Uboreshaji wa viwanja vya mpira nchini

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Nimekuja na ushauri baada ya kuona ligi yetu inazidi kukua na mpira kwa ujumla.

Nashauri, TFF na serikali ni wakati sasa wa kuboresha viwanja vyetu vya mpira kama ifuatavyo;-

Kwa kuanza, serikali igharamie nyasi bandia kwa viwanja vya mpira kwa kila kanda. Tumeona TFF wakiruhusu timu kuchagua uwanja wowote ndani ya nchi, hivyo hivi viwanja vitatumika tu hata kama hiyo kanda haina timu ya ligi kuu. Pia hivyo viwanja vitatumika kwenye ligi za chini za daraja la kwanza au pili, au hata ligi za mikoa. Kwa kweli mashabiki ambao wameishawahi kucheza mpira kwenye viwanja vizuri
watakubaliana na hili. Viwanja vibaya vinapoteza ball kontro ya mpira jamani!

NB: Wapo watakaosema hivyo viwanja ni vya CCM. Ni kweli ni mali ya CCM kiumiliki, lakini vilijengwa na wanachi kwa kuchangia nguvu kazi na pesa. Kwahiyo, sidhani kama CCM watagoma kutoa sehemu ya pichi tu kwa ajili ya kuendeleza michezo, halafu wenyewe wabaki na kupangisha frame nje ya uwanja.

CCM wakigoma, basi serikali ianze mpango wa kujenga viwanja simple kama vya azam kwa kila kanda ili kukuza michezo, kwa sababu michezo ni ajira, na ni silaha ya kuleta amani ndani ya Tanzania. Yaani Watanzania wengine hujikita zaidi kufuatilia michezo kuliko siasa, hivyo ukiendeleza michezo, basi hata ukiiba rasilimali Watanzania wengine hawana habari!

Viwanja vya mpira viboreshwe!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Soka linatoka nyasi bandia wewe unataka kuturudisha, zikarabatiwe na vipigwe nyasi halisi
 
Soka linatoka nyasi bandia wewe unataka kuturudisha, zikarabatiwe na vipigwe nyasi halisi
Nimependekeza nyasi bandia kwa sababu inaonekana mameneja wa viwanja hivi vya CCM wameshindwa kuvimwagilia.

Kwa mfano, mwaka jana (2021), Azam walitoa fedha kwa ajili ya kukarabati uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Tabora. Kweli ukarabati ulifanyika kiasi chake ila nyasi zilioteshwa vizuri tu kqa ajili ya kuchezea nusu fainali ya FA! Tangu nusu fainali kuisha, uwanja unamwagiliwa kwa kusuasua, mpaka ukoka umeanza kukauka.


Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…