Ubora wa afya yako ya akili

Ubora wa afya yako ya akili

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
282
Reaction score
275
UBORA WA AFYA AKO YA AKILI.

Ipo haja kubwa ya kutoa elimu zaidi kuhusu maana ya afya ya akili na jinsi ya kujitambua iwapo uko na changamoto hii, watu wengi wanahesabu afya ya akili ni ukichaa ambapo imani hii inawafanya hata wanapokuwa hawako sawa wanaona ni kawaida.

Lakini kwa uhalisia changamoto ya afya ya akili ni kubwa sana na inazidi kuchukua nafasi kubwa kwa athari zake kwa jamii, ipo haja ya kulisemea hili kwa mapana yake.

Jambo ninalotaka utambue leo hii ni kwamba, kuwa na afya njema soo kutokuwa na changamoto za afya ya akili mambo yanayopelekea changamoto za afya ya akili ni ya kawaida ila tunayoyazembea na mwisho yanageuka kuwa changamoto kubwa , hivyo changamoto ama matatizo yatakuja, ikiwa unahisi kutokuwa na matatizo ndio kuwa huna changamoto basi badili huenda mtazamo wako unakufanya kuwa na changamoto zaidi, kuwa na afya bora ya akili ni pamoja na jinsi unavyokabiliana na changamoto / matatizo yako.

Hii inamanisha inagusa uwezo wako wa kufanya maamzi,mapokeo lakini hadi uwezo wa kusiliana, badilisha kasumba hii na kisaidie kizazi chako, jinsi ya kukabiliana na changamoto ndio ubora wa afya ya akili ili kila mmoja aanze kujiangalia changamoto zake huwa anazipita vipi na fikra zake zikoje juu ya changamoto zake?

Ziko mbinu nyingi za kuondokana na changamoto hizi, ikiwemo kusoma vitabu, kumuona mshauri, kufanya tafakuri ya ndani na kadha.

Ikiwa utahitaji ushauri sadifu kwa ajili ya kuboresha afya yako ya akili, maamuzi yako, hisia zako, uchungu wako na mbinu za kufikia malengo yako wasiliana nami leo, kwa ajili ya mazungumzo chanya ya ubora wako, unaweza kuwasiliana nami kupitia (inbox,sms, ama tumia website www.echu.co.tz).

MAISHA NI HAYA HAYA WA KUBADILIKA NI WEWE

Echu.
 
Ukiona mtu ameanza kunywa visungura sijui Kidimbwi basi afya ya akili tayari imeshazinguwa na ndio tatizo kubwa lililopo sasa hivi.
 
Ukiona mtu ameanza kunywa visungura sijui Kidimbwi basi afya ya akili tayari imeshazinguwa na ndio tatizo kubwa lililopo sasa hivi.
Ni kweli kabisa na watu kwavile hatupendi majukumu tunamuacha aendelee, sio shida zetu kumbe baadae anaweza kuja kuathiri kizazi chako bila hata wewe kutegemea.
 
Back
Top Bottom