Ubovu wa sera na mitaala ya elimu 2023 - kurudisha ufundi sekondari ni kukosa dira na mipango

Ubovu wa sera na mitaala ya elimu 2023 - kurudisha ufundi sekondari ni kukosa dira na mipango

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Watanzania hii fursa ya kurekebisha mitaala ni fursa adhimu sana, ni nafasi ya kuweka mambo mengi sawa lakini fursa hiyo inaweza kupotezwa na watu wachache bila kuwa na maono yoyote wakavuruga.

Mpaka leo najiuliza ni mtaalamu gani anayeweza kutoa mapendekezo butu na kujaribu kuvuruga dira za taifa za maendeleo.

Labda mimi nitangaze conflict of interest kuwa mimi ni mhandisi,

sasa napenda kuwapeleka kwenye historia kidogo


mwaka 1961 wakati tunapata uhuru, taifa halikuwa na "tertiary education", tulichokifanya ni kurekebisha mitaala kuingiza study za kazi na kubadirisha umri wa kuanza na kumaliza shule ili elimu ya chini ili elimu hiyo itoe wafanyakazi.

hiyo haikuwa kutengeneza best education system bali mazingira yaliyokuwepo yalitulazimu. na kuingiza hayo kuna vitu tulivitrade off.

miaka ya 70 tukaingiza ufundi sekondari lengo likiwa ni lile lile.


hapa tulipo tumefanikiwa kutengeneza mfumo wa elimu uliokamilika wenye

  • primary
  • secondary
  • tertiary
tulichotegemea ni marekebisho haya sasa yajikite katika kuhakikisha kila stage ibebe majukumu yake ya msingi sasa.


moja ya chimbuko la ubovu wa elimu ni mchanganyiko tuliokuwa nao.


mimi kama mhandisi najua kuwa kumekuwa na "myth" kwamba vijana wanaotoka technical schools ni wazuri kuliko ma injinia lakini niwaambie haya ni maneno ya layman asiyejua anachokisema.

labda kuelezea kidogo kuhusu hilo ni kwamba vyuo vikuu hawana practical training nyingi, na kawaida vyuo vikuu vinatakiwa kutoa watu wa menejiment. hivyo hawa wanasoma maelezo zaidi lakini mtu asiyejua setup ya engineering field hastahili kutengeneza sera wala mitaala ya kuelekeza namna field hiyo inavyoweza kuzalisha wataalamu. Mtu yeyote anayepata practical training nyingi ukimpeleka kwenye field anaonekana kukijua hicho kitu zaidi na yule asiye na practical husita sita.

hivyo hivyo ukimchukua kijana aliyemaliza darasa la saba akaenda kariakoo kwa amafundi akashinda anachezea simu, huyo darasa la saba ukimuweka na mtu aliyetoka technical school kuchezea simu wa kariakoo anamshinda mbali wa technical school. planers wa mambo ya elimu ni watu wanaotakiwa kujua dira wanakotakiwa kuelekea lakini si kurudisha mambo ya hatua za nyuma.

lakini wanasema boti inapoanza safari wakati hakuna plani inayoeleweka kuwa tunaenda wapi itashinda baharini ikizunguka, akishika nahodha huyu anapeleka mashariki, akishika huyu anarudisha magaribi akija mwingine utasikia wakati tunaelekea mashariki upepo ulikuwa kidogo hivyo anaacha magharibi na kurudi mashariki tena.


hii sera na mitaala ilitakiwa tuone inaimarisha mfumo wa veta na sekondari zibaki kufanya kazi zake za msingi.

sera na mitaala ni vibovu kwa kuwa utafiti haukufanyika kujua changamoto ni zipi na hivyo mabadiriko yajikite kutatua nini.


bado tuna nafasi ya kurekebisha, ustawi wa jamii yetu kwa vizazi vyetu ni bora kuliko mda na rasilimali tulizokwisha poteza. ni bora tujipe mda wa kutosha kufanya vitu sahihi
 
Mkuu iko ivi Ata wizara ya elimu na sayansi wanafahamu policy nzuri ya elimu ndio msingi wa maendeleo ya nchi
Lakini isivyo bahati before ya kupata nafasi wanakuwa na maono na nia ya dhati ya kuleta mabadiliko
Ila bahada ya kupata nafasi sijui nini kinawakuta......
Africa [emoji288] we have long way to go......
 
Mkuu umeeleweka, kwa muundo wa masomo ya sekondar, masom gan unaona sio ya muhim?
bado narudia inahitajika kufanyika utafiti.

msingi wa mabadiriko umetoka kwenye malalamiko ya wananchi kuwa elimu yetu ni mbovu.

ukifanyika utafiti zaidi utabainisha ubovu na huo ubovu utatoa dira ya elimu yetu ya sasa iko mbovu kiasi gani.

hoja ni kwamba tulitengeneza mfumo wa elimu tukiamini uko sahihi, wakati wa utekelezaji yakaibainika mapungufu na hayo mapungufu ndiyo watu wanatumia kusema elimu ni mbovu.

jambo kwanza ni kuyatafuta haya na yatatueleza kila kitu
 
Mkuu iko ivi Ata wizara ya elimu na sayansi wanafahamu policy nzuri ya elimu ndio msingi wa maendeleo ya nchi
Lakini isivyo bahati before ya kupata nafasi wanakuwa na maono na nia ya dhati ya kuleta mabadiliko
Ila bahada ya kupata nafasi sijui nini kinawakuta......
Africa [emoji288] we have long way to go......
Tuna shida inayotoka kwenye ubovu wa mitaala huo huo. malengo watu wanaweka vizuri lakini wanashindwa kutengeneza timu ya kubeba hayo ndipo watu wanapeana posho.

jambo moja ninalojua ni kwamba sekita binafsi ndiyo tunaweza kubeba hili na likafanyika.

hakuna taasisi ya umma au mtumishi wa umma anayeweza kuthubutu kuwaambia wanasiasa kuwa wamepotoka, kwamba siasa zetu hazijafika kwenye destination ya demokrasi hivyo tu review mitaala kwa kuonyesha ni wapi tumejikwaa na ni wapi turekebishe.

ni mtumishi gani anaweza kuthubutu kusema elimu ya kukalili majina viongozi na tarehe siyo elimu bali watoto waeleweshwe tulikotoka mpaka tulipo.

mtoto leo hii akimaliza darasa la saba anajua kutaja tarehe za matukio tu na majina ya watu.

hajui machifu walipatikana vipi, hajui utendaji wao ulikuwa vipi, hajui serikali zao walizitengeneza vipi, hajui kwa nini tuliamua kuachana na uchifu.


mtoto hajui kuchagua mfumo wa demokrasia tulifuata nini? tangu tumeanza utekelezaji ukoje? na je malengo yetu ni nini?


lazima siasa na historia zimpe picha mtoto tulikotoka ni wapi, tuliko ni wapi na tunataka kwenda wapi.


ukimchukua mtoto ukampeleka uwanja wa kukimbia na kupokezana vijiti, akatazama wanavyofanya akipewa akipewa kijiti utaona na yeye anakimbia.


elimu inatakiwa kumpa picha mtoto kinachoendelea ni kitu gani na kinafanyika kwa vipi. ukiweza kumjengea mtoto taswila hiyo wakati hakuwepo uwanjani na ukampa kijiti akakimbia vilevile hiyo ndiyo dhana ya elimu.

ila sasa kuitekeleza unaweza kujikuta unamweleza mtoto mambo ambayo hayamjengei taswila, unkaa kueleza wakimbiaji walikuwa wangapi, kila mwaka aliyeshinda ni nani, n.k yaani unamweleza mtoto mambo ambayo ukimaliza kumweleza ukampa kijiti hajui akifanyie nini.

hayo ndiyo watu wakiona wanasema elimu yetu mbovu.
 
Mkuu umeeleweka, kwa muundo wa masomo ya sekondar, masom gan unaona sio ya muhim?
alternatively ni kutoa muda, kwa watanzania kutoa maandiko kama vitabu kuelezea changamoto hii,

hii inaweza kuwa a very good research badala ya kuchukua watu fulani kufanya utafiti na kulimit views za watu.
 
Back
Top Bottom