SoC04 Uboreshaji wa miundombinu ya barabara za vijijini ili kujenga uchumi bora kwa wananchi pamoja na halmashauri

SoC04 Uboreshaji wa miundombinu ya barabara za vijijini ili kujenga uchumi bora kwa wananchi pamoja na halmashauri

Tanzania Tuitakayo competition threads

Rashidi Muya

New Member
Joined
Jun 10, 2023
Posts
4
Reaction score
1
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajitahidi sana kuboresha na kukarabati miundombinu ya barabara lengo likiwa ni kurahisisha mnyororo wa thamani kwa bidha, mazao shughuri nyingine za kiuchumi ili ziweze kufanyika kwa urahisi lakini jitihada hizi za uboreshaji zimepewa kipaumbele katika miundombinu iliyopo halmashaurini yaani mijini pamoja na barabara kuu pekee. Hali hii ni tofauti na barabara za vijijini ambazo zimetelekezwa kwa kiasi kikubwa, barabara za vijijini nyingi zimetengenezwa kwa kuchongwa na matrekta na wakati wa mvua zinakuwa na changamoto na kusababisha shughuri nyingi kukwama.

Barabara za vijijini kuwa katika hali mbaya changamoto nyingi huibuka ambazo kwa kiasi kikubwa hukwamisha maendeleo ya vijijini, bidhaa kupanda bei ni miongoni mwa changamoto inayowakumba wakazi wa vijijini pindi barabara zikikubwa na mvua kwasababu wafanya biashara hutumia gharama kubwa kuwalipa wenye wenye vyombo vya usafiri kuleta bidhaa madukani na gharama hizi huongezwa katika bei za bidhaa ili waweze kupata faida, lakini gharama hizi sio katika bidhaa tu lakini kwa wakazi pia wanapotaka kusafiri kwenda sehemu nyingine basi nauli inakuwa tofauti kati kipindi cha mvua na jua kwasababu kipindi cha mvua barabara zimekua na matope, madimbwi kujaa maji na kufanya barabara ziwe ngumu kupitika kwa urahisi na haraka. Wagonjwa kushindwa kufikishwa vituo vya afya pamoja na hospitali za wilaya kwa haraka kwasababu barabara haziruhusu kwenda kwa haraka hivyo basi baadhi ya wagonjwa hufia njiani lakini wajawazito baadhi huamua kujifungulia tu majumbani ili kuepusha adha ya barabarani na wale wanaoamua kwenda vituo vya afya baadhi yao hujifungulia njiani kwasababu safari ya kwenda kituo cha afya sio kwa urahisi kutokana na matope, mashimo kujaa maji na kusababisha madimbwi.

Wananchi wa vijijini wanategemea kulima mazao yao kisha kuyauza ili kujipatia kipato ambacho kitainua uchumi wao, wapo wakulima wanaouzia mazao yao shambani na pia wapo wakulima wanaoamua wenyewe kusafirisha mazao yao na kwenda kuyauza masokoni, hawa wanaosafirisha wanakutana na changamoto kubwa ya barabara kipindi cha msimu wa mvua kwasababu barabara nyingi zinakuwa zimeharibika na kupitika kwakwe ni kwa shida sana, hawa wanaosafirisha wakati mwingine wamevuna mazao yakiwa shambani mvua inawakuta kwahiyo hawana budi kusubiri mvua zikate ndio waweze kusafirisha sasa wakati wa kusubiri mvua zikate mazao yanaharibika na wale wanaokutwa na mvua barabarani magari yanakwama zaidi ya siku 3 mpaka 4 mpaka kufika sokoni mazao yamepoteza ubora na kushuka thamani mkulima anapata hasara na hivyo hivyo kwa wafanyabiashara wanaoenda kununua mazao hayo na kuyaleta sokoni adha hizi huwakumba na kupoteza mitaji yao. Ili tujenge Tanzania tuitakayo kwanini hizi barabara zisiboreshwe ili kurahisisha shughuri za kibiashara kwa hawa wakulima na wafanya biashara.

Ili tuijenge Tanzania tuitakayo kwa miaka ijayo, Tanzania ambayo uchumi utakua imara kwa wananchi wote wa kijijini pamoja na mijini basi mambo haya yanapaswa kutekelezwa;

1: Barabara za vijijini zinatakiwa kuingizwa kwenye TARURA ili hizi barabara zitengenezwe hata kama sio katika kiwango cha lami lakini itapendeza zikitengenezwa katika kiwango cha changarawe kitu ambacho kitazifanya zitumike kwa urahisi hata kipindi cha mvua na kupunguza adha kwa waenda kwa miguu pamoja na waendesha vyombo vya usafiri mfano magari na pikipiki. Baada ya kutengenezwa TARURA wanapaswa kutenga muda maalumu (inaweza kuwa kila baada ya miaka miwili) wa kuzitembelea na kuzikagua ili kutambua hali zake na zile ambazo zitakua zinachangamoto basi ziweze kushughulikiwa.

2: Madiwani pamoja na wenyeviti wa vijiji tunatambua wanayatenda makubwa kwa wananchi wao lakini kwa kiasi kikubwa wanajisahau katika kuhakikisha barabara zinakarabatiwa na mara kadhaa tumeona wanasubiri mpaka kipindi cha uchaguzi kikiwa kinakaribia ndipo utawaona wakishughulikia hii inatufanya tuamini wanafanya hivyo ili waweze kuchaguliwa na endapo wakichaguliwa hutokomea mpaka wakati wa uchaguzi tena ukikaribia, ili tuijenge Tanzania tuitakayo wanatakiwa kuyafanya hayo hata katika miaka ambayo sio ya uchaguzi kwasababu barabara hizi hazitumiki tu nyakati za uchaguzi, wanapaswa kutambua miundombinu ya barabara ni sehemu kubwa ya kuboresha uchumi kwa taifa na kwa raia wake.

3: Halmashauri za wilaya zinakusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali ili kuweza kuboresha, kutengeneza na kukarabati sekta mbalimbali kama vile afya, elimu, barabara n.k lakini moja ya chanzo kikubwa cha mapato ni ushuru unaokusanywa kwenye mazao, mazao ambayo yanalimwa vijijini kwa kiasi kikubwa. Hivyo basi kwa kukuona hilo halmashauri zetu zipaswa kuzitazama barabara za vijijini kwa jicho la tatu ili ziboreshwe ili kurahisisha usafirishaji wa hayo mazao na halmashauri nazo zitaweza kukusanya ushuru kwa kiwango kikubwa na hatimae sekta nyingine zitaboreshwa kulingana na uhitaji kupitia mapato hayo.

Hivyo basi serikali kuu kupitia serikali zake saidizi za chini pamoja na wenyeviti wa vijiji na madiwani wanapaswa kuziangalia hizi barabara za vijijini ili tuweze kuijenga Tanzania tuitakayo kwa miaka mi 5 au 10 ijayo, Tanzania ambayo huu uchumi wa kati tunaouzungumzia basi hata kwa wananchi wetu wauone kwa kuwawekea miundombinu rafiki ambayo itaweza kurahisisha suala zima la usafirishaji kwa wananchi, wakulima na wafanya biashara.
 
Upvote 4
Back
Top Bottom