Ubora wa ukali ulioletwa na wafanyabiashara wa vibali ulithibitishwa na TMDA?

Ubora wa ukali ulioletwa na wafanyabiashara wa vibali ulithibitishwa na TMDA?

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Kabla ya matumizi ya sukari iliyoletwa na wafanyabiashara kwa njia ya vibali walitakiwa TMDA watoke hadharani kuwaelezea wananchi kuwa sukari hiyo iliyoletwa ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Taarifa hii mpaka leo haijatolewa na Mamlaka husika na wako kimya jambo ambalo linaleta wasiwasi kuwa sukari hii muda wake ulikwishapita.

Mwaka jana nchi ya jirani ya Kenya kuna sukari iliyoletwa nchini humo na muda wake ulikwishapita na baada ya Serikali kugundua hilo ilibidi ile sukari imwagwe baharini.

Tuwe tunapewa taarifa na mamlaka husika kuhusu ubora ya vyakula tunavyoletewa kutoka nje.

Ninaiomba TMDA itoke hadharani na kuihakikishia umma kuwa sukari iliyoletwa kwa vibali ilikuwa salama kwa matumizi ya binadamu vinginevyo hatutawaelewa.
 
Sidhani, kwa nchi hii ilivyojiozea, mambo ya hovyo ni mengi mnoo
 
Upo sahihi. Hata hivyo kama mwananchi mmoja mmoja ukibaini sukari ime expire report kwenye mamlaka husika. Ukiona hawakuelewi report kwenye Meza ya Rais | The President Table na tutafikisha moja kwa moja kwa Rais
 
Back
Top Bottom