Ubora na udhaifu wa suzuki jimny

Naskia Spare zake ngumu kupatikana
Nadhani spare hua wanamaanisha za kuchinja. Ila spea mpya naona ziko nyingi madukani.
Nna suzuki swift na nmebadilisha spea kibao kama disc, bush za nyuma, wishbone za mbele, plug zote na kioo.
Kwa hiyo jimny pia spea zake zinapatikana madukani.
 
Ulaji wa mafuta ikoje mkuu? Pia kusafiri masafa marefu inahimili?
Gari yangu ishaenda Safari ndefu zifuatazo Dar-Mwanza mara 8, Dar-Arusha mara 6, Dar -Songea mar 1. Safari hizi zimefanyika toka 2011. Na Kuna kipindi ilienda Dar-Mwanza-Dar, Kisha Dar-Songea-Dar Tena ndani ya mwezi mmoja. Ina engine ya K6A, 660 cc, Turbo charged. Ulaji wa mafuta 12km/L na kwa Sasa ina milage ya 260,000Km

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Spear zake zipo ,Ila Ni kweli zina Bei ya juu lakini Ni genuine. Kwa mfano toka ninunue sijawahi kurekebisha engine tofauti ya kubadirisha plug pekee, kuhusu gearbox ilishawahi kushushwa kwa ajili ya kurekebisha kitu kidogo kilichokuwa kinasababisha kung'ang'ania gia namba 5,(Ni manual), Clutch plate sijawahi badirisha, pressure sijawahi badirisha, shock up ndio kwa mara ya kwanza ninatakiwa kubadirisha toka ije 2011. Kwa hiyo running cost ya hizi gari ni ndogo saana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzoefu wangu katika masafa marefu kimbia kwa speed Kati ya 80-100, maana haziko stable saana kutokana na shape yake. Ukikimbia speed kubwa saana, Kisha ukutane na basi au roli lazima gari iyumbe. Au ukipita sehemu zenye upepo mkali Kama maeneo ya Same na Mwanga lazima uwe mpole na speed Kati ya 50-80

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kwa habari zinazohusu mashamba, vi vyema kununua pick up either Hilux, hardbody au landrover, hautojuta. Maana Kuna siku utabeba mbolea, viwatilifu, gunia mbili za parachichi, na kufanyia vitu vingine vingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana mkuu, umeniongezea ujasiri.
 
hii 12 km per liter ni kwa Safari za mjini sio?
 
Gari zuri sana spare za kumwaga ila bei kinapita sehemu yoyote hakikwamwi. Ila kina mashine ndogo cc 1300 hakiwezi kuhimili mwendo mrefu na mikiki mingi ndio maana watu wengi wanaviua vinataka misele kidogo
.nakaaa Arusha kitafika marangu?
 
Hebu pitia post hiyo namba 26
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…