Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,120
- 3,468
Hivi kweli helikopta inahitajika kweli kwenye uchaguzi wa jimbo dogo kama la Tarime? Nani analipia gharama zake? Hivi haya si ndiyo marehemu Wangwe aliyokuwa anayapinga??
Wote wapuuzi. Yaani kweli Tarime wanahitaji helikopta? Wenzao wanatamba kwa kutumia mabasi kufanyia kampeni wakati sisi tunatambiana kwa helikopta! Mawazo yale yale ya wingi wa mashabiki ndio wingi wa kura. Mimi ningewasifu kama wote wangetumia baiskeli kuonyesha wanaelewa hali duni ya wananchi wao, kupunguza madhara ya mazingira na kuonyesha umuhimu wa mazoezi maana baada ya kampeni vitambi vyote vitakuwa history! Huku ni kutia chumvi kwenye kidonda na kuwadharau hao wapiga kura.
Kamanda mkuu FMES heshima kwako,Hawana njia ila ni serikali ya mseto tu ndio njia pekee ya kutokea, kwa sababu wazungu wameshamuonya Muungwana kuwa this time hawataruhusu watu wa CCM ku-cross kutoka bara na kwenda kupiga kura huko kama zamani.
Hivi kweli helikopta inahitajika kweli kwenye uchaguzi wa jimbo dogo kama la Tarime? Nani analipia gharama zake? Hivi haya si ndiyo marehemu Wangwe aliyokuwa anayapinga??
Findi Mchundo nadhani hujui sababu inayowafanya watumie Helikopta. Tatizo ni barabara na ugumu wa kufanya mikutano mingi kwa siku moja sasa ukisema watumie baiskeli si itakuwa balaa.
Kisingizio, Mkuu. Hizo barabara zimeanza kuwa mbovu leo? Kwani ni lazima hiyo mikutano mingi kwa siku moja lazima ihutubiwe na walewale? Mbona kwa wenzetu, wanagawana sehemu za kwenda na kuhutubia. Watasemaje wanajua machungu ya wananchi kama wanakwepa hizo barabara mbovu ambazo wanazitumia? Hapana, hizi ni zile zile siasa za Simba na Yanga. Zimejaa kutambiana zaidi kuliko substance. Heri wangepanda baiskeli angalau hivyo vitambi vingepunguka.
Yale mabezo ya Helicopter yako wapi sasa? Hawa CCM kwa kula matapishi yao hawawezekani? Sasa kama Chama kikongwe kinafikia mahali kinadhani kunapoteza wapenzi na wapigakura kwa ajili ya helicopter na sio uongozi mbovu basi KWISHA KAZI.KIONDOKE TUU.
Yale maneno ya Mh. Mbowe
kutotakiwa Tarime yameishia wapi?
Nasikia anajua kuzungumza kwa ufasaha kabisa lugha tatu nazo ni KISWAHILI,KISAMBAA NA KIBONDEI. Huyo ndio Katibu Mkuu wa Chama Tawala Tanzania. Hongera sana Mheshimiwa Makamba kwa kumudu lugha tatu.aibu taiweka wapi? Hatta hivyo katibu mkuu kama makamba ingetakiwa awe anajua hata lugha ya kiingereza,lakini kwa vile chama chenyewe ni CCM,then there is no need!