Pre GE2025 Uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura wakamilika rasmi mkoani Dodoma na Singida

Pre GE2025 Uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura wakamilika rasmi mkoani Dodoma na Singida

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Siku ya jana Tume Huru Ya Uchaguzi ilikamilisha uboreshaji wa Daftari lake la kudumu lkatika mikoa ya Dodoma na Singida, ambapo uboreshaji katika maeneo hayo ulianza tarehe 25 Septemba 2024 na kumalizika rasmi tarehe 01 Oktoba 2024.

Zoezi hilo lilianza rasmi mwezi Julai katika mikoa ya Kigoma, Tabora, na Katavi, kabla ya kuendelea katika mikoa ya Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, na Manyara, ikihusisha Halmashauri za Wilaya za Babati, Hanang, Mbulu, na Mji wa Babati.

JAJI 1.jpg

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kazi hiyo ya kusasisha daftari hilo la kudumu la wapiga kura ilihusisha baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dodoma, Mkoa wa Singida, na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Manyara.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa wadau wa uchaguzi jijini Dodoma, Mhe. Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk, alifafanua kuwa mzunguko wa tano wa uboreshaji ulijumuisha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Halmashauri za Wilaya za Bahi, Chamwino, na Kongwa.

Aidha, maeneo ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Wilaya za Kiteto na Simanjiro mkoani Manyara, pamoja na Mkoa wa Singida, yalishahusishwa katika zoezi hilo kna kuongeza kuwa kikawaida vituo vya uandikishaji hufunguliwa kila siku kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

Katika mkutano mwingine wa wadau uliofanyika mkoani Singida, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari, alieleza kuwa Tume imechukua hatua za kiteknolojia kwa kuboresha mfumo wa uandikishaji.

Mfumo huo mpya unamruhusu mpiga kura aliyesajiliwa kuweza kuboresha taarifa zake au kubadilisha kituo cha kupigia kura kwa kutumia simu au kompyuta. Hatua hii inalenga kurahisisha mchakato mzima wa uboreshaji wa daftari.

Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura inatarajiwa kukamilika mwezi Machi 2025.

Zoezi hili ni sehemu muhimu ya maandalizi kuelekea uchaguzi ujao, likiwa na lengo la kuhakikisha wapiga kura wanapata fursa ya kuboresha taarifa zao kwa wakati.

Soma Pia
 
Back
Top Bottom