Uchaguzi 2020 Ubunge UVCCM Arusha moto mtoto wa marehemu Mrema chukua fomu

Uchaguzi 2020 Ubunge UVCCM Arusha moto mtoto wa marehemu Mrema chukua fomu

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
753
Reaction score
1,812
Mtoto wa Mfanyabiashara Maarufu Jijini Arusha, hayati Melleo Mrema, Michelle Mrema amejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi ya Ubunge kupitia nafasi ya UVCCM Mkoa wa Arusha na kunogesha idadi ya wagombea wanaowania nafasi hiyo kufikia 29.


Michelle amekuwa mtoto pekee aliyefuata nyayo za marehemu baba yake ambaye alifariki dunia akiwa kada mwaminifu wa chama cha mapinduzi


Michelle amesema kuwa amedhamilia kuwa mbunge wa vijana Mkoa wa Arusha na iwapo chama chake kitampitisha ataweza kuwatumikia vijana vizuri kwa kuwa anaimani na Tanzania Mpya chini ya Rais John Magufuli


IMG_20200716_160823.jpg
IMG_20200716_161225.jpg
IMG_20200716_161358.jpg
 

Attachments

  • IMG_20200716_161225.jpg
    IMG_20200716_161225.jpg
    67.7 KB · Views: 2
Kina lusinde, sugu, msukuma wamefanya watu wote waone ubunge Ni kijiwe tu kama cha mtaani.watanzania tumekwisha.pale bungeni patakuwa sehemu ya kuvuna kodi za wananchi huku wakiimba mapambio.
 
mbona mzuri hiv jamani au macho yangu tu lakin nae ana tamaa mihela ya babayake yote bado anataka ubunge aachie wenzake
 
Anaonekana anaweza ajilinde na zitto maana zitto kwa kupokea wabunge vijana hajambo, mzee bulembo hadi leo analia tu maana mwanae alidakwa na zitto kimasihara
awamu hii anaweza asirudi bungeni hivyo kuwa salama yake binti.
 
Ila hapo unaposema Marehemu Mrema alikuwa Kada muaminifu nadhani ni hisia zako tu...Jamaa yule alichokuwa anajua ni kutafuta pesa tu Watu wa chama ndio walikuwa wanamwambia "scratch our back and we will scratch your's" akawa analazimika kuchangia hapa na pale..lakini hakuwa muumini kabisa wa siasa yule.

Na hao Watoto mali alizoacha Mzee zimewaelemea sasa sijui kwenye siasa huko wanatazamia nini......ngoja tuone.
 
Halafu hajavishwa bado pete dadadeki, CCM kuna visu balaa ...
 
Back
Top Bottom