Ubingwa leo lazima

Freetown

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2008
Posts
882
Reaction score
78
Jamani mliopo TZ tuleteeni matokeo ya ligi kuu bara
 
Yanga wamekuwa Bingwa leo kimizengwe,kuna mchezaji mmoja wa Prison ambaye alitakiwa atolewe,kwa bahati mbaya kibendera akaonyesha mchezaji mwingine tena ambaye alikuwa tegemeo la Prison.Kwa ufupi Yanga Bingwa,lakini kuna rufaa ya simba ambayo wamepeleka FIFA.Hilo ndo soka la bongo.
 

malila
Asante sana, huwa wanachelewa sana kuweka habari za michezo kwenye mtandao.
 
Hiyo rufaa ya Simba inatarajiwa kuwa na impact gani?
 
Kuna gazeti nimesoma,Hassanol yule wa simba anasema wameandika barua FIFA wakidai zile point zao walizopokonywa kwa kumchezesha mchezaji mwenye adhabu, ktk barua hiyo wanaomba bingwa asitangazwe mpaka rufaa yao itakaposikilizwa huko majuu,pia wameandaa na malipo ya dola 10,000.Sijui tofauti ya points kati yao na watoto wa Jangwani ni kiasi gani.Ukipata nafasi soma nipashe la jana lina habari ya rufaa hiyo na ukijaliwa soma sunday Observer utapata kila kitu pale
 
Duu, kwa hiyo mida hii kona ya Twiga na Jangwani ni mwendo wa dundiko, vanga na mchiriku kwa kwenda mbele? Au watu wanakesha ndani ya Kaunda kama kawa, I see I really miss my bongo life!
 
kama kawaida,dundiko,vanga,maji ya Ilala na chang`ombe,michips na mikuku,ili mradi kwa muda washabiki wanasahau shida na taabu zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…