UBORA wa elimu na ajira

UBORA wa elimu na ajira

Msanumbi

Member
Joined
Sep 15, 2018
Posts
43
Reaction score
36
Tanzania hususani idara ya elimu bado tuna mapungufu kadha ambayo yakifanyiwa kazi basi soko la ajira litakua kwa Kasi na vijana kupungua kukaa vijiweni na kutumia mihadharati,

Mfano mitaala elimu ya sasa ni tofauti na miaka ya 2000 kurudi nyuma,
Tulikua na masomo kama sayansi kilimo, stadi za kazi na maaarifa ya jamii , haya masomo yalisaidia Sana kumfunza kijana akitoka shule aweze kujiajiri lakini kwa sasa ni bora ufaulu na sio ufaulu bora, wengi husoma kwa bidii ili kuja kuajiriwa serekalini na sio kujiajiri, ikumbukwe soko la ajira serekalini ni dogo hvyo tunapaswa kuwa na wigo mkubwa wa kujiajiri ili uchumi wa Nchi ukue na Kodi iongezeke ili kuleta maendeleo katka jamii na kwa mtu mmoja mmoja,

Tuna haja ya kubadili mitaala kwa sababu ya ongezeko la wahitimu kuwa wengi mtaani na hawana ajira na walitegemea kuajiriwa baada ya kumaliza masomo yao, mfano wa ajira na elimu zilizotoka mwaka huu mwez wa 7 , ukiaangalia waliotuma maombi walikua zaid ya laki8 upande Wa kada ya elimu,na kada ya afya walikua zaid ya laki2 lakini waliohitajika katka kada zote mbili hawazidi elfu17, hapo unapata picha ni kiasi gani mitaala elimu ilivyo haiko sawa.
 
Back
Top Bottom