Ubovu wa Uwanja wa Taifa maarufu kwa Mkapa

mikedean

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2018
Posts
3,267
Reaction score
4,634
Maarufu kama kwa mkapa.Huu ni uwanja wa taifa letu Tanzania upo Chang'ombe-jirani na Chuo cha ualimu Duce au kambi ya JKT-mgulani.

Uwanja huu umejengwa kisasa lakin miundombinu ya uwanja huu ni mbovu kupindukia.sina hakika na ubora wa pitch kwa kuwa sijaikanyaga au kuiona kwa ukaribu.Lakin mazingira mengine nje na pitch ni mabovu sana kuanzia viti hasa huku upande wa mashabiki wa Yanga,upande wa simba viti ni vizuri kwa sababu vilinunuliwa vipya baada ya mashabiki wa simba kuving'oa .

viti vichafu, vimechakaa havifai kukaliwa.pia rangi zake za kuta zimefubaa zinatakiwa zipakwe vizuri.Ngazi za kupanda juu zipo hovyo tu.hazijanakshiwa vizuri.

suala lililonikera zaidi ni VYOO.Vyoo vya uwanja ni vibovu sana.havina taa.Imagine mechi za Afcon zimechezwa usiku lakin kwenye vyoo vya kiume hakuna taa,masink mabovu yanavujisha maji.Yaani ukiingia unakutana na Bwawa la maji,ukihamia kingine hali ni ileile.Vyoo vya kike ndo viko vizuri.Wanaume wengi wanaenda kwenye vyoo vya kike kwa sababu ya uchache wa wanawake katika mechi.Hii ni hatari.

Ikiwa kuna makato kwa ajili ya uwanja,TFF na serikali kazi yao ya usimamizi wa uwanja inawashinda lakin siamini kama wanashindwa kununua taa za kwenye vyoo au kurekebisha njia za maji kwenye vyoo.Huu ni uzembe na Meneja wa uwanja anapaswa kufukuzwa hata kesho.Inasikitisha sana,pale kuna wachina wanasimania pia sasa sijui hilo hawalioni??

pia kuna changamoto nyingi sana pale yani nyingine wadau muongezee ili uwanja uwe na hadhi nzuri sawa na idadi ya watu inaobeba.Tusijisifu tu kuwa uwanja ni wa 6 kwa ukubwa Afrika lakini miundombinu ni mbovu.

sasa tunaweza kujiuliza je,pesa za makato kwa ajili ya uwanja tunayoambiwa yanaenda kufanya uwanjani au yanaishia kwenye vidomo ya wapigaji?
 
Achilia mbali kujaa maji lakini hata sounding systerm ni mbovu kabisa ina mwangwi sijui wataalamugani walifunga vifaa vya matangazo pale
 
Waswahili hatuwezi kutunza vyetu! Uwanja ulianza kutumika nadhani 2007 na leo ndio umechoka kiasi hicho! Ila na sisi mashabiki tunachangia sana uhalibifu wa viwanja vyetu! Mfano wale waliong'oa viti kipindi kile ........
 
Siku moja nimefika kwenye ule uwanja hakika ni ngumu kuamini kwamba ni uwanja wa mpira. Ni kama gofu la ma vampire, lina vyoo vya hovyo sana.
 
Ata pitch nayo imepoteza ubora wake kutokana na matendo ya kishirikina vile wachezaji wakiwa wanaingia kwenye mechi humwaga au kuchimbia madawa........Haya malalamiko nilisiki juzi tu watunzaji wa uwanja wakiyatoa

Tatizo kubwa ni sisi wananchi wenyewe tunashindwa kutunza vitu vyetu
 
Maarufu kama kwa mkapa.Huu ni uwanja wa taifa letu Tanzania upo Chang'ombe-jirani na Chuo cha ualimu Duce au kambi ya JKT-mgulani.

Uwanja huu umejengwa kisasa lakin miundombinu ya uwanja huu ni mbovu kupindukia.sina hakika na ubora wa pitch kwa kuwa sijaikanyaga au kuiona kwa ukaribu.Lakin mazingira mengine nje na pitch ni mabovu sana kuanzia viti hasa huku upande wa mashabiki wa Yanga,upande wa simba viti ni vizuri kwa sababu vilinunuliwa vipya baada ya mashabiki wa simba kuving'oa .

viti vichafu, vimechakaa havifai kukaliwa.pia rangi zake za kuta zimefubaa zinatakiwa zipakwe vizuri.Ngazi za kupanda juu zipo hovyo tu.hazijanakshiwa vizuri.

suala lililonikera zaidi ni VYOO.Vyoo vya uwanja ni vibovu sana.havina taa.Imagine mechi za Afcon zimechezwa usiku lakin kwenye vyoo vya kiume hakuna taa,masink mabovu yanavujisha maji.Yaani ukiingia unakutana na Bwawa la maji,ukihamia kingine hali ni ileile.Vyoo vya kike ndo viko vizuri.Wanaume wengi wanaenda kwenye vyoo vya kike kwa sababu ya uchache wa wanawake katika mechi.Hii ni hatari.

Ikiwa kuna makato kwa ajili ya uwanja,TFF na serikali kazi yao ya usimamizi wa uwanja inawashinda lakin siamini kama wanashindwa kununua taa za kwenye vyoo au kurekebisha njia za maji kwenye vyoo.Huu ni uzembe na Meneja wa uwanja anapaswa kufukuzwa hata kesho.Inasikitisha sana,pale kuna wachina wanasimania pia sasa sijui hilo hawalioni??

pia kuna changamoto nyingi sana pale yani nyingine wadau muongezee ili uwanja uwe na hadhi nzuri sawa na idadi ya watu inaobeba.Tusijisifu tu kuwa uwanja ni wa 6 kwa ukubwa Afrika lakini miundombinu ni mbovu.

sasa tunaweza kujiuliza je,pesa za makato kwa ajili ya uwanja tunayoambiwa yanaenda kufanya uwanjani au yanaishia kwenye vidomo ya wapigaji?
Ivi nani anaumiki huu uwanja..

Mechi ya sevilla na simba uwanja ulitutia aibu.

Watanzania tunasafari ndefu sana kiyafikia maendeleo.

Ivi balbu ina hitaji kipaji kuiweka au inahitaji mzungu?
 
Waswahili hatuwezi kutunza vyetu! Uwanja ulianza kutumika nadhani 2007 na leo ndio umechoka kiasi hicho! Ila na sisi mashabiki tunachangia sana uhalibifu wa viwanja vyetu! Mfano wale waliong'oa viti kipindi kile ........
Kabisa mkuu.. waswahili mambo madogo kama haya yanatushinda.
Halafu wale waliong'oa viti walipigwa faini.. Swali je ipi kazi ya mapato ya uwanja huo.
 
Afu makato ni makubwa sana.kias kwamba wangekuwa wanarekebisha kila baada ya ligi kuisha saizi ungekuwa unanga'aa.Lakin ukipita pale unaona umefubaa kama gofu la kilwa
 
Achilia mbali kujaa maji lakini hata sounding systerm ni mbovu kabisa ina mwangwi sijui wataalamugani walifunga vifaa vya matangazo pale
Sound system ni balaa sjui ilikua mwaka gani ule wimbo wa taifa uligoma kuimba ukawa unastuck stuck na ndo ukawa mwanzo wa kutumia brass band mpaka leo
 
Back
Top Bottom