Hadrianus
JF-Expert Member
- Feb 19, 2020
- 2,112
- 5,229
SIMBA &YANGA 20/21 MBIO ZA UBINGWA
1. UBORA WA VIKOSI
Simba SC Tanzania ina kikosi bora zaidi ya Young Africans Sports Club
2. MAKOCHA
Makocha wa timu zote mbili hawana CV kubwa sana. Sven wa Simba mafanikio yake makubwa ni kubeba kombe la mataifa ya Africa (AFCON) akiwa kama kocha msaidizi
Cedric Kaze huyu amewahi kupita academy ya Barcelona kama kocha, akaenda zake CANADA.
Kinachokuja kuwatofautisha ni aina ya futiboli wanayofundisha na mifumo. Sven wa Simba anaamini sana katika 4-2-3-1 mfumo ambao anaanza na mshambuliaji 1, kitu ambacho mashabiki wamekua wakilalama aanze na washambuliaji wawili.
Wakati Kaze akiamini sana katika 4-3-3 ambao unampa matokeo sana kwa sababu namba 3 hapa chini.
3. FIGHTING SPIRIT (MORALI YA UPAMBANAJI)
Kikosi cha Simba SC Tanzania ukikitizama katika mechi zake nyingi fighting spirit yake ipo chini au unaweza kusema ni ya kawaida sana, wanacheza mpira mwingi katikati ila huko mbele kumepoa
Yanga kitu pekee kinachowabeba ni FIGHTING SPIRIT, na hichi ndiyo kinaweza kuipa UBINGWA WA VPL 2020/2021. Wachezaji wa Yanga wanajituma sana, wanaonesha hamu ya kulitaka goli hata kama wameshatangulia kupata goli tofauti na Simba Sc wakipata goli 1 wanaanza kupoa na shida ya Simba wakitanguliwa ndiyo inakua mtihani sana.
Yanga wao wakitanguliwa, wanapambana sana kuchomoa goli na kutafuta bao la ushindi.
UBINGWA WA LIGI KUU 2020/2021
Kama Yanga wanautaka Ubingwa, waendelee kuwa na fighting spirit hii hii waliyonayo.
Kama Simba wanataka kuchukua kwa mara ya 4 mfululizo taji hili, wacheze kwa kupambania timu zaidi waoneshe ari zaidi.