Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Ukisikiliza sana hoja za pande mbili zinazokinzana kuhusiana na mchakato wa Katiba Mpya unaweza kuamini kuwa tatizo ni UKAWA au CCM. Naomba kupendekeza kuwa tatizo ambalo tunalishushudia na ambalo tumeshalishuhudia huko nyuma ni la kina zaidi. Ni kutokukubali ukweli ndio maana watu bado wana matumaini ya kupata katiba mpya.
Tatizo la Msingi ni uharamu mzima wa mchakato huu; hili nimelionesha toka Kikwete alipotangaza 'nia' yake ya kuanzisha mchakato huu akiwa mwenyewe ni mvunjaji mkubwa wa Katiba ya sasa. Ikumbukwe kuwa Katiba ya sasa hairuhusu uandikwaji wa Katiba Mpya na Rais wa Jamhuri ya Muungano hana Mamlaka wala Madaraka ya kuanzisha mchakato wa kufuta Katiba iliyomwingiza madarakani na kuanzisha Katiba Mpya.
Wanasiasa wetu, wanaharakati, na Watanzania kwa ujumla walipokubali uharamu huu uwe halali walikuwa wamekubali matokeo ya uharamu huo. Ikatungwa Sheria iliyoweka upendeleo wa wazi ndani ya CCM na tukakubali; tukaona sheria hiyo ilivyotengenezwa kuharibu mchakato mzima tukalalamika lakini tukakubali.
Sheria hiyo iliyotungwa na magenius wetu ikaweka kuwa wajumbe wote wa Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi kuwa ni wajumbe wa Bunge la Katiba. Hili wengine tulilipinga mapema lakini wanaharakati wetu walilikubali na kuwa sehemu ya mchakato huu haramu. Walijua toka mwanzo kwa kufanya hivyo 2/3 ya wajumbe wa Bunge la Katiba watakuwa ni wana CCM au watu wenye kusogeleana na kukonyezana na CCM kwa karibu!
Ukweli wa mambo unabakia kuwa mchakato huu hauendi popote. Mabingwa wetu watabishana, watasemana na kutunishiana macho lakini mchakato hauendi popote; fedha ishaliwa na Katiba Mpya haiji isipokuwa kama kwa kulazimisha. Hakuna uwezekano wowote ule wa kuwa na Katiba Mpya itakayoweza kutumika kwenye uchaguzi mkuu ujao. Kwa vile uwezekano huu haupo tunachoshuhudia sasa na tutakachoshuhudia wiki ijayo ni kuvunjika kwa mchakato huu na kama utaendelea tutashuhudia uharamu wake ukiongezwa kufanywa haramu.
Uhalali hautakuja kwa vikao, kwa makubaliano na kuombewa. Uhalali utakuja kwa kuufuta mchakato huu - siyo kuuahirisha tu - kukubali kuwa umekosewa toka mwanzo na hivyo kuacha uongozi ujao uanze mchakato upya. Lakini hata watu wakiombea na kufunga uharamu hauondoki kwani uharamu huu si mapepo.
MMM