Ubunge Ubungo: Karata au zawadi?

Ubungo matatizo makubwa ni ukosefu wa maji, miundo mbinu hamna na ulinzi duni. Je ahadi za CCM zitatupeleka wapi? Muda wa kupata hay mahitaji ni sasa ukingoja uchaguzi uje ni shughuli.
 

Nashukuru kwa taarifa Mkuu Paparazi.

Nilisikia kuwa majimbo ya Dar yangegawanywa tangu kabla ya uchaguzi wa 2005. Sina uhakika kama ni vizuri kufanya hivyo kwa sasa au lah. Ninachokiona ni kuwa, kuna ongezeko kubwa sana ya watu katika Jimbo la Ubungo na Kawe. Maana sehemu nyingi ambazo kipindi kifupi cha nyuma zilikuwa hazikaliwi, sasa zinakaliwa kwa kasi sana.
 

Maelezo mazuri Mkuu. Ila naona umeniacha njia panda.
 

Mimi najua kura ni siri ya mpigaji, unaposema mlimpigia Mnyika.........wewe na nani ?? Don't just generalize issues na ku asume kwamba kwa kuwa kijana alijitahidi kujinadi na ukamkuli basi kila aliyehudhuria kampeni zake alimpigia kura.

Hivi ...... niulize swali la kizushi, KURA ZINAIBIWAJE ????? Nauliza hivi kwa kuwa huu umekuwa ni msamiati wa kila mara baada ya uchaguzi. Nani wanaoiba, na wanaibaje. Halafu hao wanaoibiwa wanakuwa wapi na wakati gani wanatambua kuwa wameibiwa.
 

Swali zuri sana hilo Mkuu. Hata mimi ningependa kujua jibu lake. Natumaini tutapata jibu la maana. Ngoja tusubiri.

Kuna baadhi ya wagombea ambao kwao kushindwa lazima kuwe wamedhulumiwa. Inatakiwa ifike wakati tukubali kushindwa kama ambavyo tungekubali kushinda.
 
jimbo la ubungo lina wananchi wenye upeo wa mawzo na fikira za mbali ila kila wanachokifanya ccm na serikali yake hawtaki maamuzi ya wananchi wa eneo husika hilo jimbo ni la chadema kupita kwa mnyika kwani hata mtoto wa RAIS ALIKUWA anasema ya kuwa lile jimbo ndiyo lango la mji wa dar kwa hiyo kuchukuliwa na upinzani kuna mambo makubwa yataibuliwa mule na mnyika huwa anajuakuongea kwa hoja siyo bongo lala ndiyo maana waligoma kuliachia jimbo hilo kwa mnyika mwaka 2005 ila kwa sasa hamna wakumtoa mnyika pale ubungo hata kama ccm wamecheza mchezo mchafu wa kuhamisha kata ya goba ambayo ndiyo ngome yachadema na kuingiza kata ya kigogo ambayo ccm wanaamini ni kata ya watu wao, ccm wanajisumbua kwa ubungo kwasasa kwasababu huyo nape mwenyewe anamuongopa mnyika na shamsa ndiyo hawezi hata kujibu hoja ya mnyika na vijana wake ambao kwasasa wapo kikazi zaidi n inaaminika kuwa hapa duniani kitu chenye greenty ni kifo tuuu ccm haina uwezo huwo kwasasa kuongoza ubungo hata wao wanalijua hilo ndiyo maana wanan'gang'ana kugawa majimbo ilkuangalia wapi anasimama mnyika ili wapaache habari ndiyo hiyoooooooooooooooooooo
 
wewe endelea kuwa kihiyo wa ccm mpaka mwisho wake ndiyo utajua kura zinaibiwaje 2005 alishinda mnyika kwa zaidi ya asilimia 84.5 ya watu waliyo piga kura tulijumlisha kura za vituo vyote tukatoka na matokeo mapema kabl; ya msimamizi wa ccm kutoa matokeo machafu kama kauli zako hatutaki uongo hapa jf kama huna mada be cool dnt it again.
 
Kuletewa ??? !!!!!! Wacha nikushangae kidogo. Mnaletewa na nani ?? Kwani mmlazimishwa ?????? Nawe ukitaka si kagombee.....unalalamika wakati kisu unacho mkononi !!! Usijidhalilishe wa kwetu.
100% correct.
Mwaka 1995 nilikua Ubungo na nilipiga kura kwa Lamwai wa NCCR Mageuzi. Tulilinda kura zetu hadi serikali ikaamua kufuta uchaguzi wa mwanzo. Uchaguzi wa marudio tulihakikisha pia kura zinalindwa na Lamwai akaibuka na kutangazwa mshindi.
Tatizo lenu sasa, mnakubali eti ukipiga kura nenda nyumbani subiri matokeo!
Kwanza hakikisheni mnampigia kura yule anayefaa, isije kuwa mnadanganyana tu,Halafu msikae mbali na kituo, mpeni moyo huyo wakala namchagueni wakala ambaye mnajua yuko committed kweli - hakika mtafanikiwa.
Hata uchaguzi wa Mrema kule Temeke haukuwa lelemama. Vijana wa Ubungo walihakikisha hakuna kura inayoibiwa wala sanduku linalobadirishwa-eti mnakubali masanduku yanasafirishwa bila mawakala? Poleni sana.
 
Mkuu unauhakika wanafanya wizi wa kura, weka vithibitisho hapa jamvini na si kuongea kinadharia tu.

CCM hata siku moja hawajawahi kushinda uchaguzi bila kuiba kura; hata sehemu ambayo kuna uhakiki wa wao kushinda wataiba kura ili kuongeza idadi ya ushindi wao!! Mara zote karibu na chaguzi ccm hufanya makambi ya umoja wa vijana na huko wanawafundisha vijana wao mbinu za kijasusi za kuiba kura ili wapate ushindi!! Kama sehemu wameshindwa kuiba kura basi hufanya mbinu za kuvuruga uchaguzi mfano mzuri ni wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa hapo Kawe; ishara zilionyesha kuwa CUF walikuwa wanaelekea kushinda baada ya kuona hivyo kijana mmoja wa ccm aitwae kwa jina AZIMIO akaenda na kuvuruka masanduku ya kura na kuyamwaga!! Uchaguzi ikabidi uahirishwe na yule kijana hakuchukliwa hatua zozote zile za kisheria!! Hao ndio CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…