mikedean
JF-Expert Member
- Mar 15, 2018
- 3,267
- 4,634
Maarufu kama kwa mkapa.Huu ni uwanja wa taifa letu Tanzania upo Chang'ombe-jirani na Chuo cha ualimu Duce au kambi ya JKT-mgulani.
Uwanja huu umejengwa kisasa lakin miundombinu ya uwanja huu ni mbovu kupindukia.sina hakika na ubora wa pitch kwa kuwa sijaikanyaga au kuiona kwa ukaribu.Lakin mazingira mengine nje na pitch ni mabovu sana kuanzia viti hasa huku upande wa mashabiki wa Yanga,upande wa simba viti ni vizuri kwa sababu vilinunuliwa vipya baada ya mashabiki wa simba kuving'oa .
viti vichafu, vimechakaa havifai kukaliwa.pia rangi zake za kuta zimefubaa zinatakiwa zipakwe vizuri.Ngazi za kupanda juu zipo hovyo tu.hazijanakshiwa vizuri.
suala lililonikera zaidi ni VYOO.Vyoo vya uwanja ni vibovu sana.havina taa.Imagine mechi za Afcon zimechezwa usiku lakin kwenye vyoo vya kiume hakuna taa,masink mabovu yanavujisha maji.Yaani ukiingia unakutana na Bwawa la maji,ukihamia kingine hali ni ileile.Vyoo vya kike ndo viko vizuri.Wanaume wengi wanaenda kwenye vyoo vya kike kwa sababu ya uchache wa wanawake katika mechi.Hii ni hatari.
Ikiwa kuna makato kwa ajili ya uwanja,TFF na serikali kazi yao ya usimamizi wa uwanja inawashinda lakin siamini kama wanashindwa kununua taa za kwenye vyoo au kurekebisha njia za maji kwenye vyoo.Huu ni uzembe na Meneja wa uwanja anapaswa kufukuzwa hata kesho.Inasikitisha sana,pale kuna wachina wanasimania pia sasa sijui hilo hawalioni??
pia kuna changamoto nyingi sana pale yani nyingine wadau muongezee ili uwanja uwe na hadhi nzuri sawa na idadi ya watu inaobeba.Tusijisifu tu kuwa uwanja ni wa 6 kwa ukubwa Afrika lakini miundombinu ni mbovu.
sasa tunaweza kujiuliza je,pesa za makato kwa ajili ya uwanja tunayoambiwa yanaenda kufanya uwanjani au yanaishia kwenye vidomo ya wapigaji?