dazu
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 365
- 76
Ni kwa muda mrefu sasa ubingwa wa ligi yetu umekua ukipokezana timu za simba na Yanga tu, na kwa jinsi mwaka huu muelekeo wa ligi unavyoendelea, ni wazi ubingwa utaelekea msimbazi au wakiteleza basi yanga iliyo nafasi ya pili. Timu ya mwisho kuchukua kombe nje ya yanga na simba ni mtibwa zaidi ya miaka 6 iliyopita. Maoni yangu ni kwamba hii imekua ikiua msisimko wa ligi yenyewe, hivyo hata kushindwa kupata timu nzuri ya taifa. Nakumbuka enzi za timu ya pamba ya akina Paul Rwechungura, Hussein Marsha, George Massatu, James Washokera, Fumo Felician, Hamza Mponda, Halfan Ngasa, na wengineo walivyokua wakileta changamoto kwenye ligi; au Reli ya akina Mkali Abdallah, Mbui Yondan, na wengine, ligi ilikua tamu sana na haitabiriki. Je Timu zetu za mikoani zimekua dhaifu sana? Au Simba na Yanga zimekua Strong sana, au kuna uchakachuaji?