Tuwapongeze sana vijana wamefanya kazi nzuri. Nilichokiona leo ni uoga wa wachezaji wetu kwa wachezaji wakubwa wa mataifa mengine na papara za kupiga pasi bila umakini hasa Mzize ila wakiamua kucheza boli wanaweza. Wanahitaji mtaalamu wa saikolojia kuwapa kujiamini ligi yetu ni bora kwasasa.
Mbinu ya kukaba hadi mpinzani anachoka nasi kuanza kushambulia imetulipa. Twende nayo mechi na DRC.
Wachezaji waongeze mazoezi ya kukimbia sana beach, stamina na kasi ya kukaba na kushambulia.
Otherwise kelele zetu mashabiki ziendelee zinaleta matokeo chanya. Tuwaponde wachezaji kila wakichemsha hasa Feitoto ambae alikuwa na nafasi nzuri ya kufunga kwa ujinga akampasia Balua aliekuwa nyuma. Huyu kijana Fei ana kipaji kikubwa ila mashabiki tunahitaji akioneshe.
Timu imecheza rafu nyingi za kipumbavu na kupewa kadi nyingi ambao labda zingezaa red card, hili lisijirudie.
Gamondi aache kumpiga benchi Mwamnyeto sababu alizubaa mno kuondoa Mpira aliouzuia Baka, Nondo akawa hajielewi kabisa badala ya kuingilia na kuanua Mpira ambao ulizaa goli la kijinga. Mpira ule Job angeanua!
Hongera Kocha Morocco leo umepanga timu nzuri na imetupa raha.