Habel John
Member
- Jul 18, 2022
- 10
- 8
Miongoni mwa filamu zenye watazamaji wengi duniani ni zile ambazo huwa na wahusika ambao ni binadamu wenye uwezo wa ajabu kama vile; kupaa angani, kukimbia kwa kasi sana, kutoonekana, kuona mbali nakadhalika. Wahusika hawa ni kama Spiderman, Wonder woman, Captain America, Iron man, Batman, Black Panther na wengine wengi unaowatazama katika filamu zinazotengenezwa na studio za Marvel na DC nchini marekani.Je, umewahi kufikiria kuwa watu kama hawa huishi miongoni mwetu na tumekuwa tukikutana nao kwenye shughuli za kila siku kama kazini, kwenye michezo na masomoni?
Watu hawa hawana uwezo uliopitiliza wa kwenye filamu kama kukimbia kwa kasi ya mwanga au kunyanyua magari, bali wana maboresho madogomadogo; kimwili, katika uzazi na mfumo wa fahamu. Dhana hii imepewa jina la ‘uboreshaji wa binadamu’, kwani humwezesha mtu kuvuka vikwazo ambavyo binadamu wa kawaida asingeweza kuvivuka.
Sambamba na hayo; Maradhi, ajali na kadiri umri unavyosonga mpaka kufikia miaka 65 baadhi ya mifumo ya mwili hupungua usanifu katika utendaji kazi ikiwemo; kuona, kusikia, kutembea nakadhalika, hivyo watu huanza kutafuta namna ya kuboresha mifumo hiyo kwa namna tofauti tofauti kimwili, kiutambuzi na katika afya ya uzazi kama ifuatavyo;
A) UBORESHAJI WA KIMWILI
Matumizi ya vifaa kama vinasa sauti huongeza usikivu kwa wenye matatizo ya usikivu au kuboresha mawasiliano. Mwanasayansi kutoka nchini Japani amegundua miwani ambayo inaweza kutambua hali ya mtu kama vile kusema uongo, hasira au furaha.
Watu hawa hawana uwezo uliopitiliza wa kwenye filamu kama kukimbia kwa kasi ya mwanga au kunyanyua magari, bali wana maboresho madogomadogo; kimwili, katika uzazi na mfumo wa fahamu. Dhana hii imepewa jina la ‘uboreshaji wa binadamu’, kwani humwezesha mtu kuvuka vikwazo ambavyo binadamu wa kawaida asingeweza kuvivuka.
Sambamba na hayo; Maradhi, ajali na kadiri umri unavyosonga mpaka kufikia miaka 65 baadhi ya mifumo ya mwili hupungua usanifu katika utendaji kazi ikiwemo; kuona, kusikia, kutembea nakadhalika, hivyo watu huanza kutafuta namna ya kuboresha mifumo hiyo kwa namna tofauti tofauti kimwili, kiutambuzi na katika afya ya uzazi kama ifuatavyo;
A) UBORESHAJI WA KIMWILI
Matumizi ya vifaa kama vinasa sauti huongeza usikivu kwa wenye matatizo ya usikivu au kuboresha mawasiliano. Mwanasayansi kutoka nchini Japani amegundua miwani ambayo inaweza kutambua hali ya mtu kama vile kusema uongo, hasira au furaha.
| Kipandikizi cha koklea (www.medgadget.com) | Miwani ya ajabu (konayajamii.blogspot.com) |
Kemikali za homoni ‘anabolic steroids’ hutumika kuongeza nguvu na kuongeza maumbile ya mwili (kwa mfano anadrol, oxandrin na dianabol). Mafuta ya mnyonyo na habati soda zinaweza kuotesha nywele ikiwa upara ni tatizo kwako.
kuongeza misuli (https://medistar.is) | Kuotesha nywele (www.thesun.co.uk) |
Hakuna asiyetaka kuwa na mwonekano mzuri, hivyo matumizi ya dawa za kupunguza na kuongeza uzito yameshamiri. Pia dawa kama mlungu lungu zinatumika kuongeza makalio kwa wanawake na mkongoraa kwa ajili ya dhakari kwa vijana wa kiume.
| Kupunguza uzito (m.youtube.com) | Kuongeza makalio (www.taifaleo.nation.co.ke) |
Mazoezi yanaweza kukujengea misuli na kubadili usemi wa jeni na kutibu udhoofu wa misuli ‘disuse atrophy’ (kutotumia misuli vilivyo mwili hautopoteza nguvu kuistawisha na badala yake itaanza kudhoofika na kuwa midogo)
Disuse atrophy (www.varierfurniture.com) |
kupangilia meno kwa chuma (billingsorthodontics.com)
Kabla na baada ya kupangilia meno kwa chuma (www.bbc.com/news/uk-england)
BOTOX ni dawa itokanayo na sumu ya bakteria aitwaye Clostridium botulinum, dawa hii ni ya ajabu kwani hutoa mikunjo usoni na sehemu nyingine hivyo kukupa mwonekano wa ujana daima.
Kabla, baada ya siku 2 na baada ya siku 14 za kutumia BOTOX (www.arlingtonoms.com/facial-rejuvination)
Kabla na baada ya kutumia botox (eng.idhospital.com)
Kable na baada ya kutumia Botox (www.juverne.com)
Matumizi ya erythropoietin (EPO) husaidia katika riadha kwa kuhamasisha utengenezaji wa seli nyekundu za damu ambazo husafirisha hewa ya oksijeni ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa nguvu mwilini. Kafeini inaweza kutumika kukuboreshea utendaji kazi kwa kuhamasisha mfumo mkuu wa neva.
| Uboreshaji katika mbio (www.europarl.europa.eu) |
Pia vifaa mbalimbali vinaweza kutumika kama mbadala wa viungo vyako vya mwili vyenye hitilafu; kongosho bandia hufanya kazi ya kurekebisha viwango vya sukari mwilini endapo kongosho yako imeshindwa kufanya kazi, na kitengeneza kasi cha moyo ‘Pacemaker’ hutumika kuhamasisha misuli na kudhibiti mapigo yako ya moyo endapo unaudhaifu katika mapigo ya moyo
| Kongosho bandia (www.easterneye.biz) | Kisaidizi cha moyo (www.Kisamedlineplus.gov) |
Teknolojia za ubadilishaji wa jeni imekua ni suluhisho kwa seli na tishu zenye kuleta hitilafu, teknolojia ya CRISPR-Cas9 inaruhusu jeni kuongezwa, kubadilishwa au kuondolewa kwenye jenomu, ambapo ilimuwezesha mwanasayansi wa kichina kufanya mabadiliko ya jeni kwa mapacha ambapo iliwafanya kuwa na kinga madhubuki dhidi ya VVU.
Mapacha waliozaliwa na kinga dhidi ya VVU (www.teslarati.com) |
B) UBORESHAJI WA KIUTAMBUZI
Eicosapentaenoic (EPA) inatumika kwa ajili ya kuongeza upeo wa kufikiri na madawa mengine yapo mbioni kutibu matatizo ya kisaikolojia kama skizofrenia (ugonjwa wa akili unaosababisha fikira na hisia zisizo za kawaida).
Je, unasumbuliwa na mfadhaiko au usingizi utokanao na ‘narcolepsy’? (hali inayokufanya ulale kila wakati). Dawa kama vile Modafinil inaweza kuwa suluhisho la tatizo lako na haina madhara sana ukilinganisha na caffeine ambayo wengi wanatumia kutibu usingizi.
Hali ya usingizi inayopelekea kushindwa kujizuia kulala (www.nature.com) |
C) UBORESHAJI WA AFYA YA UZAZI
Ni zaidi ya wenzi milioni 186 katika nchi zinazoendelea wanachangamoto ya ugumba ambao mara nyingi unasababishwa na kuharibika kizazi kutokana na maambukizi katika via vya uzazi ikiwemo kisonono na klamidia. Ugumba unaweza kupelekea unyanyapaa ambapo wahusika hutengwa na kunyanyapaliwa na jamii, talaka na ugumu wa maisha.
Teknolojia saidizi za uzazi zinazoweza kutatua tatizo hili ni kama vile upandikizaji wa mbegu, uterasi, urutubishaji yai nje ya mwili na kupandikiza yai lililorutubishwa (kiinitete) kwa mwanamke kwa wenzi ambao mifumo yao ya uzazi imepata hitilafu kutokana na maradhi ya via vya uzazi, lakini pia upandikizaji huo unaweza kufanyika kwa mwanamke mwingine (Surrogate motherhood).
TEKNOLOJIA YA CYBORG
Teknolojia hii ilianza miaka ya 1960 ambapo neno ‘cyborg’ lilimaanisha kiumbe ambaye ameundwa kwa viungo vya kiroboti (bandia) na kibinadamu.
Mnamo mwaka 2017, Muingereza aitwaye Peter aligunduliwa kuwa na ugonjwa unaosababisha kudhoofika kwa misuli mwili mzima ujulikanao kama ‘Motor neuron disorder’, (MND), hivyo kushindwa kula na kupumua kulimfanya akubali baadhi ya mifumo yake ya kimwili kuwa ya kiroboti ili kusaidia maisha yake kwa kuwekewa mashine za upumuaji, sauti ya bandia, mikono ya roboti, na upasuaji wa laser kurekebisha macho yake ili yaweze kuongoza kompyuta na vifaa vingine.
Peter Scott-Morgan akawa ndiye cyborg wa kwanza duniani ambapo alifariki dunia mwezi Julai mwaka 2022 akiwa na umri wa miaka 64. Vile vile Peter alifanikiwa kurekodi filamu ya maandishi iitwayo Peter: The Human Cyborg
Peter Scott-Morgan (sw.imdailyheadlines.com) |
Peter Scott-Morgan (sw.imdailyheadlines.com) |
Baadhi ya mitazamo juu ya uboreshaji wa binaadamu hupinga kwa kuzingatia usalama wa viboreshaji (kwa mfano dawa za EPO zinaweza kupelekea mshituko wa moyo), kupoteza uhalisia wa kibinadamu kama vile teknolojia ya cyborg na pia kutokuwepo kwa usawa katika kumudu, kwani baadhi ya huduma hizo ni ghali.
Baadhi ya mitazamo inaunga mkono uboreshaji wa binadamu kwa kuwa ni jukumu la watu kujinasua na vikwazo katika afya na kiutendaji panapo uwezo wa kufanya hivyo na wanapaswa kuwa huru kukuza miili yao kwa teknolojia kama ilivyokuwa kwa Peter.
Attachments
Upvote
16