Uchaguzi 2020 Ubunge 2020: Napendekeza wananchi wawape ajira vijana 200

Uchaguzi 2020 Ubunge 2020: Napendekeza wananchi wawape ajira vijana 200

Kabulala

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2019
Posts
695
Reaction score
936
Ni ukweli usiopingika kwamba ubunge sio tuu kuwakilisha wananchi husika lakini pia ni ajira yenye malipo mazuri na uhakika Kwa kipindi cha miaka 5

Nadhani ni wakati sasa wananchi kuanza kuwapatia fursa watu kutoka Kaya tofauti ili kuboresha Hali za Kaya watokazo.

Nasema hivi Kwa sababu nimeona mifano mingi ya wabunge ambao hawakua na ajira ya kueleweka na maisha Yao yalikua duni lakini Kwa sasa Hali zao ni nzuri Sana kiuchumi..mf ni Mbunge wa Macharii.

Sasa wananchi wakiwa wajanja wanaweza kutengeneza bilionea mmoja katika jamii zao kila baada ya miaka mitano...kuliko kulimbikiza fursa Kwa mbunge mmoja tuu miaka 10 Hadi 20...wakiwa wengi opportunities zinaongezeka pia...
 
Wazo jema, ila Usiwalemaze vijana na siasa. Waende kwenye taaluma zao, serikali iwaajiri/sekta binafsi iwe supported na serikali iweze kuwaajiri!
 
Wazo jema, ila Usiwalemaze vijana na siasa. Waende kwenye taaluma zao, serikali iwaajiri/sekta binafsi iwe supported na serikali iweze kuwaajiri!
- Usiwalemaze vijana na siasa
- Waende kwenye taaluma zao
- Serikali / Sekta binafsi iwaajiri

Hii mada kama imekuogopesha hivi[emoji1][emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo naunga mkono hoja, ubunge MTU akichaguliwa sana iwe Ni miaka kumi, baada ya hapo agombee urais au akapumzike, awaachie wengine waendelee kuchota.
 
Lengo lisiwe kuwapa watu tu ajira, tuweke lengo la kutengeneza viongozi wa baadae wenye uzoefu mkubwa na mambo muhimu ya kitaifa. Tusiangalie maslahi tu.
 
Wazo zuri....sana sio Ajira pia vijana wakiwa wengi bungeni ...tutakuwa tunapitisha vitu vya msingi ktk taifa .

Pia tusichague vijana walio chini ya degree
 
Hili wazo nilishawahi kuwa nalo wakati fulani siku za nyuma, ubunge na udiwani, vyote vitumike kama chanzo cha kupatia mitaji kwa wahusika, na hii iwe kama tabia, wabunge wote bila kujali vyama vyao watambue wapo pale kwa muda, sio kuzeekea hapo.

Hivyo wakae miaka mitano, wakishapata mitaji waondoke wakafanye biashara, wawaachie wengine nafasi, kwa namna hii tutagawanya resources kwa familia nyingi zaidi, kuliko mtu mmoja kukomalia ubunge miaka 15-20 halafu wanasifiwa wanaonekana mashujaa!.

Issue kama ni kuwakilisha wananchi, kila mwenye sifa za kugombea ubunge anastahili kuwakilisha wananchi wake, tuache hii kasumba ya kuona wengine wanastahili kukaa bungeni muda wote hata ikibidi kwenda bungeni kwa ngumi na mateke.

Hili jambo ili litokee panahitajika "civilisation" ya hali ya juu kwenye jamii yetu, kwasababu wategemezi wapo wengi sana kwa muhusika, na pia, ubinafsi kwa wabunge wenyewe naona vitakuwa tatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
How? Uoga wa nini? Unadhani nategemea kutafuta ubunge at 70 yrs? Unfortunately hatujuani humu JF!
- Fear is an unpleasant feeling triggered by the perception of danger, real or imagined (Wikipedia)

- Nchi inahitaji wanataaluma wengi zaidi kuliko wanasiasa. Unafikiri vijana 200 wakiingia kwenye siasa kutakua na madhara gani katika taaluma? ( hapa ndipo nilipouona uoga wako)

- And if that threat is real, je wanataaluma waliogeuka wajasiliamali mtaani hawasababishi madhara hayohayo?

NB: Sijaandika chochote kumaanisha kwamba wewe unampango au unategemea kutafuta ubunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi inahitaji wanataaluma wengi zaidi kuliko wanasiasa. Unafikiri vijana 200 wakiingia kwenye siasa kutakua na madhara gani katika taaluma? ( hapa ndipo nilipouona uoga wako)
Inategemea ni wataalamu wa aina gani. kama ni MDs, then they is need to worry!
 
Ni ukweli usiopingika kwamba ubunge sio tuu kuwakilisha wananchi husika lakini pia ni ajira yenye malipo mazuri na uhakika Kwa kipindi cha miaka 5...nadhani ni wakati SASA wananchi kuanza kuwapatia fursa watu kutoka Kaya tofauti ili kuboresha Hali za Kaya watokazo..nasema hivi Kwa sababu nimeona mifano mingi ya wabunge ambao hawakua na ajira ya kueleweka na maisha Yao yalikua duni lakini Kwa SASA Hali zao ni nzuri Sana kiuchumi..mf ni Mbunge wa Macharii.
SASA wananchi wakiwa wajanja wanaweza kutengeneza bilionea mmoja katika jamii zao kila baada ya miaka mitano...kuliko kulimbikiza fursa Kwa mbunge mmoja tuu miaka 10 Hadi 20...wakiwa wengi opportunities zinaongezeka pia...
Hope sio UVccm
 
Hapo naunga mkono hoja, ubunge MTU akichaguliwa sana iwe Ni miaka kumi, baada ya hapo agombee urais au akapumzike, awaachie wengine waendelee kuchota.

Na haya ndio yalikuwa matakwa yetu wananchi kwenye rasimu ya Warioba, kisha ccm wakachakachua maoni ya wananchi na kuondoa hicho kifungu. Kimsingi miaka kumi ni mwisho wa kiongozi yoyote wa kuchaguliwa, lakini akikaa zaidi ya miaka 10 kwenye nafasi moja, utakuta hana jipya zaidi ya kuendekeza hila na ubabaishaji.
 
- Fear is an unpleasant feeling triggered by the perception of danger, real or imagined (Wikipedia)

- Nchi inahitaji wanataaluma wengi zaidi kuliko wanasiasa. Unafikiri vijana 200 wakiingia kwenye siasa kutakua na madhara gani katika taaluma? ( hapa ndipo nilipouona uoga wako)

- And if that threat is real, je wanataaluma waliogeuka wajasiliamali mtaani hawasababishi madhara hayohayo?

NB: Sijaandika chochote kumaanisha kwamba wewe unampango au unategemea kutafuta ubunge.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo hata vijana mamilioni wakiingia kwenye taaluma zao, wafanya maamuzi wa ajira za hao wataalamu, ni wanasiasa hata kama ni wa darasa la 7.
 
Back
Top Bottom