TRIPLE H
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 651
- 349
Wakuu,
Salaam!
Katika kufuatilia fuatilia mambo hapa na pale ili kuongeza maarifa ndani yangu, nimejikuta natafakari kuhusu ubongo wa mwanadamu unavyofanya kazi na nikakumbuka kuna siku nilifundishwa ubongo unaweza kuharibiwa au kuathiriwa na vitu tunavyoviona hasa visivyo vya kawaida.
Kama tujuavyo ubongo una maeneo (regions) mbalimbali na kila eneo linafanya kazi yake; kuna eneo linaitwa Anterior Cingulate Cortex (ACC) ambalo uhusika na KUTUNZA MAADILI au kumsaidia binadamu awe na tabia njema na maadili mema kwenye maisha yake na jamii yake.
Lakini wataalam wa mambo haya wanadai eneo hili la ubongo (ACC) likiathirika au kuharibiwa, mwanadamu anakosa sifa ya kuwa binadamu. Anabaki na umbo la kibinadamu, lakini matendo na maisha yake kama mnyama!
Inaelezwa kuwa sehemu hii ya ubongo uhathiriwa na vitu vya ajabu ambavyo mtu anaviangalia kwa makini. Mfano kutazama picha/video za ngono, mauaji ya kikatiri, utesaji na mambo kama hayo uhathiri vibaya eneo hilo la ubongo.
Mtu akizoea kutazama picha/video za X (pornography) Cingulate cortex region uharibika/uathirika atua kwa atua mpaka mtu huyu anafikia atua ya kutamani kuwa kama wale watu aliowaona na anajawa nguvu za kutaka kuanza na ndio maana kasi ya utovu wa maadili katika ngono hivi sasa ni kubwa mno duniani kwa sababu watu wengi hususani vijana wanatazama sana porn videos. Ongezeko la mashoga, wasagaji, wabakaji nalo ni kubwa sana na wafanyao hayo hawashtuki wala kuukumiwa na dhamiri kama mwanzo. Akili (ACC) ishaharibiwa na kutazama porn videos.
Vitendo vya kutesa mtu hata kifo, kuchomana visu, kuchinjana kama wanyama, kupigana risasi na kuuana ovyo vinashamiri katika jamii zetu kutokana na yale tunayoyaona kwenye Television kila siku. Hayo yote ni matokeo ya kuathiriwa na vitu vibaya tunavyovitazama na sasa akili yetu imejaa unyama. Tunawaza na kuwawazia wenzetu mabaya tu siku zote. Hofu kwa Mwenyezi Mungu imepungua sana miongoni mwa jamii. Maisha ya wanadamu ni sawa na ya wanyama au yanaelekea kuwa kama ya wanyama. Akili inawaza na kutafakari UOVU, UOVU, UOVU!
Nini kifanyike, ni JAMBO LA MJADALA.