba na mifugo.

Kwa hiyo, you are kicking the can down the road. Unàahirisha kutanzua matatizo ndani ya nchi. Lakini watu wakishaona ishara kwamba ni watu wachache tu wanaofaidika na taifa, hapo ndio unaliua taifa.

Baadaye watu wanaelewa ubaya wa ubinafsi, wanafanya marekebisho, halafu wanajenga taifa lenye nguvu, lakini hiyo huwa inatokea katika taifa jingine. Yaani, kama DRC(kwa mfano) kuna ubinafsi unaiharibu nchi,marekebisho yanafanyika katika nchi nyingine, kwamba "tusifanye mambo kama wanavyofanya DRC"

Kwa hiyo ni imani ya political scientists wengi kwamba nchi ikiwa corrupt ndio basi tena.
 
Mkuu, wewe ni mtaalam katika fani ya 'Political Science'?

Hii mada umelalamika sana, lakini haieleweki unamlenga nani hasa, huoni kuwa hilo ni tatizo katika uandishi wako?

Unaandika kijumla jumla tu, unataka msomaji wako aelewe kitu gani?

Kama unaona nakuonea wewe kwa ulalamishi usiokuwa na lengo, basi elewa kwamba siyo wewe pekee mwenye tabia ya namna hiyo. Hii ni tabia mbovu sana ya kiTanzania, na ndiyo maana, hata hao unaowalalamikia hawastuki, kwa sababu wanajua huna uthubutu wa kutaja yeyote, matokeo yake wanapuuzia malalamishi yenu.

Kuna ugumu gani kuwa 'direct', kuwa kiongozi fulani kafanya hili na lile, na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa juu yake
 
Loh....huu uandishi wako ni shida.. Malalamiko yako hasa ni juu ya nini?
 
Mkuu, wewe ni mtaalam katika fani ya 'Political Science'?

Hii mada umelalamika sana, lakini haieleweki unamlenga nani hasa, huoni kuwa hilo ni tatizo katika uandishi wako?

Unaandika kijumla jumla tu, unataka msomaji wako aelewe kitu gani?

Kama unaona nakuonea wewe kwa ulalamishi usiokuwa na lengo, basi elewa kwamba siyo wewe pekee mwenye tabia ya namna hiyo. Hii ni tabia mbovu sana ya kiTanzania, na ndiyo maana, hata hao unaowalalamikia hawastuki, kwa sababu wanajua huna uthubutu wa kutaja yeyote, matokeo yake wanapuuzia malalamishi yenu.

Kuna ugumu gani kuwa 'direct', kuwa kiongozi fulani kafanya hili na lile, na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa juu yake
Ukimjua ni nani ndio utaelewa y anaongea hv..
*Was a first first son.
 
Ukimjua ni nani ndio utaelewa y anaongea hv..
*Was a first first son.
'Poppy Hatonn', member wa JF tokea 2021.

Sasa wewe 'TEMLO DA VINCA' unaongeza utata hapa, maana wewe na yeye ni kama mapacha, pamoja na kwamba wewe umekuwemo humu JF tokea 2013!

Hivi shida yenu ya kuandika kitu kikaeleweka na msomaji hasa ni ipi; hilo ndilo swali langu kwenu.

Naomba nieleweke, sipingi chochote alichoandika mkuu 'Poppy', shida yangu ni kuandika kiujumlajumla tu kiulalamishi, bila hata ya kutaja wala kuweka mifano halisi.
Tabia ya ubinafsi inaliua taifa. Mali ya taifa siyo ya mtu mmoja,siyo ya familia moja. Na watu wengine wanatuambia kwamba hakuna mtu mwenye hati miliki ya nchi hii wakati tunaona wao wenyewe ndio wana hati miliki ya nchi hii.

Kwa hiyo awamu bàada ya awamu ya viongozi: kila kiongozi anakula urefu wa kamba yake. Hajali maendeleo ya wote. Hayo atamwachia kiongozi mwingine wa baadaye,ambaye alipokuwa mdogo hakulala ndani ya nyumba na mifugo.
Nina hakika nipo upande mmoja na mwandishi wa haya maneno. Natamani tu angekuwa 'more direct' kuhusu anayozungumzia.

Haimsaidii yeyote, si hao wanaozungumziwa (sutwa), au hao wanaonyang'anywa, kwa kuandika kiujumla kwa mtindo huu.

Hata kama hatuwezi kuwapeleka mahakamani mbele za sheria, ni maoni yangu kwamba hawa watu angalau wawe wanatajwa ili watu wawajue kwa maovu wanayoyatenda.
 
Back
Top Bottom