KERO Ubovu wa bara bara ya Mbezi msumi na kutojengwa kwa daraja

KERO Ubovu wa bara bara ya Mbezi msumi na kutojengwa kwa daraja

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Barabara ya Mbezi Msumi kutoka Mbezi mpaka njiapanda ya mbopo na Msumi imeharibika sana, daraja toka lilipo bomoka mwaka 2023 January tukaambiwa litatengenezwa ujenzi wa barabara utakapoanza mwezi wa tatu 2023 lakini hakuna kilichofanyika,

Tukaahidiwa ujenzi kuanza mwezi wa nane lakini pia haikufanyika, mpaka leo hatujui nini kinaendelea, wananchi wamejichanga kurekebisha daraja ilimradi kupunguza gharama za usafiri,, ila mvua ikinyesha mfululizo hapatapitika.

Waziri na mkuu wa mkoa Chalamila atusaidie , kama ujenzi ni bado sana watujengee daraja na barabara ipigwe greda wananchi tuendelee na maisha, usafiri umekua mgumu sana,kwa wenye magari magari kila siku yanaenda gereji juu ya ubovu wa barabara
 
Back
Top Bottom