Kama huwezi kujitafutia walimu na in mvivu wa kujisomea mwenyewe open utatoka huna kitu kichwani, kitu wanafunzi wengi wanapata tatizo nalo, lakini mitaala yao ni mizuri kama kawaida na wana manuals nzuri,ukitaka kusoma hapo lazima ujipange kutumia muda wako vizuri. Hakuna mtu atakukumbusha leo kuna kipindi njoo darasani, Mfano kuna wanafunzi wa sheria ambao walienda law school na walifanya vizuri kupita wale wa vyuo vingine. Pia wana library Ina vitabu vizuri sana. Wanafunzi wanaoona pagumu ni wale wanaoshindwa kuwatumia walimu wa pale vizuri. Ukitaka tatizo eneo Fulani wanakusaidia kukufafanulia.
Wako wengi makazini na wanafanya vizuri tu. Ila mpaka umuulize ulipata wapi degree yako kitu ambacho si rahisi.
1. Huwa nalinganisha wanafunzi wa OUT na kuku wa kienyeji (wanaojitafutia chakula wenyewe) kuliko kuku wa kigeni - wanaofugwa - (wanaopewa chakula muda ukifika).
2. Ukisoma OUT nilichojifunza ni kwamba hakuna kulala - yaani, kama huna culture ya kujisomea na kutawala vizuri muda wako huwezi kufaulu maana kila kitu kinategemea bidii yako ya kukitafuta.
3. Mimi pia nasoma OUT na ninachokifanya ni kupata 'course outlines' ya masomo ninayoyachukua na kuona ni vitabu gani nihitaji na natafuta fedha na kuvnunua vitabu na materials mengine (sheria nyingi au case laws nazipata kwenye mtandao). Kutokana na 'workload' yangu sipati muda wa kwenda 'tuition'.
4. Actually, niliacha kwenda tuition kwa maana siku moja jamaa mmoja alikuwa akitushawishi tumhonge mwalimu hela eti atufanyie assignments akidai "kusoma kwa siku hizi ni tofauti na zamani. Siku hizi tunasoma ili kupande cheo na kupata mshahara mzuri na siyo kuelewa. Huyo njemba aliwashaiwshi karibu asilimia kubwa ya darasa na siku waliyopanga kupeleka hizo fedha nikaona nikienda wanaweza kudhani nawachimba mkwara maana sikuwa tayari kuoneshwa assignment bali nilitaka nijipime mwenyewe kuliko kupata maksi ambazo sistahili.
5. Hii ilinifanya niwe negative kuhusu tuitions na tangu siku hiyo siendi tena na wala sidhani kama nitaenda hata siku moja.
6. Wapo na wanafunzi wengine waliosusia na huwa tukikutana tunajikumbusha "eti hata assignement watu wanataka waoneshwe na test au mtihani itakuwaje?"
7. Mimi nimejiwekea utaratibu wa kusoma kila siku nikiwa kazini (muda ambao sina kazi ya kufanya) na nyumbani. Nimejipangia ratiba yangu kuwa baada ya masaa ya kazi nafika nyumbani, napumzika na kisha nalala masaa 6. Yakiisha naamka na kuanza kusoma hadi muda wa kwenda kazini tena siku inayofuata. Nina muda wa kupumzika (kwa maana ya ku'relax' pia na kufanya mazoezi nisije nikawa 'anti-social'). Huenda ratiba yangu ni tofauti na ratiba za watu wengine. Naingia ofisini mara nyingi saa 4:30 (asubuhi) na kutoka saa 2:00 au 3:00 (usiku). Kama ningekuwa natoka nyumbani saa 12:00 au 1:00 asubuhi na kurudi saa 11 jioni ningepanga ratiba yangu pia inipe muda wa kupumzika na masaa 6 ya kulala usingizi. Hii ni nzuri kwa afya.
8. Kwa hiyo, achana kabisa na watu wanaodhani kiwango cha elimu OUT kiko chini maana inategemea mtu mwenyewe na jinsi anavyo'manage' muda wake. Hata kama ukiwa kwenye chuo bora kiasi gani kama wewe mwenyewe hujitumi haikusaidii kitu. Inabidi kufanya 'sacrifices' otherwise itakuwa vigumu kufaulu. Kitu kingine ni kwamba ukisoma kwa kuwategemea sana walimu unaweza kuwa 'disappointed'. Inabidi uwe kweli na 'discipline' ya kupanga na kutekeleza mipango yako mwenyewe kwa asilimia kubwa kama unataka kufaulu OUT.
9. I really like kuwa kama kuku wa kienyeji kwa maana katika kujitafutia chakula mwenyewe nagundua vitu vingi, ambavyo kama ningekuwa kwenye conventional unviversity nisingeweza kupata. Lakini mimi tangu zamani ni mtu ninayependa kujisomea peke yangu. Huwa ninatumia kanuni kwamba kama mwalimu amesoma kitu fualni na kukielewa na kisha kutufundisha kwa nini mimi nishindwe kukielewa nikikisoma peke yangu? What's wrong with me? Hii inanifanya nisikate tamaa niendelee kutafuta "chakula" hadi nipate!
10.OUT inafunza bidijii ya kujituma na kuwajibika maana bila ya kufanya hivi hakuna kufaulu!