Hopper lyfer
New Member
- Aug 31, 2022
- 4
- 4
Ili Mwanadamu yoyote aweze kufanikiwa na kupiga hatua katika nyanja mbalimbali lazima awe na afya iliyo imara na Njema, hivyo Afya ni suara Muhimu Kwa Taifa lolote lile.
Katika kuifikia Tanzania tuitakayo katika suala la Afya lazima tufanye na tuongeze vitu vifuatavyo
1: UONGEZAJI WA HOSPITALI NA VIFAA VYA KISASA KWA KILA WILAYA
Kwa kiasi Kikubwa Serikali yetu ya Tanzania imejitahidi katika sekta ya Afya lakini hiyo haitoshi hivyo juhudi katika Kuongeza Hospitali Mbalimbali za Magonjwa yanayowasumbua watu Ambayo hayapewi kipaumbele sana lakini athari zake ni kubwa mfano Hospitali za Magonjwa ya Moyo, Figo, macho, pia hospitali za Mama na Mtoto ziweze kuongezeka vifaa vya kisasa na vijengwe Kwa wingi hususani maeneo ya Vijijini ili kuokoa Maisha ya Watanzania kusudi Nguvu kazi isipotee Kwa vifo vitokanavyo na Magonjwa hayo, Kwa kufanya hivyo tutaweza kujenga Taifa imara Leye vijana wenye Nguvu na afya imara.
2: UWEKAJI WA UTARATIBU MZURI JUU YA UANDIKISHAJI WA VITUO VYA AFYA PAMOJA NA UZINGATIAJI WA SIFA ZA KUAJIRI MADAKTARI
Misingi mibovu imechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la vituo vya afya visivyokuwa na sifa jambo ambalo limepelekea vifo na kuhatarisha maisha ya watu Kwa kuwaletea ulemavu wa kudumu.
Hivyo Kuwekwe Mpango thabiti wa kuvitambua vituo vya afya vyote nchini hususani maeneo ya mjini ambapo Kwa kiasi Kikubwa vituo hivyo vya afya vinaongezeka Kwa Kasi, Mpango huu unaweza kutekelezwa Kwa Kusajiri vitu vyote vya afya kama maabara, dispensari, famasi na hospitali zote zinazohitaji kutoa huduma za afya Kwa kuzingatia Vigezo na ubora wa vituo hivyo.
Pia Kusimamia Kwa ukaribu uajiri wa madaktari wenye sifa Kwa kuepuka Kuajiri kwa njia ya Rushwa ,hii unaweza kutekelezwa kwa kuzingatia Matokeo ya waajiriwa watarajiwa lakini pia Uwezo wa kutoa huduma Kwa uweredi.
3: USHIRIKIANO NA USOMESHAJI WA MADAKTARI KATIKA NCHI ZILIZOENDELEA KATIKA MASUALA YA AFYA.
Si jambo geni kusikia mtu ameenda kutibiwa nje ya nchi kama India hii ni kutokana na hospitali zetu kutoweza kutibu baadhi ya Magonjwa kutokana na kutokuwa na vifaa na hospitali Bora kmza kutibu magonjwa hayo.
Hivyo Wizara ya Afya Kwa kushirikiana na serikali iweze kuingiamikataba ya makubaliano ya Kusomesha madaktari Kkatika nchi zilizoendelea kiafya mfano,Kila Mwaka Serikali itenge bajeti ya kuwasomesha Madakatari100 mpaka 200 wa Magonjwa Yale ambayo yanaonekana Changamoto kutibika nchini kwetu, Kwa kufanya hivyo tunaweza kupanua wigo mpana wa madaktari Bingwa na wenye Uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa mbalimbali.
Pia serikali iweze kuingia makubaliano na nchi zilizoendelea katika suala Zima la Ujengaji wa hospitali za kisasa za kutibu magonjwa yenye changamoto nchini mwetu, Kupitia makubaliano haya tunaweza kujenga hospitali za kisasa ambazo zitaweza kutoa huduma Bora za afya na kuweza kupunguza gharama ya watanzania kwenda kutibiwa nje ya nchi.
4: UTOAJI WA ELIMU ZA AFYA KWA WANANCHI NA KUWEKA UTARATIBU MZURI NA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA.
Elimu ndiyo inayomtoa mtu kutoka kwenye Giza kumpeleka kwenye mwanga, hivyo katika suala la Afya ni vyema Watanzania wakapatiwa elimu kuhusiana na Magonjwa Mbalimbali ili tuweze kuepuka na athari zitakazoweza kutokea mbeleni Kwa kutojua.
Elimu hiyo inaweza kutolewa kupitia semina Mbalimbali,kwenye vyombo vya habari, Mitandao ya Kijamii lakini pia hata mitandao ya Simu Kwa kuwataka WANANCHI waweze kuchukua tahadhari mapema kabla ya ugonjwa haujatokea
Pia katika suala la uboreshaji wa kutoa huduma za afya serikali kupitia Wizara ya Afya waweke mikakati itakayowezesha kutoa huduma Kwa ustadi na weredi wa Hali ya juu Kwa kupunguza Mrundikano wa wagonjwa hospitalini, kutoa huduma Kwa wakati, kuishi misingi ya Huduma za afya katika kuhakikisha huduma zinaboreshwa kila kukicha kwasababu Kwa kufanya hivyo tutaweza kujenga Taifa Bora na lenye watu imara na wenye afya na nguvu za kutosha.
5: MATUMIZI YA MIFUMO YA KISASA YA TEKNOLOJIA KATIKA SEKTA YA AFYA
Uandaaji wa mifumo ya kisasa kama database itakayoweza kufatilia mwenendo wa afya ya Mtu kuanzia mtoto anapozaliwa mpaka anapofariki hii itaweza kurahisisha ufatiliaji wa afya za WANANCHI Kwa ukaribu Kwa kujua takwimu za afya ya Mtu kuanzia Magonjwa yanayomsumbua, Magroup ya Damu ambapo tutaweza kuondokewa na uhaba wa uchangiaji wa damu lakini pia kukupunguza Vifo na athari zitokanazo na Magonjwa Mbalimbali.
Mifumo hiyo itaweza kutumika popote pale nchini hususani mtu anapotaka kupatiwa huduma fulani, Kwa kufanya hivi tutaweza kuondokana na athari zinazoweza kusababisha vifo vitokanavyo na Magonjwa yasiyopatiwa matibabu.
JINA: JOHN ELIYA HAULE
NAMBA ZA SIMU:0753199038
EMAIL:johnhaule1111@gmail.com

Upvote
2