Ubora wa Yondo Sister katika muziki wake!

Ubora wa Yondo Sister katika muziki wake!

Blue Bahari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,851
Reaction score
2,171
Wakuu mambo vipi!
Leo natua kwenu kama mgeni wa jukwaa hili (sababu sijawahi post kuhusu masuala ya burudani).
Niende moja kwa moja kwenye mada, hoja yangu ninayoiwasilisha kwenu inamuhusu mwanadada machachari kabisa kuwahi kuwepo ktk tasnia ya music hapa Africa.

Licha ya kipaji chake alichokua nacho, lakini cha ajabu binafsi nimeshangaa sana kutokuona ktk tovuti mbali mbali zikimuelezea kama ni mmojawapo wa mwanamziki bora wa kike kuwahi kuwepo Africa. Wanamziki wa kike wanaouzungumzwa (kwamba "the greatest") ktk mitandao, kwangu Mimi naona kuna wengi ambao hawamfikii Yondo Sister lakini tovuti hizo zinawazungumzia wengine kama vile Mbilie Bell, Miriam Makeba, Brenda, n.k.

Licha ya ukweli kwamba kuna style mbali mbali za mziki, lakini hoja yangu inajumuisha vipaji ktk style zote kwa wanawake. Na ukiingia Wikipedia, wanamtanabaisha kama ndiye Queen of Kwasa Kwasa & Lumba. Sasa kama yeye ndiyo malkia wa miondoko hiyo, kwa nini ktkt tovuti mbali mbali hawamtaji kama ni mwanamziki wa kike bora kabisa kuwahi kutokea Africa?
Wewe mdau wa mziki una lipi la kuzungumza juu ya mwanamama huyu?
 
kapalamsenga,
Hata Mimi nyimbo zake sichoki kuzoangalia. Lakini nimeshangaa ktk mitandao mbali mbali hatajwi kabisa ( kwa mujibu wa websites na blogu nilizotembelea nyingi tu)
 
Hao wakongwe siyo wa kizazi ya You tube, Muziki wao utaishi milele
Hata Mimi nyimbo zake sichoki kuzoangalia. Lakini nimeshangaa ktk mitandao mbali mbali hatajwi kabisa ( kwa mujibu wa websites na blogu nilizotembelea nyingi tu)
 
Nyimbo zake bora kama vile mbuta mbutu, po na tembe, Wapi yo n.k
Zoote utazipata hapa.
 
Mimi mwenyewe huwa nashangazwa na hilo...kama namna ulivyo shangaa Wewe...hadi leo hii huwa Nina amini kwamba yondo sister bado hajapaya mpinzani wake

Mwanamama alikua na sauti nzuri iliyosheheni melody kali sana zisizo na mfano
 
Ndiyo ushangae sasa. Mimi mwenyewe nimebaki nimeduwaaa😱😱😱😱🙄
 
Hakuwa na kipaji wale soukous stars walikua wanambeba kwa kila kitu !! Usimuweke level za kina mbilia bell wala Tshala muana kabisa huyo!
 
Kumbuka yondo sister alikuja kama upepo kwa kwetu uku tunaweza kusema kama saida kaloli, alivuma galfa na nyimbo nzuri baada ya hapo yupo kama kumbu kumbu tu

Sawa na NIMON TOKILALA unamkumbuka kwaiyo ni vigumu kukuta anazungumziwa sana kama hao uliowataja ambao walifanya mziki kwa mda mrefu
 
REJESHO HURU,
Lakini Mkuu we unaonaje? anapaswa kuenziwa mahali popote pale (even in internet platforms) au hastahili hizo tunu?
 
Teh kwenye huu uzi ma legends wa muziki wa zamani utawajua tu, vijana wa bongofleva the likes of Heaven Sent wanaukimbia
 
Teh kwenye huu uzi ma legends wa muziki wa zamani utawajua tu, vijana wa bongofleva the likes of Heaven Sent wanaukimbia
Hahaa me nimecheza sana masong ya Yondo sister
"Yondo sister mwana mama eeeh mawa
Tiii; tinti tinti tintitii tinti tinti"
Hahahaha c.c@Atoto
 
Hivi kuna mdada afrika aliyeimba nyimbo nzuri kama Monique Seka?
Inawezekana hakuna kama huyo... Lakini mkuu kwani we Yondo sister unamzunguziaje? Je, hafai kupewa tunu mahala popote pale?
 
Back
Top Bottom