Elections 2010 Ubunge jimbo la Hai

Hizo harakati na viapo vy kumng'oa Ndesa vimekuwepo siku zote lakini haijawezekana. Mimi nafikiri wafike mahali wanaompinga wakiri kwamba mzee huyu anajua kile ambacho wapiga kura wake wanakihitaji na ndiyo maana yuko mioyoni mwao. Kama aliweza kuhimili kimbunga cha kampeni za mwaka 2005, siamini kama kuna kikubwa cha kumtisha safari hii! lakini tusubiri tuone!
 

Ndesamburo anagombea hai???????,

Read the thread title before commenting
 

Kama huyu mama ana nguvu KLM kwa nn asigombee yeye apambane na Ndesa?
 
HUYO MGOMBEA wa sisi-M ambaye ANATAKA KUGOMBEA HAI LAZIMA ATAKUWA FISADI!
 
Hivi huyu viki mswilo swai ni nani? Unajua huyu mama bora angeenda kula mtori na wajukuu kuliko kuingia kwenye siasa chafu
 
Hizo hela za kujenga madaraja kuwaadaa wananchi kapata wapi?ma atazirudishaje kama cyo kufanya ufisadi

Mkuu, umesahau mtaka cha uvunguni................ Jamaa ni mfanya biashara na pia familia yao imebarikiwa kwa kuwa vijicent.Mbona ata Mbowe nae mwaka 1995 alichangia kujenga madarasa manne ya shule ya msingi Kisereni? Na yeye alikuwa fisadi au?
 
Bila ya kusahau Kanisa KKKT usharika wa Nshara,Baba yake (Mbowe) alilichangia mno mpaka awekewa kiti chake maalum...
 
na Grace Macha, Moshi


" MBUNGE wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, amesema atazisambaza kanda za video zinazoonyesha jinsi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilivyodhamiria na kujipanga kutumia nguvu kushinda ubunge wa jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba. Akizungumza na waandishi wa habari juzi mjini hapa, Ndesamburo alisema kanda hizo atazisambaza kwenye ofisi za balozi wa nchi mbalimbali zilizopo nchini.
Ndesamburo alisema mkanda huo unaonyesha namna wakazi wa mji wa Moshi walivyopigwa na wanachama wa CCM, pamoja kutolewa kauli za vitisho na viongozi wa chama hicho, wakiufananisha mji wa Moshi na eneo la vita, jambo alisema limelenga kutia hofu wapigakura wa jimbo hilo na kukiunga mkono chama hicho.
"Mbali ya kusambaza kanda hizo kwa ofisi za balozi mbalimbali nchini, pia nitapeleka kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, vyombo vya habari, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na mkuu wa wilaya ya Moshi, wajionee wenyewe hali halisi ilivyo ili baadaye yasionekane ni maneno ya uzushi," alisema.
Alisema kuwa yeye pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa tayari kushindana na CCM kwa kunadi sera zao, na si vingevyo kama ambavyo CCM wanaonyesha dhahiri kufanya mipango dhalimu, jambo alilosema si la kupuuzwa kwani linahatarisha amani.
"Mimi nayakemea kwa nguvu zangu zote na nadhani serikali nayo ichukue hatua ya kukemea yale yote yaliyotokea, na ili kuonyesha si uzushi, hizi kanda tulizirekodi nawapa nakala hizi kama ushahidi kamili, ili muone dhamira mbaya waliyonayo CCM katika uchaguzi mkuu," alisisitiza Mbunge huyo wakati akitoa nakala ya video hiyo kwa waandishi wa habari.
Matukio na kauli hizo zinadaiwa kutolewa mwishoni mwa Feberuari wakati Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Benno Malisa, alipowasimika makamanda wa vijana Mkoa wa Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Manyema mjini Moshi.
Kabla ya kusimikwa kwa makamanda hao kulifanyika maandamano yaliyopita maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi, yaliyowashirikisha viongozi wa umoja huo toka mikoa yote nchini, akiwemo mtoto wa Rais, Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa.
Makamanda waliosimikwa siku hiyo ni kamanda wa mkoa, Adam Simba, na wa wilaya nne majina kwenye mabano ni Naibu Waziri wa Ushirika , Chakula na Kilimo, David Mathayo (Same), Christopher Awinia (Hai), Seleman Mfinanga (Mwanga ) na Prosper Silayo maarufu kama Nondo kutoka Rombo.
Ndesamburo maarufu kama Ndesa-Pesa, ameliongoza jimbo hilo kwa vipindi viwili mfululizo kuanzia mwaka 2000 ambapo kwa sasa linaonekana kuwaumiza vichwa viongozi wa CCM kwa kutafuta mbinu chafu za kuweza kupata ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.
Mpaka sasa aliyetangaza hadharani nia kuwa ataomba ridhaa ya CCM kugombea jimbo hilo ni Mwenyekiti wa Wazazi CCM mkoani hapa, Thomas Ngawaiya, ingawa wapo wengi ambao hawajajitokeza rasmi.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM mkoani hapa, Godliving Mosha, alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi, alisema asingeweza kuzungumzia suala hilo kwenye simu na kwamba alikuwa kwenye kikao. Kwa upande wake, katibu wa umoja huo mkoani hapa, Yasin Lema, akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu alikanusha kutolewa kwa kauli hizo za vitisho siku ya tukio la usimikaji wa makamanda na kujigamba kuwa hata kama kuna vitendo hivyo, ushindi ni lazima. "
 


Huyu mama nae siasa zake ni za kidikteta mno.
 

Naomba kutofautiana na wewe kwenye hili,angekuwa na nguvu mama Minde asingeshindwa mara mbili...nguvu zake ziko upande wa ccm.
 

Huyu Meena wanamwandaa kwa miaka mingapi,si alishindwaga kipindi cha nyuma.
 
Yote katika yote atakayeshindana na mwenyekiti wangu awe tayari kushindwa hata kabla ya uchaguzi.
Tunahitaji kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni. Hivyo asijisumbue kwa sababu safari hii tunalinda kura zetu kwa d**u yetu wenyewe, wizi hakuna!
 

mkuu nakubaliana na wewe asilimia mia moja. Inapokuja swala la politics, kikwete, makamba, chiligati, wote hawana tofauti. Ni wapiga kelele wenye uzoefu wa kuwachota watu wawapo jukwaane. wamekuwa wazuia demokrasia na maendeleo kuliko mtu wa kawaifa anavyowezifikiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…